Changamoto iwe kama sehemu tu ya kujifunza, 'how'?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
CHANGAMOTO IWE KAMA SEHEMU TU YA KUJIFUNZA, 'HOW'?

Wewe kama mwana mafanikio, ni lazima mpaka sasa uwe unajua ya kwamba hakuna kitu ambacho kinapatikana kirahisi tu. Kila kitu kina changamoto zake, na vikwazo vyake pia.Hata uwe umejiandaa vipi, bado utakutana na changamoto, hii ni njia ya maisha.

Pamoja na changamoto hizi bado unahitaji kushinda, na utaweza kushinda vizuri sana, kama utajua vizuri kuhusu changamoto hizi.Huwezi kuchagua ni changamoto gani ije kwako, changamoto itakuja, iwe ni kubwa au ndogo, ya kawaida au mbaya sana, huwezi kuchagua.

Lakini kuna kitu kimoja muhimu sana unachoweza kuchagua, kwa kukijua hiki utaweza kuvuka kila changamoto na hatimaye kufikia mafanikio.Kitu pekee unachoweza kuchagua ni unazichukuliaje changamoto unazokutana nazo.

Kuna ambao wanazichukulia kama sehemu ya kujifunza na hivyo wanajifunza na kusonga mbele.Kuna ambao wanachukulia kama ndio mwisho wa safari na hivyo wanakata tamaa kabisa.

Je, Wewe unazichukuliaje changamoto?

Unachukua hatua gani unapokutana na changamoto?

Hiki ni kitu ambacho unaweza kuchagua wewe mwenyewe, na kutokana na utakavyochagua utaweza kwenda mbele zaidi au unaweza kupotea kabisa.

Chagua kuichukulia kila changamoto kama sehemu ya kujifunza na moja ya njia za kufikia mafanikio makubwa, na utaona fursa nyingi sana za kufikia mafanikio hayo.
 
We jamaa kila siku lazma nisome thread yako
Unapenda sana kutupia thread kila leo eeh
Anyway huwa napata kitu asante
 
Hahaha...

Mkuu undugu kufaana post nyingine uwe unanitumia pm na mimi nipost walau mara moja moja
 
Back
Top Bottom