Chanzo cha Ugomvi wa Marekani Vs Venezuela

Chanzo cha Ugomvi wa Marekani Vs Venezuela

Hiko hivi Sababu kuu nyuma ya ugomvi wa U.S. na Venezuela ni Mafuta.

Venezuela ina akiba kubwa ya mafuta duniani. Malighafi hii ni nyingi sana kwa uzalishaji wa bidhaa za wese (hasa kwa ukanda wa Americas). Kwa nini hili wese linaleta shida: Kwanza mafuta = economic power, Mafuta = geopolitical leverage, ukiwa na Mafuta yasiyokuwa ndani ya nguvu ya Mmarekani = na strategic threat (Tishio) kwa nchi kama Marekani.

Historia hiko hivi: Venezuela ilikuwa ndio supplier wa wese (Mafuta) kwa Marekani kwa miongo mingi, Bwana Hugo Chávez (1999) alivyoingia madarakani, Venezuela ikabadili sheria ya Mafuta kuifanya iwe chini ya usimamizi na udhibiti wa Serikali au Taifa na ushawishi wa kibiashara wa Marekani kwenye Mafuta hayo ukachinjiwa baharini, yani wakasitisha ushirikiano wa kibiashara. Makampuni ya Marekani yakakosa udhibiti wa mafuta → Washington ikapoteza nguvu ya kutamba na kudhibiti soko la mafuta duniani na ikapunguza ushawishi wa kimkakati kwenye kufanya biashara hiyo.

Mafuta sio kichwa cha habari, Mafuta ndio kiini cha Habari yenyewe.

Tukija kwenye Itikadi: Mfumo wa Kiujamaa Vs Mfumo wa Ubepari Huru wa Kimarekani. Hapa namzungumzia Socialism Vs Liberal Capitalism.

Kwa uwazi kabisa Venezuela ilikataa mfumo wa Ubepari wa Mmarekani, ikaanza kusisitiza kuhusu ujamaa wenye kuukataa ubeberu. Ikaanza kufuata na kuambatana na misingi ya kijamaa ya nchi kama Cuba, Russia, China, na Iran

Tukija kwenye Mtazamo wa Marekani: Nchi ya Kijamaa kwenye Ukanda wa Ncni cha Magharibi (Western Hemisphere) = Ni Mfano mbaya kwa nchi za bara la Amerika na jambo lisolopaswa kuwepo katika ukanda huo. Hususani na zaidi nchi iwe inajaribu kutunisha kifua au kuitishia Marekani waziwazi.

Jambo linaloiwazisha Marekani: “Ni kama Venezuela itaweza kumudu na kutoboa chini ya falsafa za kiujamaa licha ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Mmarekani, basi uenda na Nchi nyingine zikafuata na kuanza kukaidi Maagizo ya Marekani”

Marekani anaogopa sana nchi nyingine za ukanda huo zisijekufuata jeuri ya Venezuela, na Jeuri kwa nchi za ukanda huo ni Jambo lisilokubalika katika Dhana ya Sera za Kigeni kwa Nchi ya Marekani. Marekani uwa apendi kukaribisha maadui katika maeneo yake ya kujidai. Akiwa katika maeneo yake ya kujidai Lazima nyote mfuate sera zake.

Marekani akaja na Dhana ya Kubadilisha Utawala (Mpango wa Uendeshaji) hili kuondoa utawala wa serikali ya Venezuela: Marekani ikidai Rais Maduro sio Rais aliyetakiwa kuwepo Madarakani (illegitimate President), yupo kimakosa. Marekani ikidai uchaguzi mkuu wa kumchagua Maduro ulikuwa na udanganyifu na wizi wa kura. Marekani ikadai kuna ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Venezuela. Marekani ikadai Rushwa imekithiri katika serikali ya Venezuela. Marekani ikadai Venezuela Inahusika na usambazaji wa madawa ya kulevya.

Ni dhahiri kuwa baadhi ya madai haya ni ya kweli, lakini Madai mengine yamekuzwa kisiasa tu. Jambo kuu hapa ni kuwa Marekani lengo lake sio Venezuela kufanya mabadiliko ya kisheria (Reform) bali lengo la Marekani inataka kuondoa Uongozi wote wa serikali ya Venezuela hili Biashara za awali ziendelee kama ilivyokuwa Mwanzo.

