Changamoto za ukubwa

Dinazarde

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
36,868
2,000
Nilivyokua mdogo kuna vitu nilikua sivijui na naona kawaida wala sijali najali kucheza na kula na vingine vya kitoto
Sasa nimekua nimekutana na changamoto nyingi mpaka sasa hapa nilipo nashukuru nimekua na moyo mgumu,moyo wangu unavumilia mengi kusemwa vibaya,kukosolewa hata kama umefanya vyema,ukijitetea unaonekana umejawa na kiburi.
Walivyosema kua uyaone kumbe sio kuyaona maghorofa au magari ,
Kwa niliyopitia moyo wangu umekuwa jiwe la fatuma hautikisiki abadan hata nisikie nini kutoka kwa wanadamu najua nao sio watimilifu kama mim,namshukuru aunt yangu na mama angu hua hawanikatishi tamaa kabisa kama wengine nawapenda hawa wanawake sijui ntawalipa nini!!
naamini nimekua naweza haswa kua mke wa mtu "japo naiogopa ndoa "nishazoea kua huru aisee"
Nimejifunza kutomdharau mtu yeyote awe mdogo au mkubwa ,yeyote yule namuheshimu (wanasema dharau maiti hawez kuamka,usimdharau anaepumua,dunia duara inazunguka)
Najitahidi kujifunza kuwa kimya hata nisikie neno la kuniumiza vibaya na kusamehe halaf nakaa kimya naacha yapite,naamini kila kitu kina muda wake ,wanaokusema vibaya ndio hao hao unaokula nao na kucheka nao lakin moyo haujali ,na siku zote kikulacho kinguoni mwako
Namshukuru Mola kwa kila jambo naamin changamoto ni nyingii lakin usikate tamaa,nimejifunza kutokata tamaa maishani mwangu ,nimejifunza pia kufanya kitu kuuridhisha moyo wangu na sio kuridhisha mwingine
Nimejifunza kujipa raha sisubiri kupewa raha na mwingine maana maisha mafupi haya watu wanakufa kila siku,
Napenda kusikiliza muziki wowote unipao raha na kucheza kama nikiweza pia naburudisha mwili wangu,yale magumu sitaki yaniumize kichwa maana naamini yatapita ,
Marafiki ni muhimu kubadilishana mawazo,kuna marafiki pia nimekutana nao nawapenda ,kuna mwingine aliniletea zawadi nzuri amekua rafiki yangu sana japo yupo mbali lakin urafiki wetu unaendelea ,ni wengi mno marafiki wazuri ,naamin undugu si kufanana bali ni kufaana
Wenu Dinazarde
 

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,793
2,000
Ninaona moyo wako unaweza kuwa mgumu kama jiwe na pia mlaini kama Sufi. Kotekote unafanya kazi inategemea tu mtu anakujaje?

Afu kama sijaelewa pia vizuri hii ni new resolution yako au just confession of who you are? Just curious best.

But can I be your friend hun? I wanna live care free too!
 

Dinazarde

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
36,868
2,000
Ninaona moyo wako unaweza kuwa mgumu kama jiwe na pia mlaini kama Sufi. Kotekote unafanya kazi inategemea tu mtu anakujaje?

Afu kama sijaelewa pia vizuri hii ni new resolution yako au just confession of who you are? Just curious best.

But can I be your friend hun? I wanna live care free too!
Yap mlain kama sufi,
Unaweza kuwa rafiki wala haina shida
 

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,628
2,000
Ukubwa una mambo mengi sana yani kuna wakat mambo unapitia unaona kbs kweli umekua

Cha muhimu ni kukabiliana na maisha na kuishi na watu vzr.


Haikupunguzii kitu kuwa na roho nzuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom