Nape Nnauye na John Chiligati - chema chajiuza, kibaya chajitembeza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye na John Chiligati - chema chajiuza, kibaya chajitembeza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, Apr 28, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimeshtushwa na naendelea kushangazwa jisi Nape Nnauye na John Chiligati wnavyoendelea kuibomoa CCM kufuatia hatua yao ya kuzunguka mikoani kujinadi kuwa wanajivua gamba, nashindwa kuelewa kwnini wanazidi kumaliza hela za chama kwa jambo lisilo na mantiki? Ndiyo hakuna mantiki hata kidogo ya wao kuzurura hovyo kwa maana wenye busara washaanza kuhoji hii ina faida gani?

  Watanzania wanataka kuona mafisadi wanapelekwa mahakamani basi sio kelele za propaganda, wao watulie wawaadabishe hao mafisadi then watanzania wataona bila kuambiwa kuwa CCM imezaliwa upya hizi tambo za Nape na Chiligati hazihitajiki na hazijengi CCM hivyo zikomeshwe kabisa.

  Kwa jinsi mambo yanavyoendelea naanza kuamini kale kamsemo ka wahenga kuwa kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.


  Acha ukweli usemwe, usiposemwa hakuna atakayekasirika hapa......(Tuntemenke Sanga)
   
 2. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Tafadhali naomba, nafikiri na wengine wengi tu watakuomba, badilisha rangi ya font za post yako. Rangi uliyotumia inaumiza macho ya wasomaji. Ni ushauri tu!!!!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kambota

  inawezekana kabisa CCM wame-underspend ndio maana akina nape wanazunguka kuuza dhana ya kuvua magamba:lying:
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Allowance za safari tu zinawasumbua
   
 5. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape usife moyo, sisi wa mikoani tunafarajika na vijembe unavyovitoa, tena mje na TOT katika msafara wenu, waje watuimbie NAMBARI ONE EH!!!!
   
 6. O

  Okinawa Senior Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Msanii JK ameishawashangaa akina Nape kwa spidi waliyochukuwa baada ya mkutano wa NEC Dodoma na yeye ameanza kujitoa kwao kisirisiri na kuwasiliana na MAFISADI.

  Ushauri wa bure kwa Nape: CCM hawana dhamira ya dhati ya kupambana na UFISADI kwani karibia wote ni MAFISADI akiwemo na Mwenyekiti, kwa hiyo hatua unazochukuwa kuzunguka mikoa kuwambia wananchi kwamba CCM imeamuwa kuwafukuza MAFISADI uzichukuwe kwa tahadhari kubwa la sivyo ita-fire back kwako; si uchaguzi ni mwakani utaona MAFISADI watakavyochukuwa nafasi za juu katika chama.

  Na hapo ndipo utakapojua kwamba Mwenyekiti wako ni MSANII na hana dhamira ya dhati ya kupambana na UFISADI kwani hata yeye unamzunguka.
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Msiwasahu The comedy na Futuhi.
   
Loading...