Cheaters Reality TV show; ikifika Bongo kutakalika??

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Mara moja moja ninapopata muda, nimekuwa nikiangalia kipindi cha Cheaters kinachorushwa kupitia DSTV. Maelezo kuhusu kipindi hiki pia yanapatikana kwenye hizi links.

Cheaters | REAL Reality TV

Cheaters - Wikipedia, the free encyclopedia

Cheaters (TV Series 2000

Pamoja na kwamba kipindi hiki kinaelezwa kuwa kinawasaidia wahanga wa matukio ya kuibiwa wenzi wao kuujua ukweli, binafsi naona kwamba kuna madhara mengine mengi yanayowapata wahusika wa hizo fumanizi.

Je, kipindi hiki kikianzishwa hapa Bongo, kitapokelewaje na usalama wa wahusika utaweza kulindwa katika mazingira haya ya kitu kidogo?

Babu DC!!
 
Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
28,035
2,000
Hivi, ile kitu wanafanya kweli ama kuna kuact kidogo?
Ikija hapa watu lazma wauane..,
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Kwa Tanzania haiwezekani kukianzisha kwa sasa!

Tulishawahi kupeleka maombi ili kuanzisha hicho kipindi kwenye wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na pia katika Wizara ya Mambo ya Ndani tulichoambulia ni kuwekewa masharti na vikwazo ambavyo vilitufanya kushindwa kuendelea na mpango huo kwa kuhofia kushitakiwa na serikali kupitia waathirika kitu ambacho kingepelekea hata kukosa wadhamini wa kipindi.

Sheria haziwalindi waendesha kipindi na hata research yetu ilionesha jamii ya Kitanzania haijafikia kiwango cha kuwa wavumilivu katika maswala ya kinyumba na mahusiano na kwa sababu hiyo kuna uwezekano kipindi kingeleta athari hasi kubwa katika jamii badala ya kuijenga.
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Hivi, ile kitu wanafanya kweli ama kuna kuact kidogo?
Ikija hapa watu lazma wauane..,

Ukifuatilia kwenye kwenye link ya pili, kuna madai kwamba kuna episodes zinatengenezwa kwa maigizo. Hata hivyo, waandaaji wanakana hizo tuhuma.

Babu DC!!
 
Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,269
2,000
Kwa Tanzania haiwezekani kukianzisha kwa sasa!

Tulishawahi kupeleka maombi ili kuanzisha hicho kipindi kwenye wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na pia katika Wizara ya Mambo ya Ndani tulichoambulia ni kuwekewa masharti na vikwazo ambavyo vilitufanya kushindwa kuendelea na mpango huo kwa kuhofia kushitakiwa na serikali kupitia waathirika kitu ambacho kingepelekea hata kukosa wadhamini wa kipindi.

Sheria haziwalindi waendesha kipindi na hata research yetu ilionesha jamii ya Kitanzania haijafikia kiwango cha kuwa wavumilivu katika maswala ya kinyumba na mahusiano na kwa sababu hiyo kuna uwezekano kipindi kingeleta athari hasi kubwa katika jamii badala ya kuijenga.

Kweli kabisa, kuna mambo mengi kwenye jamii yetu ambayo kwa namna nyingi yanafanya uendeshaji wa kipindi kama hiki uwe mgumu sana.

Ila jingine ni kuwa baadhi ya wakubwa wanaosimamia hata media ndiyo wateja wakubwa wa mambo ya kutembea nje ya ndoa zao. Watakuwa tayari kuruhusu kitu ambacho kinahatarisha maisha yao wenyewe na au washirika wao??

