CHAN Finals - Tanzania imepangwa kundi gumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHAN Finals - Tanzania imepangwa kundi gumu

Discussion in 'Sports' started by Shakazulu, Dec 26, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2008
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  8:33 GMT, Friday, 26 December 2008
  CHAN draw completed in Ivory Coast  Hosts Ivory Coast will kick off the first ever finals of the African Nations Championship (CHAN) against Zambia in Abidjan on 22 February.

  The two sides have been drawn in Group A for the finals at a ceremony in the Ivorian capital Abidjan.

  The other two teams in the group, which will be based in Abidjan, are Senegal and Tanzania.

  Group B sees Ghana drawn alongside Zimbabwe, Libya and the DR Congo.

  The group will be based in Bouake, which is the Ivory Coast's second biggest city and was the former stronghold of the New Forces rebels.

  The CHAN is a new tournament organised by the Confederation of African Football where national teams may field only locally-based players.
   
 2. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35


  Tutakufa nao tu. Sasa hivi hakuna kuogopa makunyanzi tena.
   
 3. Baisha

  Baisha Member

  #3
  Dec 26, 2008
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Group A

  Ivory Coast
  Zambia
  Sénégal
  Tanzania

  Group B

  Ghana
  Zimbabwe
  DR Congo
  Libya

  wadua mnasemaje/.??ila mie naona tuatavuka tu hapa,maana ukiangaliwa tulizopangwa nazo wanawategemea sana wachezaji wa kilipwa!!!go tanzania
   
 4. A

  Alpha JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Damn!!!!!

  That's a tough group, but with good preparation and confidence it's possible.
   
 5. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yes we can, why not? As Damn has mentioned two things " we need Good preparation and confidence".
   
 6. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Really it is DAMN.
   
 7. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hapo kweli kazi ipo.
  Hao wote tulio pangwa nao wanamafanikio mazuri katika soka ingawa kweli wanategemea wachezaji wakulipwa lkn bado experience na majina ya hizo nchi ina-matter sana kwenye saikologia ya kimpira
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  If you look at the 8 teams in the finals, sisi ndio underdogs haswa! Lakini tunaweza, Angola alifika World Cup na kucheza visuri sana

  Cha kuomba ni hao wachezaji wetu wasilewe sifa, tunaweza, size zao, umri, motivation na talents zipo... Mimi nawawaza zaidi Libya na Tanzania kufanya kufuru hapo mwakani
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...sasa tutumie huo u-underdog wetu 'kupindua meza'
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Watanzania tuondoe shaka,timu yetu iafanya vizuri tu,cha msingi ni maandalizi ya nguvu na akili yanayoendana na aina ya mashindano wanayokwenda kushiriki..Taratibu tutafika tu
   
 11. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Kuna faida ya kuwa underdog so dont give up
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sioni kwanini tusishinde iwapo tulisimama na wale wa kulipwa kwanini tushindwe na hawa.
   
 13. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...SM, Hapa mimi nina imani kabisa Taifa Stars ikiwa na maandalizi mazuri na wachezaji wakishika mafundisho ya mwalimu, wakawa watulivu uwanjani bila ya kuogopa majina ya nchi kwa hakika tuna nafasi ya kufanya wonders. Unajua wachezaji wetu wanatakiwa waingie kwenye mashindano wakijiua kabisa na wao wanaenda kushindana na pia kutumia nafasi hiyo kutangaza majina yao ukizingatia mashindano yatakuwa yakiangaliwa na watu wengi kwa hiyo hapo ndipo pa kutokea. Kwani Senegal walikuwa na majina sana kabla ya World Cup? Lakini walichofanya ikiwemo kukilaza kigogo cha ulimwengu France karibu wachezaji wote walipata timu za kucheza ulaya na ndio hivyo tena wanaendelea kupeta.
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkulu L,
  nakubaliana na wewe 10/10,ni kweli hata hao Senegal hawakupata tu mafanikio hivi hivi waliwazamisha miamba France kwenye ile mechi yao ya kwanza.
  Lakini yote hayo ya sisi kufanya wonders yako mikononi mwa wachezaji wetu kama kweli wanataka mafanikio hayo basi ni lazima watimize wajibu wao kama wachezaji ,mimi nadhani mwalimu sio tatizo ila wachezaji.
   
 15. K

  Komavu Senior Member

  #15
  Dec 28, 2008
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wadau,
  Naamini uwezekano wa kufanya vizuri upo kabisa, kama tuliweza kukomaa na cameroon
  wakiwa na miamba wao tutashindwa vipi kwa hawa wengine, cha muhimu wachezaji wawe
  watulivu na wajue fika wanaenda kushindana na si kushiriki wauze sura tu huko.
   
 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  WACHEZAJI 23 wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameondoka leo alfajiri kwenda Abidjan, Ivory Coast tayari kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani, CHAN.


  Tanzania ni kati ya timu zinazoshiriki fainali hizo ikiwa Kundi A pamoja na wenyeji Ivory Coast, Zambia na Senegal. Tanzania itaanza kucheza Jumatatu dhidi ya Senegal. Kundi B lina timu za Congo, Zimbabwe, Libya na Ghana.


  Kikosi hicho kitakachoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Muungano, Muhammed Seif Khatibu.


  Wachezaji wa Stars waliagwa juzi usiku kwenye Hoteli ya New Africa walipoandaliwa chakula cha usiku na wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya Bia ya Serengeti na Benki ya NMB.


  Akizungumza baada ya kutaja kikosi hicho juzi wakati timu hiyo ilipokuwa ikikabidhiwa bendera ya taifa , kocha mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema mafanikio waliyoyapata wachezaji wa timu ya taifa yanasaidia kujenga kizazi kijacho cha wachezaji mpira wa miguu nchini.


  Maximo alisema ili timu hiyo iweze kufanya vizuri inahitaji ushirikiano mkubwa nje na ndani ya uwanja kwani yeye ameijenga timu kushirikiana ndani ya uwanja.


  Alisema wachezaji ambao amewachagua kwenye timu ya taifa lakini hataenda nao Ivory Coast alifanya hivyo ili kuwapa motisha na kwamba anajua atakuja kuwatumia au wanafaa kutumika katika timu ya Taifa kwa hiyo wasikate tamaa bali waendelee na mazoezi kwani mafanikio ya Stars ni mwanzo wa kukua na kujulikana soka la Tanzania kimataifa.


  Wachezaji walioachwa ni Omary Pazi, Jabir Aziz, Salvatory Ntebe na Uhuru Suleiman.


  Maximo alisema timu yake haiendi Ivory Coast kushiriki tu, bali wanakwenda kushindana na Watanzania wategemee kuona kandanda safi na yenye matokeo mazuri kwani TFF na wadhamini wanaoisaidia timu wameshirikiana vya kutosha.


  Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Joel Bendera akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi bendera alisema wachezaji wanatakiwa wajenge imani ya ushindi na kuwa timu yao ni nzuri na wanategemewa na wanawakilisha Watanzania zaidi ya milioni 36.


  Bendera alisema katika timu hiyo ya taifa kuna wachezaji wazembe ambao wanacheza mpira kwa asilimia 60 tu, wengine asilimia 90 wakati wanatakiwa wasakate kabumbu kwa asilimia 100.


  Waziri Bendera alisema wachezaji lazima wajenge ari wawe timamu kisaikolojia na morali ya hali ya juu ili kupata ushindi katika mashindano hayo ya CHAN.


  Wachezaji watakaokwenda Ivory Coast ni makipa: Farouk Ramadhan, Shaaban Dihile, na Deogratius 'Dida' Boneventure wakati mabeki ni Shadrack Nsajigwa (nahodha), Salum Sued, Nadir 'Canavaro' Haroub, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, na Amir Maftah.


  Viungo ni Henry Joseph, Godfrey Bonny, Nurdin Bakari, Shaaban Nditi, Athuman Idd, na Mwinyi Kazimoto wakati washambuliaji ni Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Kigi Makasy, Abdi Kassim, Haruna Moshi, Mussa Mgosi na Nizar Khalfan.


  Katika hatua nyingine Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars walichangishana zaidi ya kiasi cha dola za Marekani 95,000 kwa ajili ya shughuli maalum za kuisaidia timu ya Taifa.


  Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Stars, Mohamed Dewji alitoa dola za Marekani 20,000, Dosa na Tanil Somai dola 15,000, Kobil 15,000, Fayaz 15,000, Abji 10,000, NMB 10,000, SBL 10,000, Sanjai 10,000, Azim Dewji 5,000 na Kassim Dewji ambaye naye alitoa dola 5,000.


  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga alisema mbali na fedha hizo zilizochangwa, kamati hiyo imeshatumia kiasi cha milioni 250 katika kuisaidia huduma mbalimbali za timu ya taifa.


  Tenga alisema Stars imekaa kambini kwa wiki 61 tangu Machi 2006 na imecheza mechi 41 chini ya Maximo, kushinda 18, sare 13 na imepoteza 10. Alisema Stars katika kipindi hicho imetumia zaidi ya bilioni 1.6 ambazo ilizipata kutoka kwa wadhamini wake ambao ni Serengeti na NMB.


  Tenga aliongeza kuwa Taifa Stars katika kipindi cha kocha Maxio Maximo imecheza jumla ya mechi 41 imeshinda 18 imetoka sare mechi 13 na imefunga magoli 48.


  Alisisitiza kuwa matarajio ya Watanzania kwa Taifa Stars ni wachezaji na viongozi watakuwa mabalozi wazuri na wataonyesha nidhamu ndani na nje ya uwanja, pili Watanzania wanatarajia kuona mchezo mzuri na wa ushindi na tatu ni timu isiende kushiriki tu bali timu yetu ionekane ikishindana.


  Katika hafla hiyo, mdau mmoja wa soka aitwaye, Murtazar Mangungu aliahidi kuwa kila atakayefunga goli kwenye michuano ya CHAN atampa dola 50
  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 17. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Hapo ni kundi la kifo; ukiondoa wenyeji waliobaki wote tuna nafasi ya kusonga mbele. Hiii ni michuano ya Wachezaji wa ligi za ndani kwa hiyo viwango vyetu viko sawa. Ukiondoa wenyeji Ivory Coast nchi zilizobaki hakuna nchi yenye klabu za kutisha katika ligi ya mabingwa ya CAF- Senegal hawana klabu iliyowahi hata kufika nusu fainali, Zambia nao hakuna timu iliyowahi hata kufika fainali (ingawa Nkana Red Devils na Nchanga Rangers zimewahi kufika mbali). Simba imeshawahi kufika fainali ya Shirikisho, na Simaba na Yanga zimewahi kufika hatua ya makundi.

  Kwa hiyo sote tuko sawasawa ukiondoa Ivroy cost ambao wana vilabu vikubwa kama vile Stella Artouis, African Sports, na ASEC Mimosa.
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Tujijengee KUJIAMINI watanzania.Ofcourse ukisimama kwenye fact hizo teams sio za kubeza kabisa,lakin WE CAN DO IT BETTER BWANA!

  mungu ibariki tanzania
   
 19. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 60
  Hakika umesema ila naomba kupingana na wewe kwenye hili la kusema unadhani tatizo si kocha bali ni wachezaji.
  mimi kwa mtazamo wangu nimeona matatizo yapo ambayo ni ya wachezaji na pia mwalimu wetu ana mapungufu yake. sitaki kuzungumzia sana ya wachezaji maana yanarekebishika na pia kama mchezaji harekebishiki ni jukumu la mwalimu kumuondosha na kumuongeza mwingine, hivyo nitazungumzia zaidi kuhusu mapungufu ya mwalimu.
  1.) Mwalimu wetu anasumbuliwa na woga wa kucheza mechi na timu zenye majina/ngumu. mfano i) mwaka juzi ilipokuja timu ya taifa ya Cyprus yeye alipeleka timu buliyankulu kwa mazoezi badala ya kuomba mechi nao. mfano ii) Kwenye Mechi na Cameroon hapa Dar, kipindi cha pili baada ya Chuji kuusoma mchezo na kuanza kuziona njia za kupita ngome ya Cameroon akawa anapeleka mashambulizi mbele, kocha alimtoa na kumuingiza mchezaji mwingine akisema Chuji alikua hajapona vizuri lakini ukiangalia kwa makini utaona kuwa aliogopa kwamba vile Chuji alikuwa akifungua mchezo ingekuwa hatari kama camerron wangefanya shambulizi la kushtukia, inamaana yeye alithamini Droo na Cameroon ambayo angeweza kuifunga ati kwa kuogopa asijefungwa.
  2.) Pressure ya mechi inamshinda sana maximo hasa kwenye kupanga timu wachezaji gani waanze na nani na saa ngapi awabadilishe, utakuta anafanya substitution too late tena baada ya mashabiki kumpigia makelele sana. kama wewe ni mhudhuriaji wa mechi za stars utakuwa umenielewa.
  Mimi naamini kama tungekuwa na mwalimu jasiri na udhamini tulionao na motisha zote zilizopo saa hizi tungekuwa tunawaza Afrika Kusini badala ya CHAN.
   
 20. Ayayoru

  Ayayoru Senior Member

  #20
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tukiamua tunaweza hakuna linaloshindikana tuwaombee vijana ili waweze kufanya vizuri katika hayo mashindano watutoe kimasomaso..................YES WE CAN......YES WE CAN......YES WE CAN.....YES WE CAN
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...