Onyo Kwa Mtu Anayesababisha Wengine Watende Dhambi

Onyo Kwa Mtu Anayesababisha Wengine Watende Dhambi

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,206
Reaction score
1,695
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
Luka 17:1 BHN

Tunaweza kumlaumu aliyefanya dhambi, hatukosei kumlaumu, na hakwepi lawama na hukumu ya Mungu kwa matendo yake maovu/machafu.

Kutenda dhambi hakutokei ghafla bila sababu, kunakuwa na visababishi vinavyomfanya mtu atende mambo yanayomkasirisha Mungu.

Wasababishi wa wengine kumtenda Mungu dhambi wapo, watu wanaowavuta wengine kwenye mabaya wamkosee Mungu wao.

Watu hawa hawajaachwa na Mungu, wamepewa onyo kali, mtu yeyote anayewasababisha wengine wamtende dhambi Mungu wao wajue hawapo salama.

Tujue kuwa visababishi vinavyomfanya mtu atende mambo machafu haviwezi kukwepeka kwa kila mmoja wetu tukiwa hapa duniani.

Mtu mwenyewe anao uchaguzi wa kuamua kuingia kwenye mtego aliotegewa au kuukwepa huo mtego.

Tupo duniani, tutaendelea kukutana na vishawishi vya kututaka tuingie kwenye eneo baya, wale walinaotengeneza mazingira ya kutuingiza maeneo ya kumkosea Mungu, wana hatia mbele za Mungu.

Mtu anayewasababisha wengine waanguke dhambini asijidhanie yupo salama, ajue jicho la Mungu lipo juu yake na limtazama kwa ukali.

Asijifiche kwenye eneo la kusema 'sikuwalazimisha wanifuate au wanisikilize', hata kama hukuwalazimisha watu, kama umekuwa sababu ya watu kutenda uovu, ujue mbele za Mungu una hatia kubwa.

Mwili wako ukitumika kuwashawishi watu wamtende Mungu wao dhambi, ujue haupo salama mbele za Mungu.

Kinywa chako kikitumika kuwashawishi watu wanatende yaliyo maovu, nawe utakuwa kwenye kundi la watenda dhambi.

Mikono yako ikitumika kutengeneza vitu vinavyowafanya wengine wavutwe kutenda dhambi, ujue na wewe utakuwa kwenye kundi la watenda dhambi.

Ukurasa wako wa mtandao huu ukitumika kuwashawishi wengine wamtende Mungu wao dhambi, ujue una hatia kubwa mbele za Mungu.

Kufahamu haya kutuweke mbali na dhambi, tusiwe miongoni mwa watu wanaowavuta wengine kwenye mabaya ya kumsokosea Mungu wao.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom