Chanzo cha wanafunzi Z'bar kufeli

Invisible

JF Admin
Feb 26, 2006
16,285
8,340
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema chanzo cha wanafunzi kufanya vibaya katika mitihani yao ni baadhi ya walimu kufundisha zaidi katika shule za nje na kuwaacha wanafunzi wasiokuwa na uwezo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Haroun Ali Suleiman, siku chache baada ya kukabidhiwa ripoti iliyochunguza chanzo cha matokeo mabaya kwa wanafunzi wa kidato cha sita mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mtaa wa Mazizini Unguja, Waziri Haroun, alisema imebainika baadhi ya walimu hawatekelezi kazi zao ipasavyo na muda mwingi huutumia katika masomo ya ziada (tuition) kutafuta maslahi zaidi.

Alisema hivi sasa walimu wengi wanafundisha shule zaidi ya moja hasa katika shule za binafsi huku wakiwa watumishi wa serikali.

Alisema hali hiyo imesababisha wanafunzi kutopewa kazi za kutosha za majaribio na walimu wao na wengi wao hujenga matumaini zaidi katika masomo ya ziada.

"Imegundulika baadhi ya walimu hawatekelezi kazi zao inavyotakiwa na badala yake hutegemea zaidi kwenye tuition," alisema Waziri Haroun.

Sababu nyingine alizozitaja ni baadhi ya walimu kutokuwa na uwezo na uzoefu wa kufundisha madarasa ya sekondari, hivyo kuchangia kuathiri matokeo ya wanafunzi.

Alieleza kwamba kwa upande wa wanafunzi, imebainika wanafunzi walio wengi wanategemea zaidi kununua mitihani, badala ya uwezo waliokuwa nao na inapotokea kukosa matokeo hayo matokeo yao yanakuwa mabaya zaidi.

Aidha, alisema kumejitokeza tabia kwa baadhi ya wanafunzi kuamini zaidi walimu wa masomo ya ziada badala ya wale wanaofundisha shuleni, wakati baadhi ya walimu wa tuition hawana sifa wala uzoefu wa kufundisha.

Hata hivyo, alisema kwamba matokeo mabaya yamechangiwa na uhaba wa walimu wa sayansi wenye sifa na upungufu wa vifaa vya maabara kwa shule mbalimbali za sekondari.

Wizara ya Elimu Zanzibar iliunda Kamati Maalumu ya Uchunguzi, iliyoongozwa na Mhadhiri wa Chuo Kukuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Dk. Ahmada Khatib, kuchunguza chanzo cha matokeo mabaya ya kidato cha sita mwaka 2006, baada ya wanafunzi wote kushindwa kufaulu kiwango cha daraja la kwanza.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Novemba 19, 2007
 
Duuhh,

Hivi huyu Waziri kweli yuko serious kuzungumza hizi statements.....kama hizi
................Sababu nyingine alizozitaja ni baadhi ya walimu kutokuwa na uwezo na uzoefu wa kufundisha madarasa ya sekondari, hivyo kuchangia kuathiri matokeo ya wanafunzi.

Alieleza kwamba kwa upande wa wanafunzi, imebainika wanafunzi walio wengi wanategemea zaidi kununua mitihani, badala ya uwezo waliokuwa nao na inapotokea kukosa matokeo hayo matokeo yao yanakuwa mabaya zaidi...............


Tuna kaaazi kweli kweli
 
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Novemba 19, 2007

nilidhani watakuja na solution ya kuongeza mishahara kwa walimu, kumbe ndo kwanza wanawatupia lawama walimu, ama kweli agonjwae ndie anaetegemewa kufa.nimewahi kuwaona walimu wa serikali zanzibar wanapokea elfu 50 kwa mwezi.unadhani mwalimu huyu atakuwa ******** ili ategemee ualimu tu? yaguuju!
 
Mimi nafikiri kule napo wanakomalia sna Madrasaa sana wanasahau elimu dunia.Wengi wa kule kwanza wana komaa miaka kibao Madrasa wakikariri juzuu(?)
 
Duuhh,

Hivi huyu Waziri kweli yuko serious kuzungumza hizi statements.....kama hizi
................Sababu nyingine alizozitaja ni baadhi ya walimu kutokuwa na uwezo na uzoefu wa kufundisha madarasa ya sekondari, hivyo kuchangia kuathiri matokeo ya wanafunzi.

Alieleza kwamba kwa upande wa wanafunzi, imebainika wanafunzi walio wengi wanategemea zaidi kununua mitihani, badala ya uwezo waliokuwa nao na inapotokea kukosa matokeo hayo matokeo yao yanakuwa mabaya zaidi...............


Tuna kaaazi kweli kweli

Huyu waziri na walimu wake wooote, hawana nidhamu hata chembe. Wanapaswa kuwajibishwa. Hizo sababu alizotoa ni jinsi gani inaonekana kuwa hayupo makini na wizara yake.
Ovyooo kabisa. Nahisi kichefu chefu kabisa kabisaaa.
 
Back
Top Bottom