Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

Kuna wakati kama kweli tunazipenda timu zetu inabidi tuwaambie ukweli. Simba hii timu waliidharau na wamejiamini kupita kiasi. Wanaingia uwanjani kwa kucheza na historia

Waamke wachukulie mambo seriously
We jamaa vp. Ulikua unaleta hoja au umeleta kubishana?
Ingekua vyema ungetulia usikilize hoja za wenzako.
Kwanza umejichanganya Kwenye hoja yako, tunashukru umekiri hili.
Pili unavyosema Simba wamezadharau hii mechi ulitaka washambilie ugenini bila kujilinda?
Mwisho tafuta maneno ya kocha wa Simba baada ya mechi.
Ni kweli mechi itakua ngumu ka zilivyomechi nyingine, kwa nini uwe na hofu wakati unaenda vitani afu adui anakuja Kwenye ngome yako.
Twende uwanjani tukawatie Moyo wapiganaji wetu ushindi upo mikononi mwetu.
"Simba Nguvu moja"
 
Kwa maoni yangu Fraga azoeshwe hapo, atatusaidia sana huko mbeleni tukikutana na wajuvi zaidi kina Esperance.Halafu Tairone baadae aanze kupatna na Nyoni.Huyu Beki Mbrazili Tairone tunamuhitaji sana aondoe matatizo Mwaka Jana.Na Uzuri wote Nyoni na Tairone wanaweza Holding midfielder hivyo watakuwa wanampa Back up Fraga timu ikiwa INA mpira.
Mkuu Wala hujakosea kwa Fraga Nadhani mkude atumike kwenye mechi Za ligi ya Nyumbani zaidi na kule Za kimataifa asaidie saidie hasa Za home pia Tairone ana nguvu Sana anaweza pambana man-man na strikers wajanja wajanja wa CACL
Wawa mechi iliyopita alijitahidi lakini kwa Mpira wake kulazimisha achezeshwe yatakua Yale Yale
 
Wale jamaa wanaupiga mwingi na wanatengeneza nafasi kibao lakini wana allergy na kufunga, ni dhambi kubwa mno kuweka mpira nyavuni wale jamaa, kwa nafasi walizotengeneza siku ile na wakashindwa kuzitumia, nathubutu kusema Simba wasiwe na wasiwasi kabisa, wale jamaa hawang'ati
 
Unajiabisha, sare ya 1-1 Taifa inampa advantage gani Yanga wakat alikuwa mwenyeji mzee?
Simba wana option zaidi ya ushindi mkuu? Yanga wao wanawza wakatoka sare wakafuzu, au hesabu za goli la ugenini zinakupiga chenga?
 
Ina maana hujanielewa???kusema Tunaweza kuifunga Barcelona ni alama Ya Mentality ya Ushindi iliyoko