sasa hivi bungeni CYRIL CHAMI AKA BABA MKWE anamtetea MKurugenzi wa TBS kwa msuli mzito
mkuu, huwa sijuhi kwa nini mkurugenzi huyu ana andamwa sana! Ukiangalia kwa makini utakuta mambo wanayo mzulia niyakubuni tu, wafanya biashara wa magari hasa hasa mapya wanafanyaga kampeni kubwa sana hawataki watu wanunue used cars; kuna wakati fulani baadhi ya wafanya biashara walikuja na pendekezo eti magari yawe yanaingizwa nchini hivyo hivyo bila kukaguliwa - ukaguzi eti ufanywe nchini, mtu anayetoa mapendekezo kama hayo anakuwa na maana gani au ajenda gani ya siri.
Mimi nashauri tuwe makini sana na wafanya biashara, wana mbuni nyingi - chukulia mfano wa uingizaji wa mafuta in bulk, wafanya biashara wamekwisha anzisha malumbano na kuisema vibaya kampuni iliyo shinda tenda; mbinu hizi hizi ndio zinatumika kumsema vibaya mkurugenzi wa tbs. Watanzaia tusipo badilisha tabia zetu za kuchafuana kwa ajili ya maslahi tu hatutafika mbali - wenzetu kenya hawafanyi mambo ya ajabu kama ya kwetu hapa, tunapoteza muda mwingi kwenye malumbano ambayo hayana tija.