Bajeti ya kunguru
JF-Expert Member
- Sep 21, 2014
- 1,388
- 1,094
Habari zenu mabaharia wote mliomo humu. Mara nyingi mtu akiita mabaharia jinsia ya kike huwa wanajiweka pembeni sasa sio kwa salamu yangu,mimi nimewalenga nyote.
Sasa niende kwenye kaburi langu halafu nione kama nitatoka au nitafiamo mazima. Naita kaburi kwa sababu ni kazi ngumu sana kueleza mapenzi kwa watu na wakaelewa kwa kiwango kile kile ambacho menyewe hayaonekani lakini navaa bomu hili kama nitatoka poa kama litanilipukia basi. Sasa maisha ya ndoa nyingi yanategemea sheria za ndoa kuendesha uhai wake kitu ambacho ni kinyume na mapenzi ila dunia haijui kwahiyo hapa nilazima nikuwekee chanzo kwanza cha mapenzi kwani ukiujua mwanzo mwisho hautakusumbua.
Chanzo cha mapenzi ni nguvu iliyopo nje ya mwili wa mwanaume ambayo 99.999% ya wanaume hawaijui kama ipo na uwezo wake wa kufanya kazi ila wanawake wote wanaijua vizuri na wanaimani kwa 100% kila mwanaume anayo. Nguvu hii huwashwa/huwaka na kuzima. Chanzo cha kuwaka ni ukimya wa uumbaji (nauweka kiporo).
Sasa basi nguvu hiyo ndiyo inayotafutwa na wanawake na wakiipata basi safari yao inakuwa imefika mwisho yaani maisha kwao yanamaana kubwa endapo tu watafanikiwa kuipata nguvu hiyo. Majaribio mbalimbali hufanywa na wanawake sio kukupata wewe bali kujaribu kuiwasha nguvu hiyo,wewe ni mbebaji tu wa nguvu hiyo ambayo ndio chanzo cha mapenzi. Majaribio hayo ni kama kukuita jina lako kwa kulilemba,kuinama mbele yako akiigiza anaokota kitu na mengineyo (mitego).
Chukulia mnapita njiani usiku mkakutana hali ya joto njiani halafu mkalivuka kuna ukimya hutokea ghafla. Najaribu kuielezea nguvu hiyo ambayo huwashwa na ukimya wa uumbaji. Au chukulia mfano mvua inanyesha halafu umwambie mkeo muende buchani mkanunue nyama,ukiwa umeshika mwamvuli mkiwa katikati ya safari kwa kuonesha umeridhika usimame halafu umwambie kwa mahaba "nilikuwa sijawahi kuvuka barabara na wewe mvua ikiwa inanyesha" (hali ambayo itatokea hapo ndio ukimya wa uumbaji halafu itawasha nguvu hiyo ya kiume na mwanamke ataona mapenzi japo hayashikiki).
Kwahiyo chanzo cha mapenzi kipo kwa mwanaume na kama ukikiaply mwanamke yoyote katika dunia hii anageuka mali yako. Kwa hivyo basi ili maisha ya ndoa yasitegemee sheria nilazima chanzo hiki mwanaume ajijengee uwezo wa kukiamsha mara kwa mara{hata kama unamtongoza mwanamke yale maneno yako huwa sio kitu sana kwake wao huwa wanaiangalia hiyo nguvu kama imewaka na akiigundua imewaka ndio hujua unachokisema hakika unamaanisha}.
Kwanini nguvu hiyo ambayo ndio chanzo cha mapenzi iwake mara kwa mara? Ni kwasababu hii; chukulia mchezo wa mpira mnagombania kombe mkisha lipata/mkisha lishinda linakuwa sio kitu kigeni tena yaani linakuwa kitu cha kawaida. Sasa katika maisha ya mapenzi hakuna kuushinda uanamke/moyo wa mwanamke haushindwi kwamba umeshinda kama vile kombe, abadani. Kwani ukimya wa uumbaji hauna mwisho hivyo kutokuamka/ kuwaka kwa nguvu hiyo ambayo ndio chanzo cha mapenzi kwake ni ishara nyingine, huenda umepunguza mapenzi kwake, huenda unamwingine na uchafu mwingine kama huo...
ITAENDELEA.
MAGUFULI4LIFE.