A
Anonymous
Guest
Mimi kama mtumishi wa umma katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora, nalazimika kuripoti kero inayotusumbua baadhi ya walimu tulioshiriki zoezi la usajili wa wanafunzi mwezi Novemba 2025.
Baada ya usajili, tulianza kufundisha kwa wiki kadhaa, tukibeba jukumu la kuhakikisha wanafunzi wapya wanapata mafunzo stahiki. Tulijaza fomu za honorarium kama tulivyoelekezwa, tukiamini tutalipwa posho zetu.
Hata hivyo, hadi sasa hatujalipwa posho za kufundisha za mwezi Novemba 2025. Wahusika ndani ya kampasi wanadai hatustahili malipo kwa sababu tulisajili, jambo ambalo halina mantiki kwani tulifundisha kwa muda mrefu ukiacha wiki moja ya usajili.
Tunasisitiza kwamba kazi ya kufundisha tuliyoifanya inastahili kulipwa. Hatukupewa taarifa yoyote ya kutuondoa kwenye malipo, na tulifuata taratibu zote ikiwemo kujaza fomu za honorarium.
Tunawaomba NACTIVET na wadau husika waingilie kati ili haki itendeke. Ni muhimu mtumishi wa umma anapofanya kazi kwa uaminifu na kujitolea, stahiki zake zikatimizwa bila visingizio.
Kero hii si ya mtu mmoja bali ni ya walimu kadhaa. Tunahitaji uwazi, uwajibikaji na heshima kwa kazi tunayofanya.
Mwisho:
Tunatoa wito kwa viongozi na wahusika kuhakikisha malipo haya yanashughulikiwa haraka. Haki ya mtumishi ni msingi wa ufanisi wa taasisi.