Omnabuzegwe
Member
- Aug 16, 2018
- 95
- 73
Habari za weekend wana Jf.
Nimeonelea niweke maoni yangu kuhusiana na wazo zuri la televisheni ya Taifa (TBC) Kwa kuuona UMUHIMU uliosahaulika miaka mingi wa kuanzisha Channel maalumu ya kuvitangaza vivutio lukuki vilivyopo hapa nchini.
Mimi binafsi nauona ni uamuzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu na kuuleta leo ni jambo si tu jema,bali pia linafurahisha.
Pamoja na wema wa wazo hilo binafsi nimepata tatizo juu ya LUGHA iliyoamuliwa kutumiwa na hii channel. Nilidhania kuwa,kwa vile nia yetu km nchi ni kuitangazia dunia,na huko KISWAHILI ni lugha ngeni kabisa, ni vipi tutaweza kulifikia lengo letu kwa usahihi wake ikiwa tutaendelea kutumia hii lugha yetu?
Je,haingefikirika kwamba pengine tungetumia KIINGEREZA tungeweza kuifikia dunia nzima kwa urahisi zaidi na kwa sababu wataelewa,huenda ikaongeza motivation yao kuja kuviona kwa macho yao hivyo wanavyovisikia kupitia hii Channel yetu?
Zaidi ya yote pia ningependa nitoe ushauri wangu kuwa wahusika wajitahidi kuvifikia vivutio vyote tulivyonavyo hapa nchini. Tanzania vipo vivutio vingi sana lkn sisi ni km tumejielekeza kwenye mbuga za wanyama pekee,jambo ambalo si sahihi sana.
Natoa mfano wa "NYABHULEBHEKA",lililoko Ukara-Ukerewe. Hili ni jiwe kubwa sana linalocheza kwa kuringaringa pale linapoamriwa na wamiliki wake. Wenzetu wakifika pale hawaachi kurudi tena na tena..! Lifikieni mlitangaze pia