Changia fursa

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,582
Kama sikosei mwanzoni mwa January mwaka huu nilitoa tangazo hapa kuhusu mafunzo ya maarifa ya kazi ... sijaona mtu ametuma e-mail kwa ajili ya application.
Sasa naweka mambo wazi hapa. ...
Mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuotesha chakula cha mifugo aina zote kwa siku nne - nane tu.
Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeondoa changamoto zifuatazo:
1 Ufugaji utakuwa na tija kubwa sana.
2 Migogoro kati ya wafugaji na wakulima itaisha kabisa
3. Mazao ya mifugo yatakuwa bora kwa sababu mifugo itakuwa ikitumia chakula bora .
... na mengineyo mengi.
Wewe unayesoma hii habari, nakusihi uwajulishe na wengine ili tuweze kupiga hatua kwenye sekta ya kilimo na ufugaji.
Mahitaji ili ufanye kazi hiyo ni kama ifuatavyo: -
1. Uwe na elimu ya kuanzia Std 7 na kuendelea.
2. Uwe unafundishika
3. Uwe na mtaji usiopungua 200,000/= (Hii ni kwa ajili ya kununulia vitendea kazi vya msingi)
4. Uwe tayari kununua kitini kwa ajili ya maelekezo. Tshs. 15,000/=
Maelekezo mengine utayapata pale ukishajiunga na wazalishaji wa H-Fodder
J & B Enterprises tumeumia sana kusikia mifugo inakufa kwa sababu ya kukosa chakula.
Wasiliana nasi kwa e-mail: jnb14enterprises@gmail.com, simu 0655-533543.
Kwa walioko Mwanza karibu shamba darasa lililoko Igoma (nyuma ya St Mary's School)

TUIPENDE MIFUGO ITUPATIE CHAKULA BORA.
 
Hivi we mkwepa kodi ulifurahi watu walipopoteza mifugo yao kwa sababu ya kukosa chakula cha mifugo?
Mkuu samahani kidogo naomba kuuliza hivi malighafi zake kama shairi zinapatikana huko mwanza?na hydroponic nutrient inapatikana kwa shilingi ngapi?
 
Mkuu samahani kidogo naomba kuuliza hivi malighafi zake kama shairi zinapatikana huko mwanza?na hydroponic nutrient inapatikana kwa shilingi ngapi?
Mbegu kama ngano, mahindi, ulezi, mtama n.k zaweza kutumika.
Nutrients zipo za kutosha na zinatumika kidogo sana
Hapa kinachotakiwa ni kujifunza namna ya kuzifanya ziote ndani ya muda tajwa.

Hivi hamjawahi kujiuliza mbona mfugo ya wenzetu (majirani) ambao kwao mvua ni tatizo huwa haifi? Nenda hata Sudan!
 
Kwa watu walioko mbali na mwanza kama vile Mbeya na wanahitaji mnawasaidiaje
Kwa kuwa wengi wa watanzania wanajua kusoma, mafunzo hayo yako katika lugha ya Kiswahili na yanaeleweka vizuri sana. Tutafanya yafuatayo:-
1. Tutawatumia vitini vya kujisomea
2. Tutakusanya maswali toka sehemu mbalimbali na baadaye tutapanga semina sehemu tofauti kwa ajili kutoa majibu yatakayokuwa yamejitokeza kwa washiriki wetu.
Ila kwa uzoefu, maelekezo ni rahisi sana kwa sababu kila changamoto katika shughuli hii imeishafanyiwa utafiti na kutafutiwa ufumbuzi.
 
Sawa sawa
 
upload_2017-3-22_18-46-13.jpeg

Saidia kutokomeza migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
 
Back
Top Bottom