Changamoto za kodi kwa wafanyabiashara

Micky driver

Member
Oct 3, 2018
8
15
Habari wana jf

Nimekuwa tax consultant kwa miaka miwili sasa katika changamoto nimekutana nazo sugu nipamoja ya tra kwa wafanya biashara watu wengi wamekuwa wakisajili makampuni na kuyatelekeza bila kujua madhara yake ninini? Ambayo imepeleke badae kuwa na madeni makubwa sana leo nataka tujadili maswala ambayo yanapelekea kampuni kuwa na madeni makubwa ambayo sometimes huna hata uwezo wa kuyalipa nitataja baadhi ya mambo ambayo usipo fanya itakupelekea kampuni yako kupigwa penalty

1. Kutofanya makadilio kwa wakati
Sheria inakutaka kila mwaka kufanya makadirio ya mapato ya biashara yako ambapo mwisho wake ni 31march na usipo fanya tra inaanza kuhesabu penalt ya 225,000 kila mwezi mpaka siku utakapo fanya makadirio yako

2. Kutopeleka paye na sdl kwa wakati ambayo hii mwisho wake ni kila mwezi tarehe 7 na usipo peleka kila mwezi inakuwa ina hesabu penalty ya 225,000 kwa mwezi kwaiyo kwa paye na sdl ni 450,000 penalty kila mwezi itahesabu kila mwezi mpaka pale utakapo peleka hio returns

3. Nyingine ni returns of income ambayo hii ni hesabu za kila mwaka pia inabidi upeleke mwisho mwezi wa 7 kila mwaka na usipo peleka faini yake ni hio hio 225,000 kwa mwezi mpaka siku unapeleka hio return
Hayo ndio mambo muhimu sana ya kufwata unapo kuwa na kampuni karibu kwa mwenye nyongeza
 
Kwanza mkuu mm binafsi nashukuru sana kwa somo hili kwa wafanya biashara wa nchi hii...
Ila nina ombi moja, kama muda wako unaruhusu ningependa kila siku uwe unatupa elimu zaidi kuhusu masuala ya kodi as a CONSULTANT ili watu wote tuwe na angalau uelewa kidogo juu ya maswala haya.

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Kwanza mkuu mm binafsi nashukuru sana kwa somo hili kwa wafanya biashara wa nchi hii...
Ila nina ombi moja, kama muda wako unaruhusu ningependa kila siku uwe unatupa elimu zaidi kuhusu masuala ya kodi as a CONSULTANT ili watu wote tuwe na angalau uelewa kidogo juu ya maswala haya.

NATANGULIZA SHUKRANI
hakuna shaka mkuu tuko pamoja sana nitajitahidi kutenga muda kwa jili ya hili
 
Back
Top Bottom