so hiyo court ina mipaka ipi? ni kwamba lazima kiongozi awe kaua wananchi wake pekee, au akiwa kaiba hela anashtakiwa pia au niaje...mipaka iko mpaka wapi...maana tuna akina mugabe, museven. hapa kwetu zenj walishaua watu, pale magomeni kulishatokea vurugu wananchi wakafa, arusha juzi juzi tu so nataka nijue vikwazo wanavovitumia huko hague kwenye kukamata na kushtaki viongozi. Kumbuka hawa viongozi wanaopelekwa huko ni wale ambao walishapigwa chini na wananchi wao so wanakua sio powerful tena...But having said that sioni haja ya kumkamata kiongozi wa nchi yetu aliyeua watu50 wakati kuna kiongozi wa marekani aliyeua watu zaidi ya 100000 na hakamatwi ndio kwanza anapeta huko texas:A S angry:
Malipo ni hapahapa duniani....huyu anahusika na vita vya Siera leone vilivyouwa maelfu ya watu na pia anahusika naWakuu nimekuwa nafuatilia hii kesi ya Taylor japo mimi sio mwanasheria lakini nimekuwa navutiwa sana na jinsi kesi inavyoendeshwa hasa defensive lawyer Courtenay Griffiths ni makini sana japo hii kesi kushinda si rahisi . Leo hukumu inasomwa live on CNN na Judge Richard Lussick japo yeye Taylor amekana mashtaka yote na kusema yeye ni mwathirika wa njama za wabaya wake.
Binafsi kwajinsi ya uhalifu na mauaji yaliyofanyika Sierra lione wakati wa utawala wake huyu jamaa ana kesi ya kujibu.
Taylor amekutwa na hatia ya kufadhili vikundi vya uasi kwa diamond smuggling, kuvunja haki za binadamu-sexual slavely,child soldiers. Kuhusu vigezo wanavyotumia ICC kumshtaki mtuhumiwa sina uhakika lakini kwanza lazima nchi iwe imesaini mkataba wao.
Wondering why Taylor's trial was conducted by special court for sierra leone and not ICC (permanent tribunal) for crime against humanity? Msaada wanasheria.
Taylor hajahukumiwa ICC, bali na special court for sierra leone kama mahakama Arusha ya mauji Rwanda.
Marekani wajanja, wao mpaka Leo hawajasaini statute inayotambua mahakama ie ICC, kwa Hali hiyo bush hawezi kushitakiwa. Viongozi wetu walirubuniwa na vihela wakasaini haraka haraka. Kumbe wao ni potential victims.
Hapo sasa tusubiri uamuzi wa mahakama
Wajanja ama Wanafiki/Mahabithi?
Kila neno lina maana na upeo wake kamilifu. Ujanja ni halali na huweza kuleta faida kwa binadamu na huweza kurahisisha mambo yaliyo, venginevyo, ni magumu kuyatekeleza. Mjanja haadhibiwi isipokuwa ujanja wake huelekezwa kufaidisha watu. Unafiki na Uhabithi ni haramu na hauleti isipokuwa ufisadi, fitna, chuki na umwagaji damu kwa binadamu. Mnafiki anatakiwa aadhibiwe.
Tatizo ni nyiyi mnaobadilisha lugha, Wanafiki/Mahabithi mnawaita wajanja, na wajanja mnawaita Magaidi kwasababu Wanafiki/Mahabithi wamewaita na kukulazimisheni kuwaita hivyo. Mungu atupe maisha marefu kidogo, utawaona Wanafiki/Mahabithi wataporomoka na Wajanja watanyanyuka.
jamani mfuatilien Taylor vzuri,alipandkizwa na USA kule,ni CIA,labda kwa vile wamarekani ndo zao wakishakutumia wanakutupa kama kondomWamarekani walijua haya wajiepusha nayo, ukweli ni kwamba serikali zote ni ovu sema zinatofautiana viwango tu vya uovu
Tusubiri uamuzi wa mahakama ... Kilichofanyika leo ... ni ....?
jamani mfuatilien Taylor vzuri,alipandkizwa na USA kule,ni CIA,labda kwa vile wamarekani ndo zao wakishakutumia wanakutupa kama kondom
Anyongwe.
Zimesomwa facts za kesi na kwamba mahakama imemkuta na hatia ya makosa lakini hukumu ya adhabu haijatolewa bado,