Chapter 001: Maana/Tafsiri ya kuota kufa, maiti na yanayoambatana na mazishi

tilmikha

tilmikha

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2013
Messages
255
Points
500
tilmikha

tilmikha

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2013
255 500
Habari zenu wapendwa!
Kwanini nimeanza chapter 001 na kuanza kuelezea maana halisi ya ndoto zinazohusiana na kifo? Kifo sio kigeni kwetu na wengi tumeshaondokewa na wapendwa wetu si mmoja sio wawili. Nimechagua kuanza kufasiri maana ya ndoto zihusiano na kifo kwa kuwa mauti ndio mlango pekee wakuendea katika maisha halisia na wafu ndio pekee wanaoishi haya maisha halisi.
MAUTI
Mauti katika ndoto ni majuto kutokana na jambo kubwa mno ambalo litamtokea muotaji wake. Hivo basi atakaeota amefariki kisha akaishi tena basi maana yake atatenda dhambi kisha atatubia.
Na atakae ota amefariki pasi na kuumwa wala kupata hekaheka zaa umauti basi ataishi umri mrefu.
Na atakae ota kwamba hatakufa basi kufa kwake kupo karibu.
Na atakae ota kiongozi wa nchi amefariki basi huo mji utaharibika kama ilivyo kuota kuharibika kwa mji dalili ya kufa kiongozi. Na atakaae muota mtu maarufu ambae alishakufa kuwa amekufa tena na watu wakamlilia pasi na kupiga makelele ya maaombolezo basi muotaji ataoa ama kuolewa . Ila inawezekana pia kumuota mtu aliefariki amefarriki ikawa maana yake kwenye kizazi cha muotaji au alieotwa akafariki mtu mwengine.
Na atakae ota watu waamefariki kutokana na janga fulaani katika eneo fulani basi eneo hilo litapata janga.
Na atakae ota amefariki hali yakua yupo uchi basi maana yake atafilisika yaani atakua fukara.
Na akiojiona amelala juu ya busati basi atapata manufaa kutoka kwa watu wa nyumbani kwake, na akiota amepata maiti basi atapata mali.
Na akiota ameletewa habari ya mtu amefariki maana yake itamjia habaari ya kuharibika dini yake na kutengenea dunia yake.
Na akiota mtoto wake wa kiume amefariki basi maana yake atachomokaa kwa adui yake. Na akiota mtoto wake wa kike amefaariki basi atakata tamaa juu ya kupata faraja.
Na akiota kuna mtu anampa habari juu ya kifo cha mtu fulani basi atapata habari ya jambo la mauti ya mtu ambalo litapekea msongo wa mawazo mkubwa ambao ndio utakua sababu ya kufa kwake.
Mama mjamzito akiota amefariki na watu wakambeba huku wakawa wanalia kistarabu yaani kilio ambacho haakiambatani na kujipiga wala kuchana nguo, basi atazaa mtoto wa kiume na atafurahikia uzazi wake huo.
Single man/ single woman akiota amekufa maana yake ataoa / ataolewa.
MAOMBOLEZO
Nikizungumza maombolezo namaanisha kilio ambacho kimeambatana na kelele ama kuchana nguo, hivo basi mtu akiota kuna eneo watu wanomboleza maana yake ni kua hilo eneo litapaata balaa kubwa ambalo litakua sababu ya kuangamia hilo eneo.
KILIO
Kilio kwenye ndoto ikiwa ni machozi tu yanaatoka pasi na sauti za kulia kwa makelele maana yake huyo mtu atapata jambo lenye kumfurahisha na akiota kinyume chake basi maana yake atapata msongo wa mawazo.
to be continue.......
ila ukiota mtu ambae ashafariki anakwambia kuwa utafariki basi jua utafariki kweli kwasababu deads aren't lying.
 
tilmikha

tilmikha

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2013
Messages
255
Points
500
tilmikha

tilmikha

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2013
255 500
KUOSHA MAITI
Atakeota maiti anajiosha basi maana yake kuwa muotaji atatoka katika matatizo na utajiri wake utaongezeka.
Na anaoshwa mara nyingi huwa ni tajiri katika asili ya ndoto.
SANDA
Sanda dalili yake ni mtu kuelekea katika uzinzi, na atakae ota anavishwa mavazi kama ya maiti basi ni dalili ya kufa kwake.
KUZIKWA
Ama atakae ota anazikwa basi maana yake atasafiri safari ndefu ambayo itapelekea kupata mali ndani yake.
 
comrade wetu

comrade wetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2018
Messages
540
Points
500
comrade wetu

comrade wetu

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2018
540 500
Daah wameanza tena kutishana ,wajameni hayo mambo yaacheni wajameni daah Mungu hataki tutishane hivyo
 
boga la kiangazi

boga la kiangazi

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Messages
281
Points
500
boga la kiangazi

boga la kiangazi

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2018
281 500
na ukiota mtu aliyefariki kitambo anakupikia chakula inakuaje
 
aimi lyatuu

aimi lyatuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Messages
408
Points
250
aimi lyatuu

aimi lyatuu

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2015
408 250
mpaka hapa sijamwona mshana jr kunani??!
 
tilmikha

tilmikha

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2013
Messages
255
Points
500
tilmikha

tilmikha

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2013
255 500
Chapter 002: Tafsiri/ maana ya kuota vikao vya pombe, ala za mziki, ukarimu (hospitality) na yanayo fanana nayo.
Habari zenu wapendwa.
Karibuni katika jukwaa letu pendwa leo hakuna mambo ya kutisha katika maana ya ndoto tajwa za hapo juu hivo natumai tutasoma. Ndoto sio kitu cha kupuuza kabisa kwani ndio network ya kutuunganisha na mambo ya kiroho hivo kama huoti au ukiota unasahau au unaota vipande vipande jua ushakua hacked.
Maana ya kuota unamfanyia mtu ukarimu (hospitality), atakae ota amewaita watu kuwafanyia ukarimu basi ataingia katika jambo ambalo litampelekea kujuta na kupata lawama.
Akiota amewaita watu katika chakula na wale watu wakala mpaka wakaridhika basi maana yake ni kuwa basi hao watu atawaongoza yaani atakua oligarch wao.
Pia inatafsiriwa kuota ukarimu ni kuja kwa mtu aliekua hayupo.
Ama kuota kupiga ngoma ama kusikiliza ngoma ( ngoma ile ngoma ya ngozi) basi maana yake huyo atasikia maneno ya uongo.
Akiota anapiga ngoma nyumbani kwake basi atapata msiba pia ina maana ya uraisi yaani mpigaji hio ngoma anaweza kupta uraisi (uongozi wa sehemu yoyote sio lazma nchi). Pia inawezekana akapata depression.
Na atakae ota anapiga ala yoyote ya mziki mlangoni kwa kiongozi basi atapata uongozi ikiwa mpigaji huyo ni mtu wa hayo mambo ya mziki na ikiwa sio mtu wa mziki akiota hivo basi atazua maneno ya uongo.
Na dhumari katika ndoto ni maombolezo, atakae ota amepewa zumari na kiongozi maana yake atapa uongozi ikiwa ni mtu wa mazumari yaani ndio fani yake ikiwa sio fani yake basi atapata amani tu ya moyo.
Ikiwa mtu ni mgonjwa akaota anapiga zumari basi maana yake atakufa.
KUPIGA DUFU
Atakae ota anapiga dufu basi maana yake atapata stress, anixiety na depression pamoja na umaarufu ( fame) na ikiwa wakati wa upigaji wa hilo dufu alikua yupo pamoja na jirani zake basi maana yake ni jambo zuri litamfika huyo mtu na ukubwa wake na uzuri wa hilo jambo itategemea na ule muonekano wa ile shughuli ilivyokua.
Na nyimbo za harusi pamoja na harusi basi maana yake ni msiba wa watu wa hio nyumba iliootwa.
NYIMBO
Ama mtu akiota nyimbo, ikiwa nzuri hio nyimbo basi ni dalili ya biashara tena yenye faida, na ikiwa sio nyimbo nzuri basi maana yake ni biashara nyenye hasara.
Ila pia nyimbo inasemwa kuwa ni mzozo na ugomvi.
Na pia muimbaji anatafsriwa kama mtu msomi , msimuliaji wa stori , na mtu akiota nyimbo inapigwa sokoni basi maana yake ni fedheha na jambo baya litatokea katika hilo soko.
Na atakaeota anaimba huku anatembea mana yake ni kuwa ni jambo jema litaamfika.
Na atakaeota anaimba na yeye yupo chooni basi maana yake atatuhumiwa.
KUCHEZA ( i.e Dancing)
Na atakae ota anacheza basi atapata stress na msiba ambao utampelekea asipate utulivu.
Mgonjwa anaeota anacheza basi maana yake ugonjwa wake utarefuka.
Na maskini akiota anacheza basi atapata utajiri wa mda.
Mwanamke akiota anacheza maana yake atapata fedheha.
Mfungwa akiota anacheza basi maana yake atakua huru.
Na mtu akiota yupo baharini anacheza basi maana yake litatokea jambo baya hapo walipo.
N atakae muota mtu anacheza mbele yake basi mana yake mchezaji na anaechezewa watapata msiba sawa sawa.
Na atakaeota anacheza mlangoni kuingilia nyumbani kwake na watu wake wapo pembeni yaani hakuna mgeni yake basi maana yake ni kuwa watapata jambo zuri wote sawasawa.
JUICE
Atakae ota anakunywa juice ni dalili ya kizazi.
POMBE NA KULEWA
Atakaeota anakamua ulevi maana yake atakua mhudumu wa kiongozi, na ndani yake yatapita mambo makubwa.
Na asili ya pombe katika ndoto ni mali ya haramu ( au dhulma), na atakae ota anakunywa pombe basi maana yake atafanya madhambi makubwa na atapata riziki au manufaa kwa wepesi kabisa.
Na atakae ota anakunywa pombe wala hajazozana na mtu basi atapata mali ya haramu wengine wanasea atapata mali ya halali.
Na atakae ota amekunywa halafu akazozana na watu basi maana yake ataingia katika ugomvi na uhasama kwa kadiri ya alivyoota kule usingizini.
Na atakaeota amepata mto (river) wa ulevi basi atapata fitina katika dini yake na akiingia katika huo mto basi maana yake ataingia katika fitna kadiri ya kiwango cha maji aliyoyaingia.
Na atakae ota amelewa hali yakuwa hakunywa basi maana yake atapata depression.
Na atakaeota amelewa kutokaana na kunywa basi atapta amani kutokana na jambo lenye kuogopesha.
N.B nikisema neno msiba sikusudii ule wa kufiwa tu bali kila jambo linalomfika mtu baya.
Ndoto nzuri msimulie umpendae na ndoto uliota ikakuchukiza kuifanya isitokee basi ni kukaa kimya na usimuhadithie mtu.
Usikose next chapter.
 
WAZO JIPYA

WAZO JIPYA

New Member
Joined
Sep 13, 2017
Messages
3
Points
20
WAZO JIPYA

WAZO JIPYA

New Member
Joined Sep 13, 2017
3 20
vipi kama ukisahau ulicho kiota, lakin unakumbuka kwamba uliota.......??
 
WAZO JIPYA

WAZO JIPYA

New Member
Joined
Sep 13, 2017
Messages
3
Points
20
WAZO JIPYA

WAZO JIPYA

New Member
Joined Sep 13, 2017
3 20
Itakua wanaanza kukudukua hao
walivyo anza kukudukua na ww ulikua unaota hivyo, ..?? maana rafiki yangu ndo analo hillo tatizo, kama walianza hivyo nambie nmshauri awai maombi asije kua gwiji la kudukuliwa kama ww
 

Forum statistics

Threads 1,336,416
Members 512,614
Posts 32,538,754
Top