PreGE2025 Changamoto za "No Reforms No Elections"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sawa tunasubiri hiyo Oktoba muingie barabarani mulianzishe
 
4R hizo ni zenu nyie matapeli. Hiki si kizazi cha hizo porojo boss.
Maridhiano ni two way traffic au give and take. Hakuna "winner takes all".

Tuliona kesi za wana CDM zikifutwa kwenye Mahakama mbalilmbali, tuliona waliokuwa ukimbizini Canada na Belgium wakirudi nchini, tuliona mikutano ya kisiasa ikirudi na ruzuku mkipewa.

Sasa unaposema maridhiano ni utapeli una maana gani?. Yaani bado tupo enzi za DIKTETA wa Chato?

Tuwe wakweli, mara nyingine CDM mnadhani muna UMUHIMU kuliko Watanzania wengine
 
2. Kwa vile Rais wa sasa hataweza kugombea tena, atakuwa tayari zaidi kukubali mabadiliko kwa ajili ya uchaguzi wa 2030
Yan sisi tunataka tumuondoe Rais uchaguzi ujao ww unafikiria ashikilie nchi had 2030...labda kwa kuiba kura kama walivozoea...No reforms No elections
 
Nijibu kwanza, hivi mnamuona Lissu ana akili sawa ya kuongoza watu?
Hoja ni mifumo ya uchaguzi na sio lisu kwani lisu akifa ndio kutakuwa hakuna haja ya kubadili mifumo?

Ungeacha uchawa ili tubalance hoja
 
Inashangaza sana eti kukuwa na mabadiliko kutakuwa hakuna amani hii nchi Ina mambo ya kijinga sana sasa babadiliko ya katiba yanaletaje vita
Ndo maana nchi hii Ina watu wajinga sana kwasababu ya woga...woga unatufanya wavivu wa kufikiria, mtu mwoga hajawahi kuwa na manufaa yoyote kwa jamii na Dunia kwa ujumla...kama taifa hatuwezi kujenga taifa strong kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia....watanzania inabidi tuache uoga...na tukubali mabadiliko....otherwise we shall never reach the promised land...tukiendelea na desturi hii ya woga...
 
Watanzania sio waoga ila watawala ndio waoga kwanini kuruhusu mabadiliko ya katiba kuwe sababu ya vita? Wewe linakuingia akilini hili?
 
Sawa tunasubiri hiyo Oktoba muingie barabarani mulianzishe
Tutaomba ww ukae mbele kutuzuia. Vyombo vya dola vikae pembeni maana kwa sasa hatuna silaha.
 
Hapana kumbe kuna vitu bado hujavielewa.

Ni kwamba kunyimwa nafasi ya kurudisha fomu sio kikwazo pekee.

Utaratibu uliopo ni kuwa hata ukifanikiwa kurudisha fomu bado haikupi guarantee wewe ya kujihakikishia kuwa utashiriki kugombea.

Ni kwasababu ni mpaka huyo mkurugenzi aziwasilishe hizo fomu zenye majina yako kwenye vituo husika vya kupigia kura.

Kwa hiyo ishawahi kutokea watu wamerudisha fomu lakini walipoenda siku ya uchaguzi, msimamizi akasema siwatambui kwasababu hampo kwenye orodha. Kwa maana mkurugenzi hakuwasilisha majina yao.

Kuhusu kuenguliwa.

Hili kwanza linaanzia kwako wewe unaye hoji. Je binafsi yako una amini kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani kuna tokana na wao kufanya makosa wakati wa kujaza fomu?

Je una amini kuwa ni CCM pekee kwa 100% ndio wenye huo uwezo wa kujaza fomu kiusahihi? (Kwasababu hakuna mgombea yeyote wa CCM aliyewahi kuenguliwa kwa kukosea kujaza fomu)

Ikiwa kama una amini hayo mambo mawili hapo juu kuwa ndio sababu, basi hizo suluhu ulizodai wazifuate zinaweza kuwa na tija.

Lakini kama kuenguliwa kunakuja kutokana na mpango maalumu wa kisiasa kuhakikisha upinzani wanakosa nafasi za kugombea basi hiyo haiwezi kuwa suluhisho.

