Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Hao watu ni wabaya sana.. Huyo mkurugenzi wa nida kaenda kufukuza vijana wasio na hatia watendani wa chini kabisa huku akiendelea kula na waovu wenzake meza moja eti ili ajisafishe tumuone mtu mwema kumbe na yy ni jipu..
Hawa wanasiasa wanaturubuni sana akili zetu. Ingekuwa amri yng hao ni wakunyongwa kabisa
Yaani waende kisutu kabisa hata kesho nyie papaz mnajiona wasafi kumbe wachafu kabisa
 
Nina uhakaika asilimia 100% Mkurugenzi wa NIDA siyo mmoja ya wamiliki wa infosys. Ndiyo, Kitwanga ni mmoja ya shareholder wa infosys IPS Ltd. Kampuni ya infosys IPS Ltd ni moja ya kampuni chache za IT zenye ufanisi mkubwa na uadilifu ktk utendaji. Ni kampuni ambayo hutimiza ahadi siku zote. Infosys IPS Ltd imewahi kufanya miradi mikubwa sana na wateja kama wizara ya fedha, TRA etc, na kote huko haikuwahi kuchelewesha kazi. Tusubiri naamini kukatakuwa na sababu za kwa nini Lugumi walichelewa au wamechelewa kutekeleza mradi. Hivyo infosys IPS Ltd na Charles Kitwanga ni kampuni safi na Mh. Charles Kitwanga ni muadilifu na mchapa kazi.
Nani anayehusika sasa kma huyo aliyetajwa unakataa..
Tutajie wewe sasa tumjue maana kazi ya PAC unaikataa au naww ni mmoja wao?????
Patachimbika tu hutapona hapo
 
Kwa hiyo Waziri na DG wa Nida Ni maparter ndio maana Rahisi kaenda Kupumzika maana DG wa Nida na Waziri wa mambo ya ndani Wote majipu makubwa yaliyo hiva. Da masifa yote kumbe amnna lolote. Magazeti haliyo yatumia kuwachafua wafanyakazi wa Nida waliofukuzwa kama mbwa na kutopewa stahiki zao yamemchafua yeye. Da amakweli malipo hapa hapa Duniani mbinguni esabu.

Ndg.kwanza fanya marekebisho yafuatayo kwenye hoja yako:-

1. Rais siyo Rahisi.

2. Majipu yaliyoiva siyo hiva.

3. Hamna lolote siyo amna lolote.

4. Magazeti aliyotumia siyo haliyotumia,

5. Mbiguni hesabu siyo esabu.
 
mimi naamini 90% ya watanzania ama uchumi wao ulikuwa unategemea ufisadi au walikuwa wanahaha kutafuta opportunities za ufisadi na hawajapata.

hii ni kutokana na utamaduni tulioujenga wenyewe. kuanzia nyumbani mtume mfanyakazi sokoni ataongeza bei ili apate chake cha mfukoni.

ni mtanzania yupi leo hii utampa fedha akafanye manunuzi akuletee risiti za bei halali? ni mtanzania yupi leo hii ataona nafasi ya ajira aitangaze kwa umma kupata mtanzania mwenye sifa kama si kuita nduguze na marafikize?

ni mtanzania yupi leo hii ataona mtu anafedha anatafuta kitu amuelekeze vizuri kama si kuona kuna nafasi ya kupata? hata wenye nyumba ukifika kwake bila kupitia kwa dalali yeye anatafuta dalali kumuingiza kati.

inastaajabisha kuwa hata walio mstari wa mbele katika kugeuza meli hii kutoka ilikokuwa inaelekea kwenda sehemu sahihi bado wanajaribu kubadilisha wengine huku wao wakifanya yaleyale.

cha msingi ni kutokata tamaa uchumi wa tanzania unaweza kubadilika kutoka kwenye kutegemea ufisadi na kuwa wa kutegemea kuchapa kazi.

watanzania waanze kuwaza jinsi gani wataweza kuwa wabunifu katika kazi ili kupata vipato halali na sio kuwaza kuajiriwa sehemu zenye mirija ya ufisadi.
 
Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga na Dk Modestus Kipilimba mkurugenzi wa NIDA? Hapa kuna jambo!

Tunzeni hii formula; ufisadi(mashine za alama za vidole+Vitambulisho vya Taifa)=wizara ya Kitwanga.

Iliwahi kuandikwa humu hata kabla JPM hajatangaza baraza lake la mawaziri, kwamba Kitwanga alikuwa akijitangaza kwamba atapewa uwaziri na kweli akaupata.

Iliwahi kuandikwa humu pia kwamba Kitwanga na Magufuli ni marafiki wa kutupwa (rejea urafiki wa Kikwete na Lowassa) akakanusha.

Kwa sababu wakati anaingia mkataba huo wa mabilioni na jeshi la polisi hakuwa waziri wa mambo ya ndani lakini baadaye akapewa wizara hiyo hiyo itupe picha gani? Kwamba aliiomba kwa rafiki yake ili asimamie kuuficha ufisadi wake.

Na kama ndivyo, alimdokeza rafikie kwa nini anautaka uwaziri wa mambo ya ndani? Wizara ambayo nina uhakika haiwezi na hataiweza na niliwahi kuandika humu kwamba, Rais anampaje mfanyakazi wa benki kusimamia wizara ya mambo ya ndani.

Ngoja tusubiri yaliyo njiani.
unataka kusema,aliingia mambo ya ndani ili akafiche hiyo scandal?
 
Atafukuzwaje ? Kwan Mpaka sasa kiongozi gani wa kisiasa amewajibishwa kwa makosa yaliyofanyika wakat Wa jk, nafkri mh.anachofanya ni kusimamisha uovu na watakao kiuka ndo wakipate cha moto (Business as usual hapana) amekuwa akisistiza Mara kwa mara
 
Kitwanga Na Ngosha Ni Kama Raila Na Ngosha sidhani Kama atatumbuliwa . Ni upepo tu utapita kwa huyu jamaa wa software!!!. CCM Ni zaidi ya ujuavyo.
 
Huu ni umbeya. Mwandishi alishindwa nini kutafuta majina ya wamiliki wa infosysy na uhusiano wao na hao wamiliki wa lugumi enterprise! Huyu wanayemtaja tumeanza kumsikia na kuingia kwenye mazungumzo ya mitandaoni baada ya kupewa uwaziri, haya leo hii anaandamwa na ufisadi!
 
WAZIRI WA MAGUFULI KTK KASHFA YA UFISADI NA POLISI

- Kampuni inayohusishwa naye ya Infosys ilikuwa mkandarasi

Yadaiwa Infosys inamilikiwa na Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu NIDA

Ni mdau wa LUGUMI enterprises

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34, imeelezwa.

Kuhusika huko kwa Waziri Kitwanga imekuja siku moja, baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) kueleza kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye mkataba ulioingia kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anahusika kupitia kampuni yake ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo.

Jeshi la Polisi limekumbwa na kashfa kubwa ya manunuzi ya vifaa vya kuhifadhi alama za vidole ambapo Kamati ya PAC imegundua kuwa kampuni ya Lugumi Enterprises haikutekeleza mkataba ipasavyo.

Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa hivyo.

Gazeti hili limegundua kuwa moja ya kampuni iliyopewa kazi hiyo ni Infsosys ambayo nakala za msajili wa makampuni inaonyesha kuwa inamilikiwa na Charles Kitwanga na Dk. Modestus Francis Kipilimba, ambaye ni Mkurugenzi wa NIDA.

Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona inaonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilifanya kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa.

Kazi ambayo haikufanyika kabisa kwani mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.

Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.

Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.

Jamani, inawezekanaje kuilipa kampuni pesa zote za mkataba? Nijuavyo malipo hufanywa kufuatana na jinsi kazi inavyokuwa inafanywa. Ilitakiwa walipwe kwa awamu, kulingana na kazi iliyokusudiwa ilivyokuwa inafanyika. Kwa hili, ni vema mh. akakaa pembeni ili uchunguzi ufanyike, kwani akiwa pale kwenye nafasi aliko kazi ya uchunguzi haitafanyika ipasavyo, pia na mkurugenzi wa NIDA asimamishwe kwanza kupisha uchunguzi.
 
Tumewapa wapinzani.hoja za kuinuka nazo bungeni kwa ajili ya kulindana lindana,serikali ingekuwa safi kabisa sasa imekuwa chafu kupita ile,waziri wa mapolisi unakuwa kibaka nani atakuwa msafi....Namuona Magufuli kuzeeka ghafla kabla ya muda,nampa mwaka na nusu mvi tele kichwani
asee hizo bilioni 34 lazima watazitapika asee,,
bora hata wangekuwa wameservice vituo 100,

huu wizi wa kijinga sana
 
Tumejuzwa kuwa Kitwanga na Mkurugenzi NIDA wanazo kampuni hizo tajwa sawa. Hatujapata kujua sababu za kutotimiza shughuli husika.
Yule ambaye amekwisha kuchukuwa upande kwa taarifa hii ya mtoa mada, analake jambo hasa chuki binafsi. Tufuatilie swala hili huku tukiwa hatuna upande huku tukivutwa na uzito wahoja toka pande zote. Tukiweka ushabiki huenda tukaharibu mambo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom