"Chanzo" kilindwe au kiharibiwe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
"CHANZO" KILINDWE AU KIHARIBIWE.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Hekima hii isomwe na watu wote wapendao ufahamu. Iwajenge pale walipobomoka, iwaimarishe pale walipodhoofika.
Nayo isionekane naliandika kujipatia utukufu, Isipokuwa kutimiza kusudi.

NIITE Taikon wa Fasihi, Mwana kutoka Nyota ya Tibeli.

Kila Jambo lina chanzo chake, Lina chimbuko lake, kila Jambo linamizizi yake. Liwe Jambo zuri au Baya, jema au ovu, yote Yana chanzo chake.

Maisha yako yawe mazuri au mabaya, jua kuna chanzo chake. Kuna mizizi yake. Chanzo kinaweza kuwa kimekomaa au bado kuchanga. Haya hivyo chanzo ni chanzo tuu. Mara nyingi kama sio zote chanzo hujificha, ni Kama mizizi ya mmea. Hujificha hivyo ni mpaka uchimbe ili uweze kukiona.

Chanzo! Chanzo! Chanzo cha yote yanauokupata unakijua?

Nikasema nifikiri kuhusu wema, nikatafakari habari zake, nikazichunguza na kuzitenda, hapo nikaona chanzo cha wema ni Mema yenyewe. Tena wema mizizi yake hudumu wala haiharibiki. Nao wema ndio utakaokusaidia. Kwa maana Wema ni Msaada.

Nikasema nifikiri kuhusu Uovu, nikatafakari habari zake, nikazichunguza na kuzitenda hapo nikaona chanzo cha ubaya ni ubaya wenyewe. Tena miziz yake haidumu na huharibika. Nao ubaya hausaidia isipokuwa ni uangamivu.

Maisha yako yanachanzo chake. Hata hivyo maisha ni kuishi. Katika kuishi utaishi Kwa vyanzo vya nyuma ulivyovikuta na kisha utaishi Kwa vyanzo utakavyovianzisha.

Kama ulizaliwa kwenye familia Masikini, basi fahamu kipo chanzo cha umasikini katika Familia yenu. Halikadhalika na Kwa waliozaliwa kwenye Familia tajiri.

Unaweza kuzaliwa Kama Baraka au Kama Laana hapa Duniani kutegemeana na aliyekuzaa au chimbuko lako. Hata hivyo unaweza kuzaliwa laana lakini ukaibomoa laana hiyo ingawaje ni ngumu Sana lakini inawezekana. Pia unaweza zaliwa baraka lakini ukaiharibu baraka hiyo.

Kila mafanikio Yana chanzo chake. Kila Laana inachanzo chake.

Kila familia lazima iwe na mtu mmoja ambaye ndiye atakuwa chanzo cha baraka ndani ya Familia. Vivyo hivyo Kwa upande wa laana. Kila familia lazima iwe na mtu mmoja ambaye lazima awe chanzo cha laana ndani ya Familia.

Mara nyingi Ila sio mara zote chanzo cha baraka huwaga ni mzaliwa wa Kwanza, yaani LANGO KUU. Nimesema mara nyingi sio Mara zote.

Unapoanzisha Familia yako ambapo baadaye utakuwa ukoo lazima Kama Baba au Mama usome nyendo zako au mwenzi wako kisha watoto wako. Ili ujue Nani ni chanzo cha Baraka katika Familia yenu/yako.
Nani ndio Taa ya nyumba yenu.

Kwa bahati nzuri Taa haijifichi, Taa siku zote inang'aa hasa kwenye Giza. Kwa waliokwenye mahusiano ya ndoa au Uchumba mtakubaliana nami kuwa kuna mtu ukiwa naye kwenye mahusiano mambo yako yanafunguka, yanaenda Kwa urahisi, yaani unafanikiwa tuu. Lakini pia kuna mtu ukiwa naye kwenye mahusiano mambo yako yanaenda Mrama, yanaharibika.
Hivyo ndivyo ilivyo.

Kuna mtoto ukishamzaa, utashangaa Mambo yanaenda na unafanikiwa mno. Pia na mtoto mambo yake yanaenda, anailetea familia sifa njema zenye baraka.
Mtoto huyo ni chanzo cha baraka katika familia yako.

Kwa watu wenye akili na Maarifa, hulinda Kwa Hali na Mali vyanzo vya Baraka. Na hapa hulinda baada ya kuvitambua.
Huvilinda Kwa sababu kupitia vyanzo hivyo ndio maisha yao huwa marahisi na yenye kuvutia na kutamanika na wengine.

Huvilinda vyanzo hivyo Kwa sababu, vyanzo hivyo hushambuliwa mara Kwa mara na maadui ili kuviangusha.

Ukishajua Mkeo/ mumeo au mtoto Fulani ni baraka ndani ya familia yaani ndiye nguzo kuu au taa ya familia lazima uilinde Kwa nguvu zote.
Chanzo kizuri hulindwa.