Ushahidi wa kwanza juu la lengo la Marekani ni: Kwanza Marekani inamtambua mgombea upinzani Bwana Juan Guaidó kama ndio Rais wa Venezuela. Vikwazo vimewekwa hili Kuidhoofisha Venezuela kiuchumi hili wairambe miguu ya Marekani na vikwazo hivyo sio kwa ajili ya kuwaadhibu viongozi wanaohusika. Kingine ni kauli za wazi za Marekani wakitaka Maduro aachie ngazi kwa hiari. Hii ni kama mbinu ya kutaka kuikomoa serikali na si utatuzi wa kidiplomasia uliozoeleka.

Vikwazo vya Kiuchumi → Uchumi Kuporomoka → Msukumo Mkali Wa Kisiasa

Vikwazo vya kiuchumi havikuwekwa kwa bahati mbaya— Ni imetumika kama Silaha za kiuchumi.

Madhara yake: Kuzuiwa kwa Usafirishaji wa Mafuta, Kuzuiwa kwa huduma za kibenki, Sarafu kuporomoka, kukosekana kwa Dawa muhimu na Chakula

Uhalisia: > Raia ndio uathirika na madhara karibu yote ya Vikwazo hivyo

Matokeo: Watu wataandamana kupinga Kodi kali za serikali, watu wanaandamana kwa ugumu wa maisha, wanajeshi wataasi au wanajeshi wataamia upande mwingine hili kupinga serikali kwa kushindwa kuongoza nchi vizuri, Serikali itayumba na miimili kuporomoka

Lakini kwa Venezuela hayo yote hayakutokea, na kushindwa kuanguka kwa utawala wa Venezuela ndiko kulikochochea ugomvi zaidi na Mmarekani. Mmarekani hesabu zake zilikataa, na serikali ya Venezuela ikazidi kuwa imara licha ya Vikwazo vyote ilivyowekewa. Mmarekani nae ndio akazidi kusala kama Nyati aliyekoswa na risasi.

Jiografia ya Kisiasa: Venezuela amechagua “Marafiki Wabaya” kwa lugha nyingine amechagua marafiki ambao ni maadui wa moja kwa moja wa Marekani.

Venezuela Imeimarisha mshikamano na:

🇷🇺 Urusi (Kimajeshi, kwenye biashara ya mafuta, kidiplomasia)

🇨🇳 China (Kwenye Mikopo, kwenye Miundombinu)

🇮🇷 Iran (Ushirikiano wa Matumizi ya Nishati, Kwenye kukataa shinikizo la Vikwazo vya Uchumi)

🇨🇺 Cuba (Ulinzi na Ujasusi)

Kutoka kwenye darubini za Washington: Huu Mshikamano wa Venezuela na hizi nchi ni kama maadui zake wanacheza kabisa kwenye eneo la Sebuleni la Marekani.
Nchi hizi kuingilia ugomvi huu inatafsiriwa kama uvunjifu wa “Sheria na Sera za Monroe” ambazo zinasema “Jaribio lolote la nguvu za Ulaya kudhibiti au kuathiri kisiasa taifa lolote la bara ya Amerika lingechukuliwa na Marekani kama kitendo cha uhasama dhidi yake.”

Oyaa, Hii ni tabia ya kawaida ya ushindani kati ya nchi zenye nguvu kubwa. Kila mtu kujaribu kuingilia masuala ya nchi zingine za adui yake hili kuonesha mwamba. Mnakumbuka pia ile vita ya Ukrein na Urusi, baada ya Mmarekani kuingilia sera za Urusi na kupeleka jeshi la NATO katika maeneo ya kujidai ya urusi.

Issue nyingine inayodaiwa kwenye ugomvi huu ni Issue ya Usafirishaji wa madawa ya kulevya na suala la Usalama kwa ujumla.

Marekani inaishitumu Venezuela kuwa: Inafadhili Magenge ya wauza madawa ya kulevya na inahusika na Usafirishaji wa dawa hizo, pia vile vile Venezuela inafadhili Mitandao ya waharifu wa makosa mbalimbali. Kingine ni Venezuela inafadhili Wanajeshi au wanamgambo wala rushwa wanaohusika na Usafirishaji wa silaha na kadharika.

