Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kimepokea wanachama wapya 250 kutoka Jimbo la Kinondoni leo Jumapili, Julai 27, 2025 wakati chama hicho kilipofanya mkutano mkuu wa jimbo hilo.
Sera za chama, kushiriki uchaguzi, mabadiliko ni miongoni mwa sababu zilizofanya chama hicho kupokea wanachama wapya jimboni hapo kama alivyosema Katibu wa Jimbo la Kinondoni Chaumma, Amon Mwakasege.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chaumma, Salum Mwalimu amesema hakina hiyana, ugomvi wala chuki na yeyote bali hasira za chama hicho zipo pale Watanzania wanapodhulumiwa haki zao.
"Chaumma hatuna shida na tunatamani tuwe daraja la kuunganisha vyama vyote. Sisi hatuna unyonge. Hatuna chuki, hasira zetu zipo pale Watanzania wanapocheleweshewa maendeleo yao," amesema.
Amesema akitokea kiongozi yeyote wa upinzani anayewahamasisha Watanzania kupiga kura wao Chaumma hawana shida naye.