Changamoto katika maendeleo ya uchumi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto katika maendeleo ya uchumi wetu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rwey, May 29, 2012.

 1. R

  Rwey Senior Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Uchumi wetu kama nchi inayoendelea unatakiwa kuimarika kupitia uzalishaji na kuongeza thamani ya malighafi tulizo nazo. Ili kufanya hayo inahitajika uendelezaji wa viwanda. Uendelezaji wa viwanda unatakiwa kwenda sambamba na upanuzi wa teknolojia kutokana na hali ya uchumi wa dunia ulivyo kwa sasa. Ili kuhuhisha upanuzi wa viwanda kwenda sambamba na teknolojia, jambo la msingi ni MTAJI... That is where the challenge comes in our country. ....Chukua hatua....
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu Uchumi wetu utakua kwa kuanzisha Viwanda na si chochote kile, China iko pale ilipo kwa sbabu ya Viwanda, Jaapani iko pale kwa sababu ya Viwanda, South Africa iko pale kwa sababu ya viwanda,

  Ila watawala wanataka kutuaminisha kwamba tunaweza endelea bila viwanda, that is why nchi imegeuka ya wachuuzi, kila mtu anataka auze Simu na Radio kutoka China na Japani, kwa huu uchuzi tunakuza uchumi wa China make bidhaa zao zinazidi kupata soko,

  Kuhusu Viwanda vyetu kutengeneza bidhaa duni, ni kweli kwenye kuanza ni lazima viwe duni, CHINA WAKATI INAANZA KUTNGENEZA BIDHAA ZAKE ILIKUWA INACHEKWA SANA NA NCHI ZA ULAYA NA MAREKANI, lakini viongozi wao walisema hawatakaa wa import kitu zaidi ya raw materio na watatumia bidhaa zao hizo hizo hata kama hazina ubora

  CHINA WAKATI WAMETOA JEIFONG kama nimekosea spelingi mtanisahihisha, hili ni lile gari lao linataka kufanana na ISUZU INJECTION, hili gari la CHINA BAADA YA KUTENGENEZWA walichekwa sana na Nchi za Ulaya kwamba lina sura mbaya, ila wao waka komaa tu, Cheki leo jamaa ni wa pili na wamewapiga fimbo wale wote walio kuwa wakiwacheka,

  Bongo tunataka kuaminishwa kwamba tunaweza kuendelea kwa kujenga Hoteli za kitalii, Magest na kazalika, hakuna Nchi hata moja hapa Duniani iliyo wahi kuendelea bila viwanda, WATALII WANAOINGIA MAREKANI KUTALII NI WENGI MNO KULIKO WANAO KUJA BONGO ila USA haijawahi hata kuhesabia utalii kama moja ya nguzo za uchimi wao,

  South Africa wanapokea watalii wengi sana kuliko sisi lakini hata siku moja uchumi wao hautegemei watalii, ni viwanda pekee ndo vinaweza kututoa na wala si MIGODO YA DHAHABU

  Ishu ya mitaji ni kweli but lazima tuanze kidogo, mfano Tanzania huwa kuna zile mashine za kukamua Alzeti kwa kutumia mkono, Ule ni mwanzo mzuri na from there ndo watu wanazidi kuwekeza zaidi

  China viwanda vyake vyote vya mwanzo vilikuwa vinatumia mikono, kakini leo hii wamepiga hatua, Tatizo tunataka tuanze tu na viwanda vikubwa kitu ambacho hakiwezekani
   
Loading...