Cheka ya tshs 400 vodacom haina maana!

kulyanganga

Member
Nov 13, 2012
60
20
Wanajukwaa angalieni vizuri hii promotion ya cheka si halisi mfano siku chache zilizopita nilijiunga niliongea kwa dk 4 tu saa mbili usiku wananitumia meseji eti kifurushi chako cha TSH 400 kimekwisha sasa ina maana gani mtandao mkubwa kama huu kuwadanganya wateja? au dhana iko wapi ya unafuu wa mitandao ya simu nchini! mamlaka husika waangalie kwa umakini ikiwezekana hata wao wajiunge wajionee huu uongo!

maoni tu!
 
waweke kwa siku moja. Km ulijiunga saa 6 leo iwe mbaka kesho saa 6
 
mtandao ni mmoja tu Tanzania,vodacom hao wengne wanasubiri,hata kama wakiiba poa tu lakin network haizngui kama mitandao hyo mingne
 
vigezo na masharti kuzingatiwa. cheka inaisha saa 5 na dakika 59 usiku hata kama umejiunga saa 5 na dakika 58 ikifika 6 kamili usiku inakwisha.
 
wewe unasema inaisha haraka ulishawai kuchunguza kwamba cheka zote ni za dakika na sio sekunde maana ukipiga dakika moja na nusu ukija cheki salio utakuta dakika mbili wamekata, sasa huo si uwizi ni nini?
 
Hapo umelonga mkuu,kwanza gharama zao nafuu na mtandao ni wa uhakika,vodacom ni kiboko yao.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
vigezo na masharti kuzingatiwa. cheka inaisha saa 5 na dakika 59 usiku hata kama umejiunga saa 5 na dakika 58 ikifika 6 kamili usiku inakwisha.

Wanajukwaa angalieni vizuri hii
promotion ya cheka si halisi mfano siku
chache zilizopita nilijiunga niliongea
kwa dk 4 tu saa mbili usiku
wananitumia meseji eti kifurushi chako
cha TSH 400 kimekwisha sasa ina maana gani mtandao mkubwa kama
huu kuwadanganya wateja? au dhana
iko wapi ya unafuu wa mitandao ya
simu nchini! mamlaka husika waangalie
kwa umakini ikiwezekana hata wao
wajiunge wajionee huu uongo! maoni tu!
 
wewe unasema inaisha haraka ulishawai kuchunguza kwamba cheka zote ni za dakika na sio sekunde maana ukipiga dakika moja na nusu ukija cheki salio utakuta dakika mbili wamekata, sasa huo si uwizi ni nini?
aisee wewe umenifumbua macho. kwahyo cheka ni dk kumbe na si sekunde. juzi nilishangaa mbona inaisha mapema nilipiga nikaongea sekunde 20 kuangalia imekata dk nikashindwa kuelewa. kweli vigezo na masharti kuzingatiwa. kaaaa....
 
Wafanyakazi wengi wa voda wamewekwa na viongozi wa CCM! SASA UNATEGEMEA..............
 
Wanajukwaa angalieni vizuri hii promotion ya cheka si halisi mfano siku chache zilizopita nilijiunga niliongea kwa dk 4 tu saa mbili usiku wananitumia meseji eti kifurushi chako cha TSH 400 kimekwisha sasa ina maana gani mtandao mkubwa kama huu kuwadanganya wateja? au dhana iko wapi ya unafuu wa mitandao ya simu nchini! mamlaka husika waangalie kwa umakini ikiwezekana hata wao wajiunge wajionee huu uongo!

maoni tu!

Mara nyingi,MSG hizo,hutokea,lakini hazina maana. Unaweza ukajiunga hiyo cheka ya 400/=,kabla hata hujaitumia hata DK 1,unapata MSG ya namna hiyo. Ila,ukiangalia salio la hiyo cheka (*147#),haitakuwa imepungua,kwa kiasi ambacho hujatumia. Hivyo nawe,inawezekana,SALIO lako halali,lilikuwemo!
 
Hamia Tigo japo ni 450 lakini ni 24hrs pia wanakupa sekunde 900 ambazo ni sawa na dk15 hivyo wanakukata kwa sekunde, kwa wizi wa reja reja Vodacom Tanzania hawajambo........
 
Wanajukwaa angalieni vizuri hii promotion ya cheka si halisi mfano siku chache zilizopita nilijiunga niliongea kwa dk 4 tu saa mbili usiku wananitumia meseji eti kifurushi chako cha TSH 400 kimekwisha sasa ina maana gani mtandao mkubwa kama huu kuwadanganya wateja? au dhana iko wapi ya unafuu wa mitandao ya simu nchini! mamlaka husika waangalie kwa umakini ikiwezekana hata wao wajiunge wajionee huu uongo!

maoni tu!

kuwa makini hasa pale unapopokea sms yako ya kukubaliwa ombi lako, wakati mwingine huwa inakuwa ya kukataliwa kulingana na sababu zao..tuliowengi tukishatuma ujumbe, sms ya majibu hatuisomi tunaifuta tu...usipende kujiunga bila kuhakikisha kifurushi chako cha awali kimeisha.!
 
kuongea na kutuma sma - TIGO haina mpinzani

kwenye internet - ZANTEL ni nomma

VODA na AIRTEL ni za kuzitumia kimachale
 
Back
Top Bottom