Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Messages
5,064
Points
2,000

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2018
5,064 2,000
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Hofu yako imetimia. Siku nyingine hakikisha unafikisha taarifa kote kote huenda zikafanyiwa kazi
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Messages
8,319
Points
2,000

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2017
8,319 2,000
Sa
Hofu yako imetimia. Siku nyingine hakikisha unafikisha taarifa kote kote huenda zikafanyiwa kazi
Sawasawa mkuu. Watu hatujifunzi kwa matukio ya wenzetu. Brazil walipigwa 7-1 nyumbani kwao kwa kosa la kujiamini kupita kiasi na kuwadharau wapinzani wao Ujerumani
 
Twamo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2017
Messages
1,692
Points
2,000

Twamo

JF-Expert Member
Joined May 27, 2017
1,692 2,000
Mleta uzi popote ulipo kunywa Pepsi mwambie muuzaji nitalipa
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
 
PTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
7,812
Points
2,000

PTER

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
7,812 2,000
Kwa jinsi walivyocheza simba kule msumbiji kuna hatari wakatolewa mapema tu kwenye michuano hii.

Wakishikiliwa mpaka penalty watatolewa tu maana wanavyocheza ni kama wanalewa kwanza ndiyo wanaingia uwanjani.
Mimi safari ya simba niliona kuwa nifupi sana toka mechi ya kule Mozambique na leo hili limejidhihirisha.
 
PTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
7,812
Points
2,000

PTER

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
7,812 2,000
Kuna wakati kama kweli tunazipenda timu zetu inabidi tuwaambie ukweli. Simba hii timu waliidharau na wamejiamini kupita kiasi. Wanaingia uwanjani kwa kucheza na historia

Waamke wachukulie mambo seriously
Wachezaji waliingia kwenye mtego wa mashabiki wa kujiamini kupita kiasi
 
Forum statistics

Threads 1,392,498
Members 528,634
Posts 34,110,518
Top