Baadhi ya tuhuma ni za kweli — lakini tuwe wawazi, Usafirishaji wa madawa ya kulevya ni japo lililopo katika ukanda wote wa Amerika ya Kilatini (Latin America) huko Amerika Kusini. Na si nchi ya Venezuela pekee, lakini nchi nyingine za ukanda huo mfano Mexico hazipati shuruba kali kama namna Venezuela anavyopelekewa moto kwa issue ya madawa ya kulevya.

Kwa hiyo ni nini kiini cha sababu ya ugomvi huo?

Katika sentensi moja ni kuwa:

Hizi story nyinginezo ni mbwembwe tu za kisiasa ila ukweli, Marekani ni king'ang'anizi, ni kama mtu anayelazimisha mahusiano kwa nguvu sehemu hasiyopendwa.

⚠️ Ukweli mchungu (No Sugar-Coating)

Marekani ni nchi isiyotaka kuvumilia upinzani wa aina yoyote iwe wa kimkakati au lah katika ukanda huo wa Amerika ya Kusini au Kaskazini. Mpinzani yoyote atakayepinga sera za Marekani katika ukanda wa Amerika basi uchukuliwa kama adui moja kwa moja.

Vikwazo na shinikizo vinalenga kuvunja upinzani dhidi ya Marekani, na si kuingia katika mazungumzo.

Mkakati endelevu ni kuwa Ugomvi hautaisha mpaka: Venezuela ibadilishe uongozi au Vipaumbele vya Marekani vifanyiwe kazi au kuwe na mabadiliko makubwa ya utawala wa kimataifa yani atokee mbabe mwingine atakayeweza kumnyamazisha Marekani.
Mkiani mwa huyo mnyama anayeitwa Marekani, yuko Cuba, tusubiri aingie hapo pia!
 
Wanasema nini Madini Hadimu yaan Rare Earth Minerals
Madini adimu yako 16 mengi yakiwa kundi la lanthanums mfano Scandium,Yittrium,Lanthanum,Cerium,praseodymium,promethium,samarium,europium,gadolinium,terbium,ddysprosioum,holmium,thallium,ytrebium,lutetium.
Haya madini yanatumika kwenye electronics,lasers,magari ya umeme,wind turbines,kwenye matibabu kama cancer na kutengeneza baadhi ya components za rocket na ndege.
 
Sasa WU A U anasema Wamarekani na wengine wapenda haki wanataka kubeba madini yetu kwa hio anasisitiza tuitetee Amani tuachane na haki ili Wamarekani wasije wakayachukua.. ukiangalia upande wa pili wa shilling yeye sio muumini wa Amani ila hapendi haki
 
Hapo nimekusoma

Ingawaje Maduro nae ana makando kando yake kwa raia lakin isingeweza kufanya marekan ajitoe hvyo kwa raia wa nchi nyingine
 
Keep it civil. Wapi nimesema serikali ya Marekani haiwezi kufanya maamuzi kinyume na matakwa ya raia wake? Mimi nimekupa analysis yangu kwamba Trump katumia discretion aliyonayo kisheria kufanya maamuzi ambayo hayaungwi mkono na Wamarekani wengi including some of his own subordinates. That was my point. Na hapa tunazungumzia spefically about Venezuela. Waliovamia Iraq, Libya nao walikua na motivations zao and they paid a political price for their decisions. Na hizo missions zote mbili zilifeli na hivi leo wanakiri. National interest can be used as an excuse for elites to implement policies that are not in the interest of a nation at all. Unalijua hilo?
Alichafanya Trump ni long term goal ya Mmarekani, na sio matakwa ya Trump.... hao wamarekani wanaompinga ni wanafanya kupoteza maboya tu, hili muone Marekani ina demokrasia. Lakini yeyote akikaa kwenye icho kiti ni lazima afanya jambo kwa maslahi yaliyoangwa muda mrefu

Badae nakuja na Uzi humu juu ya tukio hilo kuonesha ni lilipangwa kitambo

Soma huu uzi: Series ya Jack Ryan S02 (2019): Ilitabiri Tukio la Venezuela — Miaka 6 Baadaye Marekani Ikapiga kwenye mshono
 
Mkiani mwa huyo mnyama anayeitwa Marekani, yuko Cuba, tusubiri aingie hapo pia!
Cuba ni nchi ndogo sana kwa Marekani, haina jambo la kuishitua Marekani kuanzia jeshi, uchumi, hadi rasilimali.... Cuba ingekuwa na Rasilimali ingekuwa ishapigwa kitambo... Cuba kaachwa abweke tu... Marekani uwa anapigana na Big Fish tu, yani samaki wakubwa na tishio kwake
 
