CHASO,Tanga wakana Uasi: Waunga mkono Zitto kutimuliwa CHADEMA

molemo,
kazi unayoifanya ya kukinga maji kwenye gunia itakutesa sana. subiri kidogo tu utaona matokeo ya mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya saccos ya mtei. ni kama cuf baada ya kumfukuza hamad rashid. hata uchaguzi wameshindwa kufanya, hakuna watu. chadema falls the same line
 
chaso vyuo vikuu tumewasikia, chadema tanga tumewasikia, geita chadema tumewsikia na mbeya wamezipiga live, mleta mada kalale, malizia usingizi wako
 
Sisi tunauliza kwanini hamuwafukuzi Zitto, Kitila Mkumbo na wote wanaowaunga mkono?

Mnaogopa?
 
Sasa hivi naona harakati ndani ya chama zimesimama na kelele za mjini sasa hivi ni Zitto na Mkumbo.
Mda unaenda tu
 
TANGA WAKANA UASI
Kwa upande wake, Chadema Mkoa wa Tanga kimekemea viongozi waliyoibuka kupinga maamuzi ya Kamati kuu ya kuwavua nyadhifa Zitto na wenzake na kwamba kitendo hicho ni kinyume cha Katiba ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, alikemea viongozi hao kuwa wanakiuka katiba kifungu cha saba ibara ya saba na 16 (V) inayoipa mamlaka na uwezo Kamati Kuu ya kuteua na kumuondoa mtu yeyote atakaebainika kwenda kinyume cha katiba.

Bahweje alieleza kuwa viongozi hao wanatenda kosa la kikatiba na kwamba hawana haki ya kuhoji wala kukosoa kilichotendeka kwa kuwa wao ni ngazi za chini, hivyo hawawezi kutengua maamuzi ya chombo kilichopo juu yao.

CHASO YAONYA
Shirikisho la Wanachama wa Chadema Vyuo Vikuu (Chaso) Mkoa wa Dar es Salaam, limesema watu wanaojitokeza hivi sasa na kutoa matamko yanayopinga uamuzi wa kumvua Zitto na wenzake nafasi za uongozi wanatumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mratibu Mkuu wa Chaso, Elihuruma Jackson Himida, alisema hayo jana alipozungumza na NIPASHE na kusema katika kutekeleza mbinu zao alizoziita ‘chafu’, watu hao wamekuwa wakijitambulisha kuwa ni wanachama wa Chadema wakati siyo kweli.

Alisema Chaso itatoa majibu leo kuhusiana na matamko yanayoendelea kutolewa na watu hao ili Watanzania wajue ukweli halisi wa kile kinachoendelea juu yao.

Alisema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Sekretarieti ya Chaso, kilichofanyika jana kujadili watu hao, ambao alisema hawamo hata kwenye kumbukumbu za Chadema kuwa ni wanachama wake, lakini wanashangazwa kuona waandishi wa habari wakiwashabikia.

Kauli hiyo ya Elihuruma imetolewa siku moja baada ya juzi watu waliojitambulisha kuwa ni wanachama wa Chadema, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kile walichokiita mgogoro wa kiutawala kati ya wapigania demokrasia na wahafidhina ndani ya chama hicho.

IRINGA WANENA
Katika hatua nyingine, Chadema katika mikoa ya Iringa na Tanga kimeunga mkono hatua ya Kamati Kuu kuwavua nafasi za uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto na wenzake.

Zitto alivuliwa uongozi Ijumaa iliyopita sambamba na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, kwa tuhuma za kukisaliti chama.

Wote wanatuhumiwa kuandaa waraka ambao ulikuwa na tuhuma dhidi ya chama na viongozi wake ngazi ya taifa.

Chadema mkoa wa Iringa kimesema hatua zilizochukuliwa na Kamati Kuu dhidi ya viongozi hao ni sahihi.

Mjumbe wa Kamati ya Uendaji wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Abdu Changawe, aliwaambia waandishi wa habari mjini Iringa jana kuwa chama hicho kinaongozwa na katiba na kama mtu yeyote atakayehusika kutoiheshimu katiba hiyo, lazima katiba itamshughulikia kikamilifu.

“Kutokana na tabia zao za usaliti ndani ya chama sisi kama wanachama wa Chadema Iringa tunapongeza maamuzi yote na pia tunatoa msimamo wetu kuwa yeyote aliye na tabia kama hiyo ajirekebishe haraka kabla sheria haijachukua mkondo wake,”alisema Changawe.

Aidha, alisema kuwa chama hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa haki inatendeka sehemu zote na pia wamejipanga kuwa tayari kutokumbatia uovu wa aina yoyote kwani mafanikio ya chama mpaka sasa yamegarimu damu za watu, mali za watu na hata wengine kufungwa magerezani.

Source:Nipashe Ijumaa
Bado tamko la kanda ya kaskazini na misukule group
 
molemo,
kazi unayoifanya ya kukinga maji kwenye gunia itakutesa sana. subiri kidogo tu utaona matokeo ya mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya saccos ya mtei. ni kama cuf baada ya kumfukuza hamad rashid. hata uchaguzi wameshindwa kufanya, hakuna watu. chadema falls the same line

Kama ni hivyo nyie CCM mnatakiwa kufurahi na kushangilia..

Sasa mnanuna nini?
 
Jana kupitia radio Mlimani saa 10-11:00 jioni Mnyika alikuwa studio na kusema kweli nilipenda alivyoongea na kuiongelea CDM

Alisema usaliti ni sawa na jipu ama kansa dawa yake ili isisambae mwili mzima ni kukata kiungo na jipu ni kulitumbua kutoa usaha nje na
Kwamba CDM ikifikia hatua ya kumchukulia mwanachama hatua kama hizi ni kwamba inakuwa imeshindikana kwa jitihada zingine huko nyuma,kwahiyo hizi ni za mwisho
Lakini hata wakati wa kupiga simu kila mtu aliipongeza CC ya CDM kwa kuchukua hatua.
 
ukitaka kugundua ni project ya ccm, angalia mtamdaoni wanaokereka kwa kutimuliwa akina mkumbo ni nani?utakuta ni ID zile zile zinazopingana na chadema, unajiuliza,kama hawaipendi chadema, na chadema imewatimua waandamizi wake mabingwa, hawa watu walipaswa kulia au kufurahia? no way, ccm na supporters wake wananufaika na wasaliti wa chadema kubaki chamani...mwanzo nilinuna kuona dr kitila naye kanasa wakati tulitegemea akamkimbize nchemba kule singida..ila niliposoma magazeti, nkaja jf nkarudi kwenye mitandao ya ccm, ya nchemba na waandamizi wengine...wooote wanalia na kusaga meno kwa kuondokewa na wasaliti chamani...nkaona kweli kuna mirija ya ccm imekatwa....kwa nini kama hawa walikuwa mwiba kwa ccm leo badala ya akina ff, hamy d, ritz, zer marcop, chili wa majuu, n.k kufurahi, wanalia na kupata homa ya matumbo wakati cdm waliokuwa wana hawa wanachama wanacheklelea saaanaaaaaaa! Tafakariiiiiii
 
Huyo ndiye John Mnyika..

Naibu Kiongozi wa upinzani bungeni tunayemtarajia..
 
Mkuu wangu hawa watu hawana chao tena.

Mtu anapotaka kukata roho anarusha mateke na ngumi..
 
Back
Top Bottom