Changia kwa hekima, kosoa kwa heshima

Changia kwa hekima, kosoa kwa heshima

Jamii forums imetoa uhuru wa kutumia utambulisho bandia kwa akili ya kulinda maslahi binafsi ya mwanachama.. Lakini kupewa huo uhuru haina maana uwatweze wengine kwa vile tu hujulikani utambulisho wako halisi

Ndani ya huu mtandao kuna mwanachama wa aina mbili au tatu
1. Wanaotumia utambulisho halisi
2. Wanaotumia utambulisho bandia
3. Wanaotumia utambulisho halisi na bandia
Watu wanakutana hapa hawafahamiani lakini kutokana na mahitaji ya kimaisha na maslahi ya kila mmoja ama ya upande mmoja watu hufikia hatua ya kufahamiana zaidi nje ya huu mtandao

Kuna wajinga wachache wenye uono kimo cha mbilikimo wanaodhani kwa kutumia utambulisho bandia basi wanaweza kufanya lolote na wasijulikane popote bila kujua ya kwamba maandishi hayafitiki.. Ni kupitia maandishi yako ya jana ama hitaji lako la mbeleni unaweza kujifunua na kubaki uchi kabisa

Heshima sana maandiko ya wengine hasa wale ambao inaishia kuwaona jukwaani lakini hamjawahi hata kuonana.. Hata kama maandiko yake hukubaliani nayo kosoa kwa adabu kosoa kwa heshima..Kosoa kwa hoja jadilifu na si vioja, kashfa, dharau au kejeli!

Heshima muda wake aliotumia kuandika hiyo mada, kifurushi chake, ujumbe na maudhui yake..! Si lazima ukubaliane naye.. Hivyo mpinge kwa hoja zenye mantiki ama mpotezee.. Sometimes kuna kipengele cha kukubaliana kutokubaliana na kinyume chake!

Ukiona mada imeruhusiwa kuwa hewani na kupata wachangiaji... Iheshimu sana kwa maana ina kibali cha kanuni na sheria za jukwaa! Kwa maana ya kwamba imekidhi vigezo vyote vya kuruhusiwa kuwepo hai.. Watu wanaweka mada na hazichukui round zinaliwa kichwa na kutupwa jalalani..

Mada inayoachwa hewani iheshimu sana kulingana na jukwaa lake husika..kitendo cha kuiita ya kipuuzi ama ya kipumbavu si kwamba umemtusi na kumkejeli mtoa mada tu, bali hata wachangiaji wengine na hata walioiruhusu iwepo hewani

Unapokuwa mwanachama mgeni (sio multiple ID) Unakuwa mkweli sana.. Unaongea maisha yako unajitambulisha uhalisia wako na kuomba ushauri hapa na pale. Unapokuwa mzoefu unaanza kuvimba kichwa na kujisahau wewe ni nani uko wapi na unafanya nini.. Unasahau hata background yako na kudhani hujulikani..

Usiwe ndezi kiasi Hicho una background that can be traced to the maximum... Maandishi yako mwenyewe ya awali yanaweza kuwaongoza watu mpaka ulipo na wakakufikia bila shida na 8 bandia usidhani ndio umeyawezea maisha.. Kumbuka bado unaishi na shida hazikomi.. Lakini pia kumbuka una background ambayo kwa namna iwayo yote huwezi kuifuta na watu wanayo mkononi..

Ni hayo tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Usitutishe, yaani ulete mada yako ya kuidhihaki Yanga halafu tukuangalie tu, wewe ni mmoja kati ya members mnaopenda sana sifa mnajifanya mpo karibu na jf hamgusiki, nyie ndio nyie, sasa hakuna na namna lazima tuwaeleze ukweli period.

Unawaasa watu wachangie kwa hekima wakati wewe mwenyewe unabwatukaga tu humu. Siku zote nimenotice wewe unaongozwa na chuki katika vitu viwili SERIKALI na YANGA. Yaani hunaga jema kwa serikali kila kinachofanywa na serikali kwako kibaya, kama unabisha lete mada au comment yako yoyote ukiizungumzia vizuri serikali pale walipopatia.

Ukija upande wa Yanga nako hivyo hivyo kazi yako ni kuiponda tu Yanga mara jezi ya Yanga nzito na shutuma kibao. Pamoja na mafanikio mengi ya Yanga misimu kadhaa ila sijawahi kuona ukipongeza hata mara 1.

Mtu kama Gentamycine pamoja na ujuha wake ila kwenye ukweli anasema tofauti na wewe umejaa chuki. Pia jamiiforum tangu imeanzishwa hakuna zama zilitokea eti members wote wakawa cream and clean, kutofautiana kupo na wakati mwingine watu hutokea kutukanana na kugombana tangu jambo forum ilikuwa hivyohivyo na yote ni kwa sababu hatuko sawa humu, ila mara nyingi unakuta kwenye mada hii watu wanacharukiana balaa ila kwenye mada nyingine wanaungana mkono same members na hii ni kwa sababu ya uhuru wa maoni kila mtu anatoa maoni kulingana na mtazamo wake.
 
Jamii forum ni kwa wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Jamii forum ni freezone andikeni mnachotaka bila woga. Jibu unavyojisikia bila kujali staha na nyazifa ata kama ni waziri mkuu faili lake likidukuliwa wekeni humu. Hii ndio maana ya jamii forum.

Achaneni na hekaya za Mshana Jr asishawishi uoga kama kufa ata wasiojulikana wanakufaga na wengine wanafanywa chochote na wenzao wasiojulikana, ata Rais wa nchi na Mshana anaweza akauwawa zamu yake ikifika

Kuna kisa cha aliekuwa mkurugenzi wa usalama wa Burundi mwaka 2018 alivaamiwa mchana kweupe akiwa na msafara wa magari matatu na akauwawa.

Jamii forum si jukwaa la kutengeneza maadili ni jukwaa la kila aina ya watu, wazuri, wenye maadili, wabaya, wakosoaji na wenye kusifu serikali, wauza dawa za kulevya na watumiaji wa madawa. Walipa kodi na wakwepa kodi, vijana, wazee na wahuni.

Sitetei maovu wala sishauri watu kufanya mambo mema mhimu ni wachangiaji kuwa huru na wasiogope kuwasema vigogo ama wachawi na wasiojulikana
 
Mkuu mshana jr humu members wote wana ID zaidi ya mbili za matusi na za hekima. Huwezi amini ID yangu moja ya heshima nashushaga nondo madini ushauri na mawahidha ila mngejua ndo maghayo.

Usije shangaa Mohammed Said ndie kidukulilo
Ww jamaa bana. Kwa hiyo Mzee Muhamed Said anaweza kuweka mbwembwe zote zile za Kidukulilo!?
 
Jamii forums imetoa uhuru wa kutumia utambulisho bandia kwa akili ya kulinda maslahi binafsi ya mwanachama.. Lakini kupewa huo uhuru haina maana uwatweze wengine kwa vile tu hujulikani utambulisho wako halisi

Ndani ya huu mtandao kuna mwanachama wa aina mbili au tatu
1. Wanaotumia utambulisho halisi
2. Wanaotumia utambulisho bandia
3. Wanaotumia utambulisho halisi na bandia
Watu wanakutana hapa hawafahamiani lakini kutokana na mahitaji ya kimaisha na maslahi ya kila mmoja ama ya upande mmoja watu hufikia hatua ya kufahamiana zaidi nje ya huu mtandao

Kuna wajinga wachache wenye uono kimo cha mbilikimo wanaodhani kwa kutumia utambulisho bandia basi wanaweza kufanya lolote na wasijulikane popote bila kujua ya kwamba maandishi hayafitiki.. Ni kupitia maandishi yako ya jana ama hitaji lako la mbeleni unaweza kujifunua na kubaki uchi kabisa

Heshima sana maandiko ya wengine hasa wale ambao inaishia kuwaona jukwaani lakini hamjawahi hata kuonana.. Hata kama maandiko yake hukubaliani nayo kosoa kwa adabu kosoa kwa heshima..Kosoa kwa hoja jadilifu na si vioja, kashfa, dharau au kejeli!

Heshima muda wake aliotumia kuandika hiyo mada, kifurushi chake, ujumbe na maudhui yake..! Si lazima ukubaliane naye.. Hivyo mpinge kwa hoja zenye mantiki ama mpotezee.. Sometimes kuna kipengele cha kukubaliana kutokubaliana na kinyume chake!

Ukiona mada imeruhusiwa kuwa hewani na kupata wachangiaji... Iheshimu sana kwa maana ina kibali cha kanuni na sheria za jukwaa! Kwa maana ya kwamba imekidhi vigezo vyote vya kuruhusiwa kuwepo hai.. Watu wanaweka mada na hazichukui round zinaliwa kichwa na kutupwa jalalani..

Mada inayoachwa hewani iheshimu sana kulingana na jukwaa lake husika..kitendo cha kuiita ya kipuuzi ama ya kipumbavu si kwamba umemtusi na kumkejeli mtoa mada tu, bali hata wachangiaji wengine na hata walioiruhusu iwepo hewani

Unapokuwa mwanachama mgeni (sio multiple ID) Unakuwa mkweli sana.. Unaongea maisha yako unajitambulisha uhalisia wako na kuomba ushauri hapa na pale. Unapokuwa mzoefu unaanza kuvimba kichwa na kujisahau wewe ni nani uko wapi na unafanya nini.. Unasahau hata background yako na kudhani hujulikani..

Usiwe ndezi kiasi Hicho una background that can be traced to the maximum... Maandishi yako mwenyewe ya awali yanaweza kuwaongoza watu mpaka ulipo na wakakufikia bila shida na wakakufanya chochote watakacho hasa kama hawana hofu na Mungu aliye hai

Kikubwa unapotumia utambulisho bandia usidhani ndio umeyawezea maisha.. Kumbuka bado unaishi na shida hazikomi.. Lakini pia kumbuka una background ambayo kwa namna iwayo yote huwezi kuifuta na watu wanayo mkononi..

Ni hayo tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi kaka mkubwa, ni muhimu kujisahihisha asante sana
 
Kaka kwema lakini.
Karibu CCM tujenge nchi.
 
nimestuka sana nakushangaa kumbe huyu jamaa nistaa sana jf ee?hataki kupingwa naukimpinga anakutafuta
Mpaka uvunguni aisee.

Binadamu tunatofautiana sana.

Wengine mtu hata akikutukana unayaacha hapa hapa maana haikupunguzii chochote in real life.

Huku katika dunia halisi maisha yanaendelea kama kawaida.

Unatukana nikizima simu inaishia hapo.

Mimi huku naendelea na mishe kama kawaida.
 
Kaka kwema lakini.
Karibu CCM tujenge nchi.
[emoji3][emoji3][emoji3] asante sana[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Umenikumbusha kipindi Hicho cha itikadi za chama tulikuwa tunaimba
Chama chetu cha mapinduzi chajenga nchiii....!
Siku hizi hizo nyimbo hazipo tena
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom