Cheap popularity?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,205
Reaction score
866,461


Simlaumu katu Mzee wetu Dr. Shika... Naye ni mhanga wa chama chawala.! Na madhila yake ya kuondoshwa Urusi ccm inahusika na balozi wake kwa wakati huo amekiri kumuondosha Dr shika wakati huo kwa hati ya dharura na pengine kwa maelezo ya kisheria PI (prohibited Imigrant)

Kabla ya mnada wa nyumba za Lugumi (kizungumkuti cha aina yake) Dr shika hakuwa lolote... He was nobody.. Akiishi kwa msaada wa msamaria mwema... Na baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 kama masharti ya mnada yanavyosema alikamatwa na kusweka lupango..

Kamanda wa polisi mbele ya vyombo vya habari akautangazia uma kuwa Dr shika alikuwa si chochote si lolote na hana thamani hata ya shilingi za kitanzania million moja sawa na dola Mia NNE za kimarekani...! Tafsiri yake ilikuwa moja tu kwamba kumbe watanzania sasa tunapimana thamani kwa viwango vya fedha...! [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji47] so sad... Lakini pia mamlaka zetu zina inteligensia ya mizani ya kupima utu wa mtanzania kwa viwango vya fedha... Tumefika pabaya

Ukisoma kitabu cha Mchonga.. "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania.. " unaweza kudhani yule Mzee alikuwa nabii ama mbeba maono... CCM wanakikwepa sana hiki kitabu....!!! Utaona wazi kilichoandikwa wakati ule na Mchonga ndio kinatokea sasa...

Shaka Dr msomi si wa kumlaumu mwache atumikie kafiri... Apate mradi wake.. Mkono uende kinywani... Tumbo lijae miguu imwongoze maliwatoni... Tumbo la njaa haliendi chooni....

Cha kushangaza kuchekesha na kuudhi sana kama si kutia simanzi ni eti sasa Dr shika ni muhimu sana na wa thamani sana KIASI cha kutumika kwenye kampeni za uchaguzi ili achangie kuleta ushindi kwa ccm,.... Shika huyu huyu mtuhumiwa aliyelazwa mahabusu saa 72 bila dhamana....!!!!

Akishatumika(pengine ameshatumika) atatelekezwa kama toilet paper chooni... Lakini je tujiulize hapa ndipo ccm ilipofikia? Sijajadili ya gulio la madiwani wabunge na viongozi wengine wa upinzani.... Mostly CHADEMA..!!!
 
Angekuwa na chadema ungelalama hivi?? Mbona ufipa inawauma sana kumwona shika akiwa ccm..
 
Hivi chadema mna akili kweli? Hiyo democrasia mnayosemaga iko wapi kama kila mtu akiwa upande ule mnaanza kumtukana?
 
Angekuwa na chadema ungelalama hivi?? Mbona ufipa inawauma sana kumwona shika akiwa ccm..

Hivi chadema mna akili kweli? Hiyo democrasia mnayosemaga iko wapi kama kila mtu akiwa upande ule mnaanza kumtukana?
Enyi ngurumbili mso maarifa mkishindwa kuelewa muktadha wa mada msione aibu kuuliza mtaeleweshwa
 
mi nikiyakuta yanayoihusu sisiem nachefuka tu! nishaishiwa hoja make siwaelewi "asilani abadani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…