Alichafanya Trump ni long term goal ya Mmarekani, na sio matakwa ya Trump.... hao wamarekani wanaompinga ni wanafanya kupoteza maboya tu, hili muone Marekani ina demokrasia. Lakini yeyote akikaa kwenye icho kiti ni lazima afanya jambo kwa maslahi yaliyoangwa muda mrefu

Badae nakuja na Uzi humu juu ya tukio hilo kuonesha ni lilipangwa kitambo

Soma huu uzi: Series ya Jack Ryan S02 (2019): Ilitabiri Tukio la Venezuela — Miaka 6 Baadaye Marekani Ikapiga kwenye mshono

I don't buy your conspiracy theory. If what you are saying was true Republicans and Democrats wouldn't bittery campaign against each other over foreign military interventions. Wamarekani wanakubaliana kwamba Maduro is a dictator who destroyed his own country. Na wengi wanafurahia kwamba he is no longer running the country. Ila majority wanapinga sababu zilizotumika kumtoa na zinazotolewa hivi sasa kuhalalisha Marekani kuiongoza Venezuela.

Sababu zinazotolewa zinaonekana ni maslahi ya wachache na siyo national interest. These are facts. Wapo wanaongea and they are on record. Tarajia Trump kuanza kujitoa kwenye mpango wake kutaka kuitawala Venezuela kiuchumi taaratiiibu kadiri upinzani dhidi yake juu ya hili suala utakapozidi kuongezeka na kukigharimu chama chake kisiasa.
 
Wewe anaongelea maoni ya wananchi, mimi nakupa Mipango ya CIA... Rais yeyote anayeingia madaraka lazima aihakikishie Marekani nguvu na ushawishi wa kutawala Dunia, Global Dominance....

Wewe unaongelea sijui eti sijui national interest na maslahi ya wachache.... kwani unajua Global na national interest za Marekani ni zipi?

Kumtoa kiongozi kinguvu haijaanza Leo wala jana, marais wengi tu walioenda kinyume na matakwa ya Marekani walitolea kwa mfumo huo, at least huyu yeye kakamatwa na kupelekwa mahakamani... wenzake walipigwa risasi na kuuwawa mfano kina Gaddafi. Haijalishi ni chama gani kinaingia Madaraka, interest za Marekani za World Dominance zinabaki pale pale... nitajie Rais yeyote wa Marekani ambaye ameingia madarakani na hakufanya alichofanya Trump
 
Give me a break. Wewe "Mhaya" unajua "Global na national interests" za Marekani? Uliona comment ya Vice President wa Marekani wa sasa iliyo leak kwenye Signal Chat App? Alipinga Trump kushambulia Iran. Huyu ni kiongozi msaidizi wa Trump. Kwenye hiyo leaked conversation aki chat na members of the national security team, alinyakwa akitoa maoni yanayopingana na msimamo wa boss wake. Maoni yake siyo maoni ya average citizen tu.

Unasema nikutajie Rais yeyote wa USA ambaye hakufanya alichofanya Trump Venezuela. Biden alimtoa rais wa nchi gani madarakani? Jimmy Carter? JFK? Weengi tu - in fact wengi wao - hawakufanya alichofanya Trump. Jifunze tofauti kati ya conspiracy theories na empirical evidence. Empirical evidence ni facts. Conspiracy theories ni maoni ambayo yanaweza kuwa yanashawishi ila bado yakawa hayana ukweli. Maoni yako ni conspiracy theory for the most part.
 
Nikisema wewe jamaa bado ujui kitu husikatae... bado unaamini propaganda za Mmarekani kwamba Makamu wa Urais chat zake zimevuja kwenye ukimwengu huu wa A.I na propaganda. Kwa akili zako unahisi Chat za kiongozi wa Marekani mwenye cheo icho zinavujishwa kiboya tu. Na ikitokea chats zimevuja basi jua ni moja ya Mpango wa Propaganda. Na Marekani ni bingwa wa hizo mambo, ile nchi ikikupoga Propaganda unaweza hata mwenyewe kujikataa.

Tukija kwenye swala la Rais gani wa Marekani kamngoa nani, hii issue sio kama kuamka na kupika maandazi ni mpango mkakati endapo utaenda kinyume na matakwa yap. Hii issue hapangi Rais, zinapanga Mamlaka za kijasusi... Rais analetewa file mezani yeye anatoa tu Go Ahead... wazee wanaingia kazini... na sio lazima kila uongozi mtu atolewe madarakani, inategemea kwa wakati huo wanataka nini na nani anawazengua ku-accomplish mission zao.

hebu tuiweke sawa kwa historia, nguvu, na ukweli wa kisiasa—bila drama, bila conspiracy, bila kuchanganya majina juu ya marais uliowataja

JOE BIDEN alifanya ubabe kupitia PROPAGANDA na MFUMO, SIO MAPINDUZI ya moja kwa moja

Biden hakumtoa rais yeyote maarufu madarakani moja kwa moja. Lakini chini yake, Marekani iliendeleza ubabe kwa njia hizi:

(a) Ukraine vs Russia

Biden aliiongoza NATO kuisaidia Ukraine kumdhoofisha Urusi, Aliweka sanctions kali sana dhidi ya Russia, Alidhoofisha Uchumi wa Russia na Influence ya Putin Ulaya. Huu ni ubabe wa kimkakati, si kuondoa rais

(b) China

Biden aliendeleza vita ya kiuchumi na kiteknolojia mfano Chip bans, AI restrictions, alliances Asia-Pacific lengo ikiwa Kuzuia China isiwe “boss wa dunia”

(c) Middle East

Aliendeleza ulinzi wa Israel kutuliza mataifa ya uarabuni hasa kuinyamazisha Palestina. Akaweka pressure Iran kupitia sanctions na proxy containment

3. JIMMY CARTER yeye alitumia kitu kinaitwa SOFT POWER

Jimmy Carter (1977–1981) alikuwa tofauti kidogo: Alifanya nini? Alitumia mambo ya kutetea haki kama silaha ya kisiasa

Alitumia Diplomasia, Mikataba (Camp David Accords – Israel & Egypt), Aliepuka vita kubwa
Matokeo yake Marekani ilionekana “dhaifu”, Ilipoteza heshima kimataifa.

Maamuzi yake yaligharimu Marekani pakubwa, kiasi kwamba kuna wamarekani 66 walitekwa kwenye ubalozi wa Irani na kisha waakchilia wakabaki 52 mateka. Baadae Rais huyo akatuma kikosi kikawaokoe mateka huko Iran lakini bado wamarekani 8 walifariki.

Kwa kifupi utawala wake alichukuliwa kama Utawala mbovu na dhaifu hasa kwenye falsafa za kueneza ubabe, baada ya Miaka yake 4 kuisha alivyogombea tena kwa Muhula wa Pili aliangukia pua, wamarekani wakamtema. Akaishia kutawala Muhula mmoja tu wa miaka 4, wakati Marais wengi utawala mihula 2.... Marekani ukiona unatemwa ndani ya Muhula mmmoja basi jua Taifa limeona hakuna kitu umefanya, na ndio kilichotaka kumkuta Trump baada ya kutaka kuleta mambo ya utawala wa Amani. Lakini akapigana akarudi tena na sasa anaeneza ubabe

Baada ya Jimmy Carter kushindwa kwenye uchaguzi wa Muhula Ndiyo Reagan, Reagan alikuja na mkono wa chuma, alitembeza kichapo vibaya mno kwa maadui wote wa Marekani.

4. JOHN F. KENNEDY (JFK) – UBAABE WA BARIDI (COLD WAR)

Huyu sasa alikuwa alpha male wa Cold War (vita baridi).

JFK alifanya nini kuweka dominance?

