Chanzo cha Kisukari, Kansa, Ukimwi hiki hapa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanzo cha Kisukari, Kansa, Ukimwi hiki hapa...!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mediaman, Mar 23, 2011.

 1. mediaman

  mediaman Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zilizoandikwa katika gazeti la Mwananchi zinasema kwamba "barabara inayokwenda kwa babu Loliondo inazidi kuharibika na kusababisha mamia ya wagonjwa na jamaa zao kukwama porini. Zaidi ya abiria 600 waliokuwa wanatoka Arusha kwenda huko wamekwama umbali wa kilometa 306 kutokana na ubovu huo. Hadi kufikia juzi, idadi ya magari yanayopeleka wagonjwa kwa Mchungaji Mwasapile yanakadiriwa kufikia 40,000."

  Habari hizo zinaonyesha jinsi Tanzania ilivyo na maelfu ya watu wenye magonjwa mabaya(sugu). Kwanini watu waugue namna hii? Tatizo ni nini? Chanzo ni nini? Katika kutafuta jibu la swali hilo nimekutana na Maandiko katika Biblia, kitabu cha Kutoka, yanayosema kwamba Mungu aliwatia(aliwapa) Wamisri, maradhi(magonjwa) mabaya kama vile tauni nzito sana na majipu yenye kufura na kutumbuka kwa sababu ya dhambi zao. Nilipoendelea kusoma kitabu hicho nikaona maandiko mengine ambapo Mungu aliwaambia Wana wa Israeli kwamba hatatia maradhi juu yao kama alivyofanya kwa Wamisri. Hata hivyo aliwaamuru waisikize kwa bidii sauti ya BWANA Mungu, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio wasikie maagizo yake, na kuzishika amri zake. Kinyume cha hapo na wao wangetiwa maradhi mabaya kama Wamisri.

  Yamkini Watanzania hatutaki kuisikiliza sauti ya BWANA Mungu ndio maana tunapatwa na maradhi mabaya. Yawezekana hatutaki kutenda mambo mema na yaliyo ya haki. Hatutaki kutii amri zake. Na hapo pana ukweli. Angalieni vitendo vya rushwa vilivyokithiri. Watu wanachakachua kura. Watu wanawaua Albino na kuchuna ngozi za binadamu wenzao eti wapate utajiri. Ubadhirifu wa mali ya umma, wanyonge hawapewi haki zao, majambazi wanaiba fedha benki, biashara ya ukahaba/uzinzi imeshamiri mpaka kwenye tovuti, mishahara inatolewa kwa wafanyakazi "hewa", wanafunzi wanaiba mitihani, waandishi wa magazeti nao wanadiriki hata kuandika habari za uongo ili kuvuna bila jasho! Matusi hata kwenye jamvi la JF. Madawa ya kulevya, pombe, kashfa, dharau… Hayo ni machache tu katika maovu mengi tunayoyaona hapa Tanzania.

  Jamani wana JF, Mungu yupo. Ni kweli ana huruma, lakini upande mwingine anaghadhibika sana tunapomkosea kwa kufanya maovu kama hayo, na anaweza kutuangamiza ghafla hata tukifanya mazoezi ya kujikinga na hatari kama walivyokuwa wakifanya Wajapan kila mwezi. Sikia Mungu anavyosema katika Yeremia 30:12-15 "maumivu yako hayaponyekani, na jeraha yako ni kubwa…kwa jeraha yako huna dawa ziponyazo…maana nimekujeruhi…kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako…Mbona unalilia maumivu yako? Hayaponyeki…kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya." Kumbe dhambi zinaweza kumfanya Mungu atutende mabaya.

