Chanzo cha ajali ya Delux Bus Service ni kupasuka tairi au mwendo kasi?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wanaJF, kwenye taarifa ya habari ya saa 3:30 usiku (October 26,2011), nilimsikia Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (traffic police) kupitia Mlimani TV akielezea chanzo cha ajali ya Delux Bus Service akisema siyo mwendo kasi kama baadhi ya abiria walivyodai bali ni kupasuka kwa tairi kulikopelekea bus kupinduka na kuwaka moto. Alisema hayo yalibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na Kikosi cha Usalama Barabarani. Kwa mawazo yangu, uchunguzi unapofanyika wanaoweza kutoa uhalisia wa tukio lenyewe ni ‘eyewitnesses’ – hawa ndio ‘primary source of information’. Kupata chanzo cha habari nje ya ‘eyewitnesses’ inakuwa ‘reconstruction’ ili kupata ‘conclusion’ fulani inayoendana na lengo la wachunguzi. Kwa maelezo ya kamanda, alidai si rahisi kwa abiria kubaini mwendo kasi wa gari maana ‘speed limit’ bus kubwa ni 80km/hr na kwamba bus linalokimbia ndani ya mwendo huo halikimbii mwendo kasi. Mwendo kasi ni pale bus linapokimbia zaidi ya mwendo huo. Kwangu mimi, inaleta maana kusema mwendo kasi unaweza kusababisha (na huenda ndio uliosababisha) tairi kupasuka na hivyo bus kupindika na kuwaka moto kuliko kusema mwendo wa kawaida unaweza kusababisha (au ndio uliosababisha) tairi la bus kupasuka na hivyo bus kupinduka. (Ingawa in rare cases inaweza kutoka na ndio maana tunasema ajali haina kinga). Wakati Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani akielezea ajali hii, nilihisi kuwa alikuwa anajaribu kulitoa jeshi la polisi (traffic police) kwenye lawama maana kama angesema ajali ilitokana na mwendo kasi kama ‘eyewitnesses’ wanavyodai ingeonekana kama traffic police hawakufanya kazi yao vizuri (kama ni eneo ambalo wapo). I could be wrong or right. What’s your opinion?
 
Eyewitnesses wako highly unreliable na kila mtu anakumbuka anachotaka yeye, pia mwendo kasi sio rahisi kusababisha matari kupasuka kama yapo kwenye standard inayotakiwa. Kuchunguza physical evidence ndo njia sahihi zaidi ya kutafuta sababu ya ajali, ikisaidiwa na eyewitness accounts.

Of coz anaweza akawa anadanganya lakini hilo ni gumu sana kujua. Nadhani ni muhimu watuambie kama matairi yalikuwa kwenye kiwango kinachotakiwa, sio kwa vile tairi limepasuka basi ndo mwisho wa hadithi.
 
lakin hata gar likiwa linatembea taratibu linweza kupasuka tair kwhiyo yuko sahihi
 
Tairi kupasuka inaweza kuwa mwendo kasi,kiwango cha tairi n.k. Vipi kuhusu basi kuungua moto? Mbona mengine yanapata ajali hayaungui? Naomba wataalam wa magari watusaidie hapa.
 
Tujiulize njia zingine zinazoweza kusababisha tairi kupasuka, na je vipi kuhusu moto hauwezi kusababisha? Na kama kulikuwa na moto, chanzo cha huo moto ni nini? Huo moto hauwezi kutokeo kabla tairi haijapasuka?
 
Back
Top Bottom