Kuna hii issue ya Cuban Missile Crisis (1962), mchiz alisimama kidete kupambana dhidi ya USSR (Urusi). Labda nikueleze kidogo. Cuban Missile Crisis ilikuwa mgogoro hatari zaidi wa Vita Baridi, ambapo dunia ilikaribia kuingia vita ya nyuklia kati ya Marekani (USA) na Soviet Union (USSR) kwa muda wa siku 13 (Oktoba 1962). 1959: Fidel Castro anapindua serikali iliyokuwa inaegemea Marekani. Marekani ilijaribu kumng’oa Castro (Bay of Pigs – 1961) → ilishindwa vibaya. Cuba ikageukia USSR (Urusi) kwa ulinzi. Marekani ilikuwa tayari imeweka makombora ya nyuklia Turkey & Italy, karibu na USSR (Urusi). USSR ikaamua kuweka makombora Cuba, umbali wa km ~150 tu kutoka Florida. Hii ilikuwa provocation ya kiwango cha juu. Oktoba 1962: U-2 spy planes (ndege za kishushushu) za Marekani zapiga picha makombora ya nyuklia Cuba. JFK apata taarifa → mgogoro ukaanza rasmi. JFK akajibu mashambulizi kwa kuzuia meli za Soviet kufika Cuba. Dunia itagawanywa wanajeshi walikuwa tayari kupigana vita. Ndege ya Marekani ikapigwa Cuba, majeshi ya Marekani yakataka kuanzisha mashambulizi badae JFK anakataa ushauri wa mashambulizi ya moja kwa moja. Badae wakafanya makubaliano USSR ikakubali kutoa makombora Cuba, Marekani nayo akakubali Kutoivamia Cuba na Kuondoa kwa siri makombora yake Turkey.

Badae Mwaka Mmoja akapigwa Risasi na kuuwawa, hivyo alitawala miaka 3 tu (miaka 2 na miezi 10), Lakini, ndani ya historia ya mauwaji yake, kuna mvutano mkubwa kuhusu mashirika yaliyohusika, kama CIA au mafia ndio waliomuua, lakini hakuna ushahidi wa kisheria uliothibitisha hayo.

Punguza kushupaza shingo... Marais wengi wa Marekani wanaingia wanakuta tayari kuna Agenda... Rais yeye anapewa miongozo tu na anabaki kusema ndio au hapana tusifanye
 
Asilimia 99 ya ya comment yako hii ni conspiracy theory. Unatumia seemingly logical connection of events kama ushahidi. Napenda kuamini kwamba wewe ni msomi na unajua tofauti kati ya correlation na causation. Ukiwa muumini wa conspiracy theory kupitiliza unakuwa huna tofauti na wanaoamini ushirikana. Yaani kwako wewe matukio yakionyesha uhusiano hata kwa mbali tu basi ni ushahidi tosha. That is not the best way of looking at things intelligently.

Tuachane na hilo. Sasa nikuulize tu, kwa mfano, ni chombo kipi cha serikali ya Marekani ambacho huwa kinapanga agenda ya maslahi ya nchi ambayo kila Rais ni lazima aifute? Je hicho chombo hakina political influence? Kina binadamu wa aina gani ambao hawana upande au misimamo binafsi au misimamo ya kimakuzi na kitamaduni au kidini juu ya masuala ya kiataifa kiasi kwamba kisiwe influenced na rais au chama kilichopo madarakani au mitazamo ya kijamii kwa nyakati husika?

Kama unaamini kwamba mifumo ya kiutawala ya Marekani ni "peferct" kiasi kwamba makamu wa rais wa Marekani haweza kukosea akaandika au kusema jambo likavuja basi huenda pia huamini kwamba Bill Clinton taarifa zake za kunyonywa uume na binti intern wa ikulu na kuvuja ni za ukweli. Pengine pia huamini kwamba taasisi za kiutawala za Marekani zinaweza kufanya makosa kiasi cha kuhatarisha au kusababisha rais kuuwawa au kujeruhiwa kama Trump alivyojeruhiwa hivi karibuni tu kule Pennsylvania vijijini.

My friend, kwa kifupi ni kwamba, pamoja na uwezo wake mkubwa ktk maeneo mengi, ukilinganisha na serikali za nchi nyingine, serikali ya Marekani pia huwa inafanya makosa mengi sana tu ya kipumbavu na huwa inafeli mbaya sana tu kuanzia ktk kufikiri, kupanga na kutekeleza mipango yake. Pia mambo mengi mnaidhania Marekani inayajua au inafanya siyo ya kweli. I am sory to sound patronizing but I doubt una uzoefu wa kimaisha wa kutosha na nchi ya Marekani. Ungekua unazoefu huo kuna mifano fulani halisi kabisa ningekupa naamini ungenielewa ninachokisema. In short many things that are being said about the U.S are not true. Ni conspiracy thoeries tu. I rest my case.
 
Back
Top Bottom