Babu DC!!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,779
2,000
Babu cheaters haina madhara kama jerry springer's show. Hatareee.
Uzuri wa ndoa za kibongo ni mahaba niue. Kwanza anaesifiwa ni mwanume smart ambaye anajua kuficha mambo yake. Ila ndo ukiwa na mume mmasai kila siku anarudi saa nane usiku unaconclude mwenyewe tu. Huhitaji kumlipa mtu a dime akuhakikishie
 
Hivi Jerry Springer's show ina ukweli wowote?
Mbona naona watu wanact tu, ama ni mie..
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Babu cheaters haina madhara kama jerry springer's show.

We nawe uko mshamba mshamba wakati mwingine. Kipindi cha Jerry kina madhara gani?

Jerry yupo hewani kwa zaidi ya miaka 20 na nimeanza kumwangalia kwa zaidi ya miaka 16 iliyopita na mpaka sasa sijaona madhara yoyote yale zaidi ya burudani na ku highlight vijimambo vya waja katika baadhi ya sehemu za jamii ya Kimarekani!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,779
2,000
We nawe uko mshamba mshamba wakati mwingine. Kipindi cha Jerry kina madhara gani?

Jerry yupo hewani kwa zaidi ya miaka 20 na nimeanza kumwangalia kwa zaidi ya miaka 16 iliyopita na mpaka sasa sijaona madhara yoyote yale zaidi ya burudani na ku highlight vijimambo vya waja katika baadhi ya sehemu za jamii ya Kimarekani!

Wewe ushadhurika, utaonaje madhara yake? Hebu niondokee hapa na ujuaji uchwara wako. You should be on the show kwanza.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Unaniita mie mshamba na yet 'hudhani'! Hahaha I will spare you on this one.

Ndiyo, una ushamba ushamba. Eti Jerry Springer kina madhara....good lawd.

Hiyo sidhani inamhusu niliyemnukuu, kwamba, sidhani hata yeye anaweza kudai kuwa zile ngumi ni za ukweli.

Comprehension, comprehension, comprehension, please.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,779
2,000
Madhara yake ni yepi? Yaorodheshe hapa pamoja na wahanga wake.

Weeh mmasai kweli. Hahaha eti na wahanga wake wote niorodheshe. Hivi umejifikiria sawasawa kabla ya kuuliza hilo swali? Lmfao, ujuvi wako ni wa aina yake. 16 yrs of watching it and that is what you ask? Khaaa
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Weeh mmasai kweli. Hahaha eti na wahanga wake wote niorodheshe.

Wapi nimeandika wahanga wake "wote"? Unaota au unaona maruweruwe? Unapenda sana ku comment comment vitu ambavyo hata huna uelewa navyo mzuri. Ili iweje sijui....uonekane na wewe unajua sana yajiriyo Marekani au?

Hivi umejifikiria sawasawa kabla ya kuuliza hilo swali? Lmfao, ujuvi wako ni wa aina yake. 16 yrs of watching it and that is what you ask? Khaaa

Umeshindwa kutaja madhara na umeshindwa kumtaja mtu hata mmoja aliyedhurika. Usijichekeshe...hiyo ni dalili ya kutokuwa na jibu/majibu ya swali/ maswali yangu.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,779
2,000
Wapi nimeandika wahanga wake "wote"? Unaota au unaona maruweruwe? Unapenda sana ku comment comment vitu ambavyo hata huna uelewa navyo mzuri. Ili iweje sijui....uonekane na wewe unajua sana yajiriyo Marekani au?Umeshindwa kutaja madhara na umeshindwa kumtaja mtu hata mmoja aliyedhurika. Usijichekeshe...hiyo ni dalili ya kutokuwa na jibu/majibu ya swali/ maswali yangu.

Hahaha kumbe kichwani kwako unajiskia unaijua hiyo show kwa sababu uko marekani? Dunia kijiji haikuhusu wewe? Hebu nipishe na stress zako za sikukuu. I don't have to have answers for silly questions. Kuna vitu navitaftia majibu kwa dhati na haya maswali yako hayamo kwenye list. We all know wewe ni mjuaji 20 times than me NN. Why all the fuss sugar boy?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom