Changia kwa hekima, kosoa kwa heshima

Changia kwa hekima, kosoa kwa heshima

Ungehitimisha kwa kumrushia tusi moja hivi heavy ili akili zake zimkae sawa.
Hachelewi kuniita kizazi cha 2000s wakati niko humu tangu jamboforum wakati huo nikija na miaka 16 tu na wengi wa umri wake tumewafundisha sisi kutumia simu kubwa na internet
 
Na unaweza kurogwa pia kwa kutumia angle maalum
Kumroga mtu wa namna hiyo ni dhambi kubwa maana mwenyewe
.Hajasimama kimaisha bado anajitafuta
. Hajasimama kimahusiano ana majanga kama yote
.Hana bado cha kujivunia kwa mipaka aliyoishi hapa duniani
.Ana stress na maumivu mengi moyoni hasira na sononi.. Kumpiga kipapai ni dhambi kubwa.[emoji23]

Jaribu kuwadukua wenye hizo tabia utaniambia walivyo katika uhalisia wao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mrejesho nitatoa kuhusiana na hii mada hasa kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine walishindwa kabisa kujadili hoja badala yake mashambulizi yao wakayaelekeza kwa mtoa hoja in his personality
Kwa namna moja walikuwa wanajaribu kumu outsmart akasirike wapate kujenga mjadala sasa.. Lakini pia wamepata nafasi ya kutoa nyongo zao na sasa pengine wamepunguza maumivu yao na sononi zao

Small minds discuss people.. Smallest minds abuse others without strong reasons ... Kila mada kila reply ni funzo kwa wote, tutumie bando na muda watu vizuri na kwa hali.. Kuna kesho... Na kesho yetu inajengwa leo kwa msingi tuliojenga jana..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamii forums imetoa uhuru wa kutumia utambulisho bandia kwa akili ya kulinda maslahi binafsi ya mwanachama.. Lakini kupewa huo uhuru haina maana uwatweze wengine kwa vile tu hujulikani utambulisho wako halisi

Ndani ya huu mtandao kuna mwanachama wa aina mbili au tatu
1. Wanaotumia utambulisho halisi
2. Wanaotumia utambulisho bandia
3. Wanaotumia utambulisho halisi na bandia
Watu wanakutana hapa hawafahamiani lakini kutokana na mahitaji ya kimaisha na maslahi ya kila mmoja ama ya upande mmoja watu hufikia hatua ya kufahamiana zaidi nje ya huu mtandao

Kuna wajinga wachache wenye uono kimo cha mbilikimo wanaodhani kwa kutumia utambulisho bandia basi wanaweza kufanya lolote na wasijulikane popote bila kujua ya kwamba maandishi hayafitiki.. Ni kupitia maandishi yako ya jana ama hitaji lako la mbeleni unaweza kujifunua na kubaki uchi kabisa

Heshimu sana maandiko ya wengine hasa wale ambao unaishia kuwaona jukwaani lakini hamjawahi hata kuonana.. Hata kama maandiko yake hukubaliani nayo kosoa kwa adabu kosoa kwa heshima..Kosoa kwa hoja jadilifu na si vioja, kashfa, dharau au kejeli!

Heshima muda wake aliotumia kuandika hiyo mada, kifurushi chake, ujumbe na maudhui yake..! Si lazima ukubaliane naye.. Hivyo mpinge kwa hoja zenye mantiki ama mpotezee.. Sometimes kuna kipengele cha kukubaliana kutokubaliana na kinyume chake!

Ukiona mada imeruhusiwa kuwa hewani na kupata wachangiaji... Iheshimu sana kwa maana ina kibali cha kanuni na sheria za jukwaa! Kwa maana ya kwamba imekidhi vigezo vyote vya kuruhusiwa kuwepo hai.. Watu wanaweka mada na hazichukui round zinaliwa kichwa na kutupwa jalalani..

Mada inayoachwa hewani iheshimu sana kulingana na jukwaa lake husika..kitendo cha kuiita ya kipuuzi ama ya kipumbavu si kwamba umemtusi na kumkejeli mtoa mada tu, bali hata wachangiaji wengine na hata walioiruhusu iwepo hewani

Unapokuwa mwanachama mgeni (sio multiple ID) Unakuwa mkweli sana.. Unaongea maisha yako unajitambulisha uhalisia wako na kuomba ushauri hapa na pale. Unapokuwa mzoefu unaanza kuvimba kichwa na kujisahau wewe ni nani uko wapi na unafanya nini.. Unasahau hata background yako na kudhani hujulikani..

Usiwe ndezi kiasi Hicho una background that can be traced to the maximum... Maandishi yako mwenyewe ya awali yanaweza kuwaongoza watu mpaka ulipo na wakakufikia bila shida na wakakufanya chochote watakacho hasa kama hawana hofu na Mungu aliye hai

Kikubwa unapotumia utambulisho bandia usidhani ndio umeyawezea maisha.. Kumbuka bado unaishi na shida hazikomi.. Lakini pia kumbuka una background ambayo kwa namna iwayo yote huwezi kuifuta na watu wanayo mkononi..

Ni hayo tuu
Naomba unisamehe nina mke na watoto wananitegemea pia ni juzi tu nimenunua kiwanja msolwa bado sijajenga.
Pia ni shabiki kindakindaki wa moroko
 
Uzi mzuri sana,

Kuna Uzi nimetukanwa matusi ya nguoni...

Niliumia, sema tu hekima ninayo, nilijibu watu hao kwa hekima...

Wakisoma hapa watajijua
Hata mi mwenyewe kuna sehemu nilitukanwa ila hata sikujibu kitu.

Na mtu anayefanya hivo ni mtu mzima, ana familia kabisa.
umri ule sio wa kusema mambo kama yale..

Nikaja kugundua kuna watu wana shida katika afya ya akili.
 
Hata mi mwenyewe kuna sehemu nilitukanwa ila hata sikujibu kitu.

Na mtu anayefanya hivo ni mtu mzima, ana familia kabisa.
umri ule sio wa kusema mambo kama yale..

Nikaja kugundua kuna watu wana shida katika afya ya akili.
Wengi wana stress za maisha na maumivu mengi rohoni.. Wengi bado wanajitafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ifike mahali member wakongwe wajitofautishe na member wapya.

Hasa kwa kuchangia michango mizuri hata kuweka hoja nzuri.

Ili member wapya waige hekima na heshima za wakongwe.

Tuepuke kuharibu JF yetu ambayo inasifika kwa hoja na michango mizuri.
 
Ifike mahali member wakongwe wajitofautishe na member wapya.

Hasa kwa kuchangia michango mizuri hata kuweka hoja nzuri.

Ili member wapya waige hekima na heshima za wakongwe.

Tuepuke kuharibu JF yetu ambayo inasifika kwa hoja na michango mizuri.
Tuepuke kuharibu JF yetu ambayo inasifika kwa hoja na michango mizuri.[emoji173][emoji419][emoji375][emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom