Chawa, bado wapo?

Kuna wale wa kwenye nguo na wa kichwani; kizazi hiki wanajua chawa ni nini?

Nini chanzo cha chawa? Uchafu tu?
Kuna bahadhi ya maeneo chawa ni kawaida, kama Magerezani na pale Ubungo Bus Terminal kwenye jumba la kupumzikia wageni, ukikaa pale ni lazima uondoke na mifugo, kama sio chawa basi kunguni.

 
Hahahah.....nahisi we tulikuwa tunawaza pamoja! Mara hii tu nimetoka kumwambia mtu abadili nguo maanake ilivyochafuka, duh awezapata hata chawa aisee!
Kipipi,

Nilikaa na kujiuliza kama wadudu hawa bado wapo!
Kuna bahadhi ya maeneo chawa ni kawaida, kama Magerezani na pale Ubungo Bus Terminal kwenye jumba la kupumzikia wageni, ukikaa pale ni lazima uondoke na mifugo, kama sio chawa basi kunguni.
Michael Scofield,

Na chawa wa kichwani pia? I see hahahaha
 
Last edited by a moderator:
Maeneo ya vijijini ambayo kuna vumbi sana bado wapo..unataka kuwafuga nikuletee?:lol:
 
JKT ikirudi na chawa watarudi.

Ila wahindi na waarabu nadhani bado wanao!

So unamaana siku hizi watu ni wasafi kuliko zamani?
Au sabuni na maji ilikuwa shida? Mnaonaje kama hii ni case tumpe credit for once JK kwa kuweza tokomeza chawa!
 
chawa na kunguni vijijini bado watakuwepo ila watakuwa kwa kidogo, shule na usafi umesaidia,

asikwambie ulale kitanda cha kunguni, enzi hizo kusalimia kijijini...

je, hivi na funza wa miguuni bado wapo?
 
Invisible hawa jamaa walikutesa sana nini?
Enzi zile nilikuwa napenda sana kutafuta watu chawa kichwani. utoto kazi sana, siku moja si nikajiweka chawa mmoja ili azaliane kichwani kwangu. nilikuwa na nywele ndefu sana na nilikuwa nazipenda. chawa wakazaliana, kilichotekea, nilipitishwa mkasi bila majadiliano, nilikoma.
watoto wetu siku hizi sidhani hata kama wanajua kuna viumbe kama hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Si chawa tu, hata Utitiri ukiwauliza kizazi hiki cha Dot.com , hutopata majibu toshelevu.
Hili la Utitiri sababu yake kubwa ni kwamba wengi wa wazazi wa sasa wanaishi nyumba za kupanga, hivyo kufuga Kuku inakua ni nadra sana.
Na wale wanaoishi kwenye majumba yao wamepoteza silka ya kufuga Kuku wa asili, na Utitiri haupatikani kwengine zaidi ya Kunako Kuku asili. Hata hapa Jeiefu lazima watakuwepo tu wasiojua ninachokisemea hapa.
 
hahahahahah Invisible usinikumbushe......

enzi zile nikiwa na miaka kumi na kitu hivi, nahisi nilikuwa 10 au 12
tulipata mgeni ikabidi niwe nalala nae...
kumbe mgeni ana chawa.......
siku moja nikamuomba sista anifumue vijirasta vyangu karibia shule inaanza hamadiiiiiii kaona mayai.....kupekenyua kakutana na chawa...
akaniambia BADILI TABIA una chawa weweweeeeeeeeeeeeeeeeeeee
:A S 20:nililiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa:A S 20: nikaliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa :A S 20:nakuliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa:A S 20:

kumuuliza mgeni akasema "mbona hao kawaida, nyumbani wote tuna chawa"

nashukuru mama alivyorudi akashughulikia loh!!!!


toka siku hiyo hata uje mgeni toka mbingu ya saba silali na wewe ng'ooooo.... watoto wangu pia siwalazi na mtu except mama yangu au ndugu zangu wa tumbo moja......
 
bado pia kunguni...........
mie mwenye ngozi mbovu........
waliwahi kunikumba kitambo nikiwa kijijini...
nyumba nzima najikuna mie tu, navimba mie tu, usiku silali......... wenzangu wote wako poa sijui watu wengine wana ng'ozi za tembo........

i see Invisible umenikumbusha mbali isee

mpaka home wakawa wananiita "kipimo" popote niendapo kama kuna kunguni hata nyumba nzima wasipojikuna na kuvimba, mie ndo nitawashwa na kututumka.....

kwa sababu hii trip za kutembelea ndugu mie zilikuwa zinanipita kando...
ngozi yenyewe hii ya kuazima
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom