Chapter 002: Tafsiri/ maana ya kuota vikao vya pombe, ala za mziki, ukarimu (hospitality) na yanayo fanana nayo.
Habari zenu wapendwa.
Karibuni katika jukwaa letu pendwa leo hakuna mambo ya kutisha katika maana ya ndoto tajwa za hapo juu hivo natumai tutasoma. Ndoto sio kitu cha kupuuza kabisa kwani ndio network ya kutuunganisha na mambo ya kiroho hivo kama huoti au ukiota unasahau au unaota vipande vipande jua ushakua hacked.
Maana ya kuota unamfanyia mtu ukarimu (hospitality), atakae ota amewaita watu kuwafanyia ukarimu basi ataingia katika jambo ambalo litampelekea kujuta na kupata lawama.
Akiota amewaita watu katika chakula na wale watu wakala mpaka wakaridhika basi maana yake ni kuwa basi hao watu atawaongoza yaani atakua oligarch wao.
Pia inatafsiriwa kuota ukarimu ni kuja kwa mtu aliekua hayupo.
Ama kuota kupiga ngoma ama kusikiliza ngoma ( ngoma ile ngoma ya ngozi) basi maana yake huyo atasikia maneno ya uongo.
Akiota anapiga ngoma nyumbani kwake basi atapata msiba pia ina maana ya uraisi yaani mpigaji hio ngoma anaweza kupta uraisi (uongozi wa sehemu yoyote sio lazma nchi). Pia inawezekana akapata depression.
Na atakae ota anapiga ala yoyote ya mziki mlangoni kwa kiongozi basi atapata uongozi ikiwa mpigaji huyo ni mtu wa hayo mambo ya mziki na ikiwa sio mtu wa mziki akiota hivo basi atazua maneno ya uongo.
Na dhumari katika ndoto ni maombolezo, atakae ota amepewa zumari na kiongozi maana yake atapa uongozi ikiwa ni mtu wa mazumari yaani ndio fani yake ikiwa sio fani yake basi atapata amani tu ya moyo.
Ikiwa mtu ni mgonjwa akaota anapiga zumari basi maana yake atakufa.
KUPIGA DUFU
Atakae ota anapiga dufu basi maana yake atapata stress, anixiety na depression pamoja na umaarufu ( fame) na ikiwa wakati wa upigaji wa hilo dufu alikua yupo pamoja na jirani zake basi maana yake ni jambo zuri litamfika huyo mtu na ukubwa wake na uzuri wa hilo jambo itategemea na ule muonekano wa ile shughuli ilivyokua.
Na nyimbo za harusi pamoja na harusi basi maana yake ni msiba wa watu wa hio nyumba iliootwa.
NYIMBO
Ama mtu akiota nyimbo, ikiwa nzuri hio nyimbo basi ni dalili ya biashara tena yenye faida, na ikiwa sio nyimbo nzuri basi maana yake ni biashara nyenye hasara.
Ila pia nyimbo inasemwa kuwa ni mzozo na ugomvi.
Na pia muimbaji anatafsriwa kama mtu msomi , msimuliaji wa stori , na mtu akiota nyimbo inapigwa sokoni basi maana yake ni fedheha na jambo baya litatokea katika hilo soko.
Na atakaeota anaimba huku anatembea mana yake ni kuwa ni jambo jema litaamfika.
Na atakaeota anaimba na yeye yupo chooni basi maana yake atatuhumiwa.
KUCHEZA ( i.e Dancing)
Na atakae ota anacheza basi atapata stress na msiba ambao utampelekea asipate utulivu.
Mgonjwa anaeota anacheza basi maana yake ugonjwa wake utarefuka.
Na maskini akiota anacheza basi atapata utajiri wa mda.
Mwanamke akiota anacheza maana yake atapata fedheha.
Mfungwa akiota anacheza basi maana yake atakua huru.
Na mtu akiota yupo baharini anacheza basi maana yake litatokea jambo baya hapo walipo.
N atakae muota mtu anacheza mbele yake basi mana yake mchezaji na anaechezewa watapata msiba sawa sawa.
Na atakaeota anacheza mlangoni kuingilia nyumbani kwake na watu wake wapo pembeni yaani hakuna mgeni yake basi maana yake ni kuwa watapata jambo zuri wote sawasawa.
JUICE
Atakae ota anakunywa juice ni dalili ya kizazi.
POMBE NA KULEWA
Atakaeota anakamua ulevi maana yake atakua mhudumu wa kiongozi, na ndani yake yatapita mambo makubwa.
Na asili ya pombe katika ndoto ni mali ya haramu ( au dhulma), na atakae ota anakunywa pombe basi maana yake atafanya madhambi makubwa na atapata riziki au manufaa kwa wepesi kabisa.
Na atakae ota anakunywa pombe wala hajazozana na mtu basi atapata mali ya haramu wengine wanasea atapata mali ya halali.
Na atakae ota amekunywa halafu akazozana na watu basi maana yake ataingia katika ugomvi na uhasama kwa kadiri ya alivyoota kule usingizini.
Na atakaeota amepata mto (river) wa ulevi basi atapata fitina katika dini yake na akiingia katika huo mto basi maana yake ataingia katika fitna kadiri ya kiwango cha maji aliyoyaingia.
Na atakae ota amelewa hali yakuwa hakunywa basi maana yake atapata depression.
Na atakaeota amelewa kutokaana na kunywa basi atapta amani kutokana na jambo lenye kuogopesha.
N.B nikisema neno msiba sikusudii ule wa kufiwa tu bali kila jambo linalomfika mtu baya.
Ndoto nzuri msimulie umpendae na ndoto uliota ikakuchukiza kuifanya isitokee basi ni kukaa kimya na usimuhadithie mtu.
Usikose next chapter.