julius caesar
Member
- Mar 20, 2015
- 94
- 27
kwani mnaishi mtwara na kigoma kiasi kwamba ni shida hata wikiend moja kufika anakoishi mwenzio.??
kuna watu wanalalamikaga humu kuwa wadada wa humu wanaanzaga na kuvuna pesa badala ya kujenga trust kwanza.
hii ni changamoto ambayo dada zetu inabidi waifanyie kazi. sio kila mtu ni mpita njia kwamba maji utamuuzia. wengine ni wakaaji
Bila kuonana kwanza kuhudumia mtu roho inakaaa kabisa. Fanya mipango muonane kwanza, mzungumze, alafu vingine vitafuata.
Asante kwa ushauri mkuu!
Usitume hela
Usimtumie hela bali tafuta muda unakaonane naye kwanza ana kwa ana, usikute hata picha alizokutumia si zake.
Halafu kama nia yako ni uchumba kweli kweli, stuka kwa anayeomba omba hela ilhali hata hamjafahamiana vizuri, utalia baadae. Kwa taarifa yako wanawake wako wengi mno, lakini wa kuoa ni wa kumulika na tochi, si kila mwanamke ni wife material
Tuma pesa bwana acha ubahiri huko!!! Teh teh teh
Naye si yupo humu? Subiri naye atakuja kukushauri kama umtumie au laah!
Usimtumie hela bali tafuta muda unakaonane naye kwanza ana kwa ana, usikute hata picha alizokutumia si zake.
Halafu kama nia yako ni uchumba kweli kweli, stuka kwa anayeomba omba hela ilhali hata hamjafahamiana vizuri, utalia baadae. Kwa taarifa yako wanawake wako wengi mno, lakini wa kuoa ni wa kumulika na tochi, si kila mwanamke ni wife material
Boss, sidhani kama kuna Mwanamke/Manzi yeyote humu ambaye utatangaza unatafuta mchumba/mke, ajitokeze na awe normal. Lazima ana flaws za kutosha ndio maana kashindwa kupata mtu in the real world. Vizuri havipatikani kirahisi kamwe. So wanaojitokeza kutangaza hizo nafasi, inabidi wawe wamejiandaa kisaikolojia.
Sista unaonaje na mimi niweke bandiko la kutafuta mke wa pili