  Sisi tumewazidi nini Wamisri waliopata mapigo kwa sababu ya kiburi na ugumu wa mioyo yao? Je, tu watakatifu kuliko wao? Kama sivyo, tusishangae basi tunapoyaona magonjwa sugu(kisukari, kansa, pumu, ukimwi) katika miili yetu. Na wala tusimlaumu Mungu. Mungu hapendezwi na matendo ya dhambi kabisa. Miriam alipomsema vibaya mtumishi wa Mungu, Musa, alipata ukoma. Mungu aliiangamiza miji ya Sodoma na Gomora kwa sababu ya uzinzi na maovu mengi yaliyokuwa yakifanyika katika miji ile. Wakati wa Nuhu, watu wote(isipokuwa Nuhu na jamaa yake) waliangamizwa kwa gharika kwa sababu ya kutotaka kuyashika maagizo ya Mungu. Wakati wa Matendo ya Mitume Anania na Sa**** walipata adhabu ya kifo kwa kuficha sadaka/fungu la kumi na kusema uongo!

  Nafikiri huu ni wakati mwafaka wa kubadili tabia zetu na kuanza kumcha Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Labda sasa unasema, "Ah hata tukiugua, babu yupo Loliondo tutapata kikombe!" Unaweza kufia njiani kabla hujafika kwa babu, si umesikia foleni ilivyo ndefu? Hata kama hakuna foleni, unaweza kufa njiani kwa ajali. Na hata baada ya kufika huko unaweza usipone kama ndugu zake Rostam na majirani zangu walioenda huko! Na hata ukipona, kesho utaugua tena maana chanzo cha magonjwa hujakiondoa. Ukinywa dawa ya kutibu malaria, utapona; lakini usipoondoa vyanzo vya mbu wanaoleta malaria nyumbani kwako, utaugua tena malaria baada ya muda mfupi.

  Vipo vyanzo vingi vya magonjwa, lakini kama tulivyoona katika maandiko yale, inaonekana wazi kuwa dhambi ni chanzo kimojawapo cha magonjwa sugu yasiyoponyeka. Katika Yohana 5:14 Yesu alimwambia yule mtu aliyeponywa(na Yesu) "...Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."

  Sio rahisi kukiondoa chanzo hicho kwa nguvu na jitihada zetu. Lakini tukitubu dhambi zote na kuziacha na kumpokea Yesu kwa imani katika mioyo yetu, awe Bwana na Mwokozi wetu tutapewa(na Yesu mwenyewe) uwezo wa kushinda dhambi(Yohana 1:12; Warumi 8:37). Hapa na pale, tutaugua, maana bado tupo duniani, lakini kama Mungu alivyoahidi, hatatia maradhi mabaya juu yetu kama yale aliyowatia Wamisri, maana Yeye ni BWANA Mungu atuponyaye. Tukitubu dhambi na kuziacha na kumwamini Yesu, tutakuwa pia na uhakika wa kuingia mbinguni baada ya kufa. Huwezi kukwepa kifo kwa kupata kikombe cha babu. Babu mwenyewe ana miaka michache iliyosalia ya kuishi, maana miaka yetu ni 70 au 80 tukiwa na nguvu(Zaburi 90:10). Tusisahau, watakaoingia mbinguni ni watakatifu tu(Ufunuo 21:27). Tukiingia mbinguni tutastarehe milele na milele maana huko hakuna magonjwa wala kifo.
   
 2. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  .... kwa hakika sipendi kuona matatizo hasa ya maradhi yakisumbua mwili wa mwana-adam.
  Madhambi ni chanzo cha magonjwa.
  Na sio wote wafonjwa wanayo madhambi.
  Lakini huyo Bwana uliemtaja hapo ndie Mungu?
   
 3. mediaman

  mediaman Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BWANA ndiye Mungu. Ndio maana Jina hilo limeandikwa kwa herufi kubwa. Katika Biblia Jina hilo limeandikwa mara nyingi likimaanisha Mungu. Na katika vifungu vingine imeandikwa: BWANA, Mungu. Kwa mfano Mwanzo 2:18.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Unweza ukawa sahihi ndugu lakini onyesha moyo wa upendo kwa wenzio waliokuwa wagonjwa! Utasemaje kwa wanaozaliwa na kisukari? Wanaopata UKIMWI kupitia damu yenye virusi au wanaozaliwa kwa vile wazazi waliathirika?
  Usirukie kuhukumu kuwa wote wana dhambi.
  Ingekuwa vipi kama wewe ungezaliwa ukiwa na virusi kwa sababu mama yako alikuwa muathirika? Ingekuwa vipi kama ungepata saratani? Hujafa hujaumbika!
   
