Channel ya Dizzim Online ilipotelea wapi?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Miaka ya nyuma kidogo baada ya Wasafi TV na FM kuingia mjini, basi Dizzim online nayo ikafata na kuingia mjini na mbwembwe nyingi wakifanya interviews bab kubwa na mambo kadha wa kadha. Maendeleo yalizindi kukua na kupelekea kufungua kituo cha TV na Radio na kuoneshwa kwenye Ving'amuzi mbalimbali.

Lakini hivi sasa Channel hiyo ya Dizzim online kule YouTube ina miaka mingi sana hawaweki Video wala content ya aina yoyote, vilevile kule Instagram hatuoni tena hekaheka za channel hiyo iliyokuwa imeanza kupata wafuasi wengi.

Nini kimeisibu Dizzim online?
 
Ukurupukaji ndio sababu.

MEDIA SIO JAMBO DOGO, LINAHITAJI INVESTMENT YA MUDA MREFU.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hiyo chaneli ni kichovu balaa, hata kwenye king'amuzi ninachotumia nako haionekani picha, wakati wenzake akina wasafi tv na e tv wanaonekana. Kwanza muonekano wa tv hiyo hauna mvuto picha ni za hovyo sana. Wakasome kwa zamaradi tv
 
Back
Top Bottom