Changamoto kubwa kwa UKAWA wakiingia madarakani itakuwa ni kumpata CDF na IGP

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hivi katika majeshi yetu haya ya leo,kuna watu wa kuaminika kutumika kama CDF na IGP katika serikali itayoongozwa na UKAWA endapo mgombea kutoka vyama vinavyounda UKAWA atafanikiwa kuwa raisi wa nchi hii?

Kwa maneno mengine,vigogo katika majeshi yetu haya ya leo wanaonyesha utayari wowote kuwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu kutoka upinzani?

Hili jambo ukilitizama kwa mapana na marefu,utagungua si jambo la kulipuuza hata kidogo.
 
Waoga hufa mara nyingi kabla ya vifo vyao vya kweli, lakini jasiri hufa mara moja tu, kwa akili fupi kama yako hili jambo si la kupuuza
 
Point yako ni nzuri na nyeti. Kwa nafasi kama hizo, lazima uzifanye kwa namna ya kugonga na kusikiliza ni mwangwi. Hapa nina maana kwamba, kwa yeyote ambaye atakalia kati ya hivyo viti, lazima awe mwajibikaji kwa kazi watakazopangiwa kuzifanya mara tu serikali mpya inapoanza kazi. Wakati huo huo ndio unatayarisha cream mpya. Kwa vyovyote vile jamaa wa sasa hawataweza kukamilisha baadhi ya assignment watakopewa kutokana na udhaifu na ushikaji miongoni mwa mafisadi. Hiyo itakuwa sababu tosha ya kuwafuta kazi na kuwageuka hapohapo kwa deals za kifisadi walizoshiriki huko nyuma. Itachukua muda. Huwezi kubadilisha system nzima mara moja. Eventually itabidi kwani iliyopo sasa 97% imeoza from top to bottom.
 
Hofu yangu kubwa ni kuweza hata kuihujumu hiyo serikali mpya maana CCM iko mpaka kwenye majeshi yetu.
 
CDF sio tatizo kwa vile uzalenda bado upo vya kutosha JWTZ na JKT. Ila kwa nafasi ya IGP hakuna kitu bora kuajiri mzungu wakati wa kipindi cha mpito kuliko hawa polisisiemu waliopo
 
ujinga ni mzigo. cdf, igp watspatikana huko huko jeshini waliko. wale ni watumishi wa umma, wa vyma vyote.
 
CDF sio tatizo kwa vile uzalenda bado upo vya kutosha JWTZ na JKT. Ila kwa nafasi ya IGP hakuna kitu bora kuajiri mzungu wakati wa kipindi cha mpito kuliko hawa polisisiemu waliopo

Umesahau matamko ya kina Shimbo ingawa hivi sasa ni mstaafu?
 
Mambo yatakuwa vilevile tu, hizo ni ajira, na mwajiriwa umtii boss wake tu, utiifu wao utabadili upepo tu. Haitaleta matatizo yoyote, imeenda vizuri tu nchi nyingine.
 
mawazo finyu,sawa na kipindi kile Nyerere anang'atuka watu walikuwa wanajiuliza hivi ni nani anaweza kuwa rais?,Ko ndg tupo wengi tu tunaoweza kuwa IGP au CDF.
 
Hivi katika majeshi yetu haya ya leo,kuna watu wa kuaminika kutumika kama CDF na IGP katika serikali itayoongozwa na UKAWA endapo mgombea kutoka vyama vinavyounda UKAWA atafanikiwa kuwa raisi wa nchi hii?

Kwa maneno mengine,vigogo katika majeshi yetu haya ya leo wanaonyesha utayari wowote kuwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu kutoka upinzani?

Hili jambo ukilitizama kwa mapana na marefu,utagungua si jambo la kulipuuza hata kidogo.
Mkuu vijana wenye elimu na utaalum wa kutosha ila tulioshindwa kuprosper kutokana na mfumo wa kujuana na kulindana mbona tupo wengi sana huku-hilo wala si tatizo
 
Hivi katika majeshi yetu haya ya leo,kuna watu wa kuaminika kutumika kama CDF na IGP katika serikali itayoongozwa na UKAWA endapo mgombea kutoka vyama vinavyounda UKAWA atafanikiwa kuwa raisi wa nchi hii?

Kwa maneno mengine,vigogo katika majeshi yetu haya ya leo wanaonyesha utayari wowote kuwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu kutoka upinzani?

Hili jambo ukilitizama kwa mapana na marefu,utagungua si jambo la kulipuuza hata kidogo.
Kwa taarifa yako nchi hii kila idara kuna wana UKAWA ingawa hawapendi kujionyesha, we subiri wakati ufike utashangaa na roho yako.
 
mawazo finyu,sawa na kipindi kile Nyerere anang'atuka watu walikuwa wanajiuliza hivi ni nani anaweza kuwa rais?,Ko ndg tupo wengi tu tunaoweza kuwa IGP au CDF.
Unaweza kuona ni wazo finyu ila ujue majeshi yetu yametawaliwa na makada wa chama na hiki kina mizizi mirefu huko kuliko unavyofikiri.