Usiishie kusema vyema havidumu, havidumu Kwa sababu havilindwi.
Familia nyingi zimejikuta zilipoteza chanzo muhimu cha baraka kwa kushindwa kukilinda chanzo hicho.
Unakuta Yule mtoto anayetegemewa anawahi kufa mapema ili familia na ukoo uanguke na uhenyeke. Na hakika koo na familia nyingi zinahenyeka baada ya chanzo kikuu cha baraka kudondoka.

Kwenye familia yoyote Ile hamuwezi kuinuka wote Kwa Pamoja. Hata Kama wote mtainuka na kuwa mpo juu. Lakini lazima awepo Chanzo kikuu cha wengine kuinuka. Lazima awepo aliyewainua wenzake.

Katika mapambano, Adui anapotaka kuishambulia Familia au ukoo wenu. Hashambulii tuu ilimradi anashambulia, adui hawezi poteza nguvu zake kijinga hivyo. Anaangalia familia Fulani mzizi Mkuu WA mafanikio unatoka Kwa Nani. Akishakuwa, basi anapiga kule Kule,

Hata kwenye mpira hii hutumika,
Mchezaji anayetegemea hutafutiwa dawa azibitiwe ikiwezekana apewe Kadi nyekundu atoke nje ya mchezo.
Hiyo imejitokeza mara nyingi, mfano kwenye mechi ya Simba na Yanga ya Juzi, club ya Simba ilishamuona Mukoko Tonombe ndiye Taa, chanzo, na tegemezi WA timu ya Yanga, hivyo wakamfanyia hila ili apewe Kadi nyekundu ili kufifisha Ari ya wachezaji wenzake wa Yanga. Baada ya Mukoko kutoka basi mechi ikawa rahisi Kwa Simba.
Hii pia ilitokea Kwa Zidane miaka ile alipompiga kichwa mchezaji mwenzake.

Adui hadili na Kundi soma isipokuwa anadili na chanzo cha mafanikio ndani ya Familia.

CHANZO Kilindwe.

Kitalindwaje? Zifuatazo ni sehemu ya mbinu za kulinda Taa ya Familia;

1. Kwanza itambulike kuwa Fulani ndiye chanzo cha baraka katika ukoo wetu.

2. Iundwe kamati ya Ulinzi na usalama wa kukilinda chanzo Hiko.

3. Kamati hiyo uhusishe kategori ZIFUATAZO
I. Sayansi, Teknolojia na elimu.
2. Ujasusi, Dola, na Serikali.
3. Mizimu na Falme kuu za kiroho.

1. Sayansi, Teknolojia na elimu
Kamati hii kazi yake iwe kumlinda na kumshauri Taa/chanzo kikuu cha mafanikio ya familia yenu kisayansi, kielimu na kiteknolojia.

2. Ujasusi, Dola na Serikali
Taa ilindwe kulitia medani za kijasusi Kwa kuchunguza na kupata taarifa nyeti za kuwafahamu maadui wa Taa yenu, kuzichakata taarifa hizo na kuzifanyia kazi. Kujua wanipango gani na wamekusudia kuitekelezaje na lini Kwa kutumia au kumtumia Nani na wapi.
Lazima mtafute connection ya Dola na Serikali kuhakikisha Taa yenu ipo salama salimini, ni heri afungwe au afe mwingine lakini sio Taa yenu.

Taa izimwe Kwa mapenzi ya Mungu na sio mipango ya Wanadamu. Kama ilivyosasa Taa nyingi zinazimwa Kwa mapenzi ya wanadamu.

3. Mizimu na Falme kuu za kiroho.
Hii ni sehemu nyeti zaidi.
Mizimu ni Wale mashujaa WA ukoo waliotangulia kuzimu. Hawa wameshakufa lakini Kwa namna moja ama nyingine wanamchango Kwa ulimwengu WA waliohai.
Hawa utawafanyia Hisani za Shukrani Kama vile kuwakumbuka, kuwataja Kwa Mema, kufanya Yale mambo waliokuwa wanampenda kuyafanya, mambo Mema.

Kisha chanzo mkipe Ulinzi wa Kiroho kulingana na miungu mnayoiamini. Lengo ni kuwa Mungu/miungu ikilinde chanzo chenu cha baraka kisiangamizwe alafu nanyi mkaonja joto ya jiwe.

Chanzo lazima Kilindwe na hapa nazungumzia chanzo kikuu cha mafanikio ndani ya Familia.

Hata hivyo ni kawaida kuona ndani ya Familia kuna mifarakano na migogoro.
Kikawaida Yule aliyechanzo cha laana ndani ya familia lazima ahasimiane na Yule aliyechanzo cha baraka ndani ya Familia.

Ni kawaida kuona ndugu akienda kumloga mwenzake ili asifanikiwe. Ndugu au mtoto wa hivi ujue ndiye chanzo cha laana kwenye familia.

Mtoto yeyote anayewaonea wenzake Wivu, anayewagombabisha ndugu na kusambaza fitna huyo ni chanzo cha laana ndani ya Familia.

Chanzo kibaya lazima Kiharibiwe. Kitaharibiwaje?
Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
0693322300
 
Back
Top Bottom