Kuhusu mawakala kuwepo kwenye vituo na kuhakikisha kura zinapigwa kwa uwazi na kuzuia kura feki

Nadhani kabla ya yote kwenye hili swali tujiulize ni nani mwenye uwezo wa kumzuia polisi mwenye silaha ambaye amebeba kura feki?

Nani mwenye huo uthubutu?

Kwasababu tumekuwa tukiona vyombo vya dola ndio vikiwa vimepewa hilo jukumu la kusambaza kura feki.

Sasa ukizingatia kauli yako ya awali ya kulinda Demokrasia unawezaje kulinda kura katika mazingira kama hayo at the same time uwe umelinda na Demokrasia?
 
Hizo zilikuwa ni haki zao hao cdm wala sio hisani. Ama kwakuwa walipata hivyo unavyosema, basi si haki kupatikana uchaguzi wa haki?
 
Haya uliyoandika hapa ndio yasiyotakiwa na ccm. Na hapa ndio ulipo msingi wa madai yao ya halali.
 
Yan sisi tunataka tumuondoe Rais uchaguzi ujao ww unafikiria ashikilie nchi had 2030...labda kwa kuiba kura kama walivozoea...No reforms No elections
Mnataka kumuongezea muda hadi 2028 halafu ndio uchaguzi ufanyike. Mnataka kumpa miaka mitatu ya bure. Akishinda atakuwa amedumu kwa miaka 13 unless mshindi wa uchaguzi huo atawale kwa miaka miwili tu ambapo kama atashinda mwengine atakuwa amepinjwa.
Mimi ninachosema ni kuwa kwa sababu kwa vyovyote vile Rais wa sasa atashinda uchaguzi ujao ( uwe 2025 au 2028) ni bora amalize muda wake 2030 kuliko 2033.

Amandla...
 
Katika uchaguzi wa 2020 kuna wagombea waliozuiwa kurudishwa fomu. Boni Jacob aliambiwa amefukuzwa uanachama wa Chadema hivyo amepoteza sifa. Kuna wengine waliambiwa mgombea wa Chadema ameisha chukua fomu kwa hiyo hawezi kupewa fomu nyingine. Kuna waliokuta ofisi za Msimamizi zimefungwa au Msimamizi hayupo ofisini hivyo walishindwa kuziwasilisha kabla ya deadline. Mkurugenzi alijitokeza baada ya deadline na kutangaza kuwa mgombea pekee aliyewasilisha ndani ya muda ni wa CCM. Utagombea vipi kama hata fomu haujawasilisha?

Amandla...
 
Haya uliyoandika hapa ndio yasiyotakiwa na ccm. Na hapa ndio ulipo msingi wa madai yao ya halali.
Ndio maana nasema kuwa uchaguzi hata uwe 2028 hautakuwa tofauti na zilizopita. Ni kujidanganya tu kufikiria vinginevyo.

Amandla...
 
Unajua tusifike mbali tukaji pofosha kupitia bias zetu kujifanya hatujui kabisa kinachoendelea kwenye kipindi cha uchaguzi.

Tusifike hatua ya kuona kama kulikuwa na possible alternative kwenye hizo scenario ambayo ingezuia hayo yasifanyike na kudhani kama kuna sehemu wapinzani walizembea

Kwanza tuanze na wewe mwenyewe

Sababu hizo ulizozitaja kwako unaziona zina mashiko?

Kwamba wapinzani wote nchini ni wazembe kiasi hicho?

Na kwamba CCM pekee ndio watu makini sana ambao hawakosei?

Tuanzie hapo kwanza
 
Pumba
 
Wapi nimesema kuwa CCM hawakosei? Inaelekea haujasoma au haujaelewa nilicho andika.

Amandla...
 

View: https://www.instagram.com/p/DIBMHZmgmUV/?igsh=OTByM3UzbDQ4aDFz
 
Ndio maana nasema kuwa uchaguzi hata uwe 2028 hautakuwa tofauti na zilizopita. Ni kujidanganya tu kufikiria vinginevyo.

Amandla...
Bila machafuko hakuna uwezekano wa kuwa na uchaguzi wa haki.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…