Kuna kisa kimoja cha dogo mtaani, yy alioa mapema sana akiwa mdogo around 20yrs, 2015, alifanikiwa kupanga chumba na sebule kikiwa full yaani kila kitu.
Alimfumania mke wake mara mbili chumbani kwenye kitanda wanacho lala na mkewe, mara kwanza jamaa akamsamehe mkewe baada ya wazee kumsihi, mara ya pili ktk kitanda kilekile na jamaa yule yule akamfumania mkewe, jamaa akamwambia achagu chochote anachokitaka aondoke nacho. Demu akaamua kumkomoa kwa kuchukua kila kitu, yaani hakuuacha kitu.
Yule dogo akaanzia 0,akaenda kwa mjomba wake akamuomba mkeka,jamaa kalalia mkeka, baada ya mwezi akavuta kitanda na mpaka sasa kishanunua kila kitu na mwaka jana kaoa mke mwengine. Maisha yana endelea, yule binti baada ya mwaka mmoja akawa mtu wa starehe, mpaka kufikia hatua ya kujiuza maeneo ya Ubungo Riverside, sasa hivi ana mimba na mwenye mimba hajulikani basi yupo yupo tu.