Chanjo za Corona ni ovyo kabisa

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,152
10,866
Kwa hakika maradhi ya corona yameutikisa ulimwengu pakubwa sana. Kama ilivyo kwa maradhi yenyewe kutokueleweka vyema, pia na chanjo zake zimekuwa za kubahatisha sana kiasa kwamba tunaweza tukaziita chanjo za ovyo.

Chanjo 4 kubwa ndizo ambazo zimeshatangazwa na kuuzwa nje ya nchi zilikotengenezwa.

1. Astrazeneca ya Oxford-Uingereza: Zimetajwa kugandisha damu kwa baadhi ya wallochanjwa. Nchi kadhaa zimewahi kusitishwa halafu wakafungulia. Leo Denmark wamesitisha kabisa na kusema hawana haja nazo tena.

2. Sinovic ya China: Nchi ya mwanzo kununua na kutumia ni Brazil. Inasemekana maambukizi nchini humo kila siku yanaongezeka na juzi China imekiri chanjo hiyo ina ufanisi mdogo sana kiasi cha asilimia 50 tu.

3. Johnson & Johnson ya Marekani: Jinsi inavyotengenezwa kutumia mimba changa imepingwa na wengi na hata ufanisi wake nao una mashaka.Marekani kwenyewe na nchi kadhaa wamesitisha.

4. Sputnik ya Urusi: Haijasikika sana. ufanisi na shida zake hazijawekwa wazi.
Hali zote hizo ni miezi michache tu tangu kuanza kutumika kwa chanjo kuzuia corona.Haijulikani hali itakuwaje kwa waliochanjwa huko mbele

1618411867175.png
 
Back
Top Bottom