Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Messages
8,280
Points
2,000

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2015
8,280 2,000
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Una akili lakini wenzio ni mbumbumbu hawakukuelewa.
 
ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
5,458
Points
2,000

ZionGate

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
5,458 2,000
Hata kwenye ligi simba haitakuwa ya kutisha sana kama inavyodhaniwa kwanza kuna uwezekano wakamfukuza kocha
Kumfukuza kocha itakuwa kosa kubwa, sioni kosa lake, hizi lawama ziende kwa management kwa usajili usio na tija, viwango na kushindwa kuwabakiza baadhi ya wachezaji, yale ya kina wawa kupiga mpira na kuukosa kwenye mechi ya azam leo tena yamejirudia, pumzi hakuna.
 
Lukub

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Messages
1,567
Points
2,000

Lukub

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2012
1,567 2,000
Timu yetu ya simba tangu day one na Power dynamo kwakweli tunacheza hovyo sana kipindi cha kwanza.Hata Azam wangweza kumaliza mchezo kipindi cha kwa siku ile sema tu hawakuwa makini.Ukweli lazima usemwe first half zimekuwa si nzuri sana na huwa timu inakaba kwa macho. Tutakuja kushindiliwa goli na timu za ajabu ligi kuu na zisirudi walai tena. Kuna ombwe kubwa tena sana la ukabaji,tunaeza dhalilika siku tukikutana na mtani.
Wenye simba waliondoka nayo unamuacha KOTEI nilimuita invincible huyu ndie uti wa mgongo wa mafanikio ya simba mwaka Jana,OKWI ubishi mganda huyu ndio kwenye simba ,NIYONZIMA mechi zenye presha kama hizi anaziweza sana
 
pachachiza

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Messages
1,654
Points
2,000

pachachiza

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2012
1,654 2,000
Kumfukuza kocha itakuwa kosa kubwa, sioni kosa lake, hizi lawama ziende kwa management kwa usajili usio na tija, viwango na kushindwa kuwabakiza baadhi ya wachezaji, yale ya kina wawa kupiga mpira na kuukosa kwenye mechi ya azam leo tena yamejirudia, pumzi hakuna.
Usajili usio na tija upi wakati ni mapendekezo ya kocha
 
myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
3,434
Points
2,000

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
3,434 2,000
Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha
Kiongozi hii ni kweli kabisa! Sikumbuki ni lini tumewahi kuwafunga Msumbiji kuanzia kwenye klubs au timu ya taifa! Tangu walipotutia nuksi kwa Mchina, Msumbiji siwataki kabisa!! Yaani ile mijamaa inajua kabisa tumeiita kudumisha udugu wetu katika kuzindua uwanja wetu lakini bado ikatutandika!!!
 
Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Messages
5,457
Points
2,000

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2012
5,457 2,000
U
Kiongozi hii ni kweli kabisa! Sikumbuki ni lini tumewahi kuwafunga Msumbiji kuanzia kwenye klubs au timu ya taifa! Tangu walipotutia nuksi kwa Mchina, Msumbiji siwataki kabisa!! Yaani ile mijamaa inajua kabisa tumeiita kudumisha udugu wetu katika kuzindua uwanja wetu lakini bado ikatutandika!!!
Uwanja tulizindua na Uganda..wait walifuata baada ya Uganda mechi ya qualifications za CAF
 
myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
3,434
Points
2,000

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
3,434 2,000
U

Uwanja tulizindua na Uganda..wait walifuata baada ya Uganda mechi ya qualifications za CAF
Kumbe enh! Labda kwavile bado nina kumbukumbu mbaya ya ile mechi ambayo nilikuwa mkoa nikasafiri hadi Dar! Hadi leo naipata taswira ya wachezaji wa The Mambazi na zile jezi zao walivyokuwa wanashangilia ushindi!
 
Forum statistics

Threads 1,381,718
Members 526,174
Posts 33,809,692
Top