Champion Bus yaua watu 8

dah...pole kwa wote waliofikwa na msiba huu na mungu awape afya njema wale wote waliopata majeraha.
 
Tatizo mtu anakuwa na leseni kabla hata ya kujua kuendesha gari.WENGI HAWAJUI CODE ZA BARABARANI.
 
Mara nyingi madereva wanaobeba abiria ni wavuta bangi. Mfano daladala hapa bongo sijuhi ni kwanini
 
Hiz4 ajali zimeshakuwa kama wimbo...kila kukicha watu wanapoteza uhai,wengine viungo vya mwili,lakini serikali ipo kimya!wiki iliyopita Simba coach Tanga imeua,jana Mbamba bay tumepoteza ndugu zetu!POLENI WOTE wafiwa na majeruhi.
 
Naomba niwape pole wafiwa wote na kutoa rai kwa Serkali yote ya JMT kuwajibika kwa hili kwani moja wapo ya kazi yake ni kulina usalama na maisha ya raia wake. Kama wameshindwa hili wawapishe wengine watakao weza kujali wananchi wao.
 
Shida ninayoiona siyo VETA shida ni madereva kuizoea kazi kupita kiasi na kupuuzia alama za barabarani ikichagizwa na mwendo kasi, ubovu wa matairi, ubahiri wa matajiri kubadili mipira n.k


Mkuu usiombee na usiseme kitu kama hicho, kama ni dereva hata wa private yako utakuwa umeshawahi kupata kaajali hata uchwara je ulijitakaia?
Kwa kweli ajali isikie mwenzako kafikwa nayo au ndugu wa mwenzako basi wangekuwa ni ndugu zako wamepata hiyo ajali wala usingelopoka kuwa wacha wafe. Unajaua inawezekana wewe ni mmoja wa wale waliofanoikiwa kupata magari ya mitumba kutokana kuwaibia watanzania hivyo kudhani kila mtu asiye kuwa na gari ni mjinga.. TUSIOMBE NDUGU ZANGU AJALI MBAYA SANA. MUNGU AWAPE FARAJA WOTE NDUGU WA W WA WALIOPOTEZA MAISHA NA KUGANGA MAJERAHA YA WALIOPATA MAJERAHA
 
Baada ya kuwekewa lami yameshaanza kuchinja upande huo kweli madereva wabongo hatari sana
 
Tatizo la ajali hapa kwetu ni madereva. Hawa jamaa wanadharau hii kazi kiasi kwamba hawawezi kukaa darasani angalau hata mwezi mmoja wakapate elimu ya nidhamu ya barabarani.
Wangekuwa wanapitia VETA angalau ajali zisingekuwa nyingi.
Mfano mzuri ni madereva wanaotokea nchi za jirani kuja kwetu, mbona hawapati ajali?
Udereva jamani ni taaluma na ustadi, vyote hivyo vinapatikana VETA.

Hebu kanusha maneno yako hayo.
 
Kwa jinsi ninavyoelewa mimi,ajali nyingi husababishwa na matairi yanayoingizwa nchini bila kukaguliwa,mataili yasiyo na ubora yamekuwa mengi sana nchini,wauzaji wao wanaangalia faida tu mambo ya viwango hayawahusu,na serikali yetu haifatilii imekaa kimya tu,KAZI YAKE NAYO NI KULALAMA BILA KUCHUKUA HATUA,poleni wahanga wa ajali hiyo RIP MAREHEMU WOTE.
 
Acha tu waendelee kufa. Wanayataka wenyewe.

Hao waliokufa kwani wamependa..Fikilia mara 2 kabla haujatoa Coments kijana.Hii ni dunia,hujafa...hujaumbika.Shauri yako bwana mdogo.Ndugu zetu wametangulia mbele za haki,wewe unafurahia sio.Mungu akubariki na kukulinda.
 
Jamani ajali walio uawa ni wanawake 3,wanaume 3 na watoto 2.Chanzo ajali Polisi bado wanachunguza!SOURCE Personal observation na taarifa ya habari tokaTBC.
 
Champion Bus - ni kampuni kongwe ya mabasi, ilianzia na safari za Dodoma - Kondoa, Dodoma Dar na sasa naona kama hili lililopata ajali lilikuwa linatoka Mwanza na Shy. Ninalotaka kusema hapa ni hii kampuni ina mabasi mabovu wala usipime! Kila bus linapotoka safari unakuta liko juu ya mawe kwa matengenezo, unategemea nini hapo, vitu kama kukatika steering, kuzima taa za mbele ghafla, kupasuka mipira nk. ni vya kutegemewa sana kwenye mabasi ya mfumo huu wa spana mkononi. Ningepedekeza itungwe sheria ya kutupa magari (scrap) ya abiria yanapozidi umri wa miaka 25.
 
Back
Top Bottom