 5. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Maana
  Bwana ndie Mungu.
  Yesu ni nani?
  Usinijibu kwa jazba humu hua twaeleweshana kwa hoja!.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Akubariki almighty the Great! kweli umeongea kama nabii..
  Huku akina dada wanatoa mimba mithiri ya uchafu tumboni.,kule baba kamlala bintiye..pale mapadre/mashee wamewageukia akina dada na wajane..juzi tu,eti wachungaji nao kumbe wanaabudu misikule na kuishi nayo madhabauni...acha muumba atuadhibu!
   
 7. mediaman

  mediaman Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hiyo post hujaisoma kwa makini. Nimeandika kwa herufi nzito(bold) kwamba chanzo kimojawapo cha magonjwa sugu ni dhambi. Najua vipo vyanzo vingine kama hivyo ulivyovitaja.
   
 8. mediaman

  mediaman Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jazba iko wapi? Au kwakuwa nimeandika maneno machache?

  Yesu anaitwa Mwana wa Mungu. Lakini pia ni Mungu.
   
 9. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nina kisukari na ninatamani kum-tusi mwenye hii sredi, kweli vile!
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Crap.
  Chanzo cha magonjwa ni dhambi?'
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Mtukane tu, hana adabu huyu.
   
 12. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  asante mkuu
   
 13. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ban inaweza kuongeza blood glucose bure nishindwe hata kuinjoi maisha haya ya sindano twice a day
   
 14. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo unachanganya watu....
  Mungu awe mwana....muda mwingine awe Mungu???
  Yesu amekataza asiitwe mwana wa Mungu soma Luke:4:41.
  Mungu hana mfano soma Isaya : 46:5
  Kama Yesu ni Mungu....hapa Yesu aliomba kwa Mungu. Soma Luka 6:12 ...ni Mungu gani mwingine? Kuna Miungu wangapi?
   
 15. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  naona utakuwa muislam ukianza kuhoji iman ya kikristo utachoka ila kwa ufahamu wako YESU NI MUNGU SOMA ISAYA 9:6 NA INJILI YA YOHANA 1:1 na kuendelea utaelewa kwa nn yesu ni Mungu. Biblia hiyo hiyo inatuambia Mungu ni moja na hapana Mungu mwingine lazima uelewe sisi tunaamini utatu mtakatifu BABA MWANA NA ROHO MTAKATIFU HUTENDA KAZI KWA PAMOJA.Kibinadamu hutaelewa ila kwa kufuniliwa na Roho Mtakatifu,sijaelewaa ninnyi mwafunuliwa na nani. Mchungaji Mediaman atakuongezea zaidi.
   
 16. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Eee!! Bwana wangu naomba niongezee ulinzi kinywani mwangu.
   
 17. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu watu tu watumishi/wapendwa na tunaumwa
  acha kabisa iyo maneno sema ni sehemu tu,ila kuna upande wa pili yanakutokea tu

  njoo hospitali uone watoto wanavoteseka ndipo utasema "je ni dhambi ya wazazi?"

  la hasha
   
 18. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nimefuatilia sana thready yako lakini hii kwanjia moja au nyingine nakupa BIG UP binadamu tuwache dhambi! Lakini kuna Post yako moja hapa ulijaribu kama kuwazuia watu wasiende kwa babu kule Loliondo kupata dawa na kudai kua babu yule ni tapeli sasa naona kama unajikaanga kwa mgongo wa chupa kwakupitia hii thready yako! Halafu unajaribu kama kuwatishia watu na wewe kujifanya kama nabii fulani, lakini sikushangai sana kwakua hapa nakuona bado ni mgeni sana lakini karibu.
   
 19. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wapone afya ya Utu Ndipo watapona afya ya magonjwa...!!

  Dawa + UTU = KUPONA

  Asiye na utu na asinywe dawa hatapona!!

  DHAMBI sio UTU!!

  wanasiasa wahubiri utu, viongozi wahubiri utu, watanzania wapende utu, utu ni afya!!
   
Loading...