Kumbuka kuna makashifa yanahusu hawa jamma na upinzani umekuwa ukituhumu hizi taasisi hivyo usilichukulie kirahisi tu hili jambo.

Labda nikuulize tu;tuhuma za meremeta zinahusu watu gani?Leo hii kwenye hiyo sytem baadhi yao hawapo?
 
Rais hateui CDF kama inavyofanyika kwa polisi au magereza. Jeshi lina utaratibu kama majeshi mengine duniani so raisi anathibitisha uteuzi tu kisheria lakini kuna tume ya kijeshi ndani ya jeshi lenyewe.
 
Kwa taarifa yako nchi hii kila idara kuna wana UKAWA ingawa hawapendi kujionyesha, we subiri wakati ufike utashangaa na roho yako.
Wazo lako nalikubali ila nashauri viongozi wa UKAWA wajenge mahusiano mazuri na majeshi yetu ili iwe rahisi kupata watu wa kuwapa nafasi za juu katika majeshi yetu na wakawa waaminifu kwao.
 
Hivi katika majeshi yetu haya ya leo,kuna watu wa kuaminika kutumika kama CDF na IGP katika serikali itayoongozwa na UKAWA endapo mgombea kutoka vyama vinavyounda UKAWA atafanikiwa kuwa raisi wa nchi hii?

Kwa maneno mengine,vigogo katika majeshi yetu haya ya leo wanaonyesha utayari wowote kuwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu kutoka upinzani?

Hili jambo ukilitizama kwa mapana na marefu,utagungua si jambo la kulipuuza hata kidogo.

Kwa upande wangu nafikiri hili litawezekana sana maana si wote walioko kule wanaofurahia utawala wa ccm. Huku kwa mapolisi hiyo kazi wanampa G.Lema ndo utaona watakavyojiengua wenyewe. Halafu CDF kule huwa hakuna mjadala. Huyo Shimbo niliwahi kudokezwa kwamba ndo alimsaidia mkulu kutoroka kule Monduli baada ya kuwa amelikoroga dhidi ya mkuu wa kikosi. Hivyo hayo mambo yote kulikuwa na kulipana fadhila na Shimbo alilijua hilo ndo maana hakuwa na woga wala nini maana aliambiwa apige tu!!!
 
Huu ndio upuzi mwingine niuona kati ya viongozi wa upinzani, kushindwa kutofautisha vyombo vya dola na chama tawala. Hawa walio katika vyombo vya dola wanafanya kazi chini ya kiapo cha utii hilo tu.

Siku wapinzani watakapo jua siri hii ya utofauti kati ya vyombo vya dola na ccm, basi kuiondoa ccm madarakani itakuwa kama kumsukuma mlevi.
 
CDF sio tatizo kwa vile uzalenda bado upo vya kutosha JWTZ na JKT. Ila kwa nafasi ya IGP hakuna kitu bora kuajiri mzungu wakati wa kipindi cha mpito kuliko hawa polisisiemu waliopo
Ha ha ha ha Nora kuajiri mzungu...... Hii kali.....Ila kiukweli kwa waliopo ndani ya jeshi la polisi kwa Sasa wapo Ila itabidi kuchukua wale wa ngazi za Chini ambao migao ya kifisadi haikuwakuta na kuwalemaza akili.
 
Wataingia lini? Nyie mna ndoto za bangi? Mnaijua CCM nyie? Subirini najua jibu lenu kwa mliowapa matumaini mtakimbilia mahakamani ili mjikoshe! halafu siku mbili tatu mnamkubali Rais wa CCM kiulainii( kama Slaa alimkataa JK 2010 akamkubali 2012) muda kidogo hasira zinaisha mnaanza tena kampeni za mwaka 2020. Wait
 
Huu ndio upuzi mwingine niuona kati ya viongozi wa upinzani, kushindwa kutofautisha vyombo vya dola na chama tawala. Hawa walio katika vyombo vya dola wanafanya kazi chini ya kiapo cha utii hilo tu.

Siku wapinzani watakapo jua siri hii ya utofauti kati ya vyombo vya dola na ccm, basi kuiondoa ccm madarakani itakuwa kama kumsukuma mlevi.
Kiapo kinapochanganyika na ukada huzaa kitu tofauti kabisaa.

Watu wa mataifa wengine huweza kubadilisha vyama vilivyokaa madarakani kwa muda mrefu bila kuathiri system ya majeshi yao lakini hapa kwetu ni mashaka sana.
 
Back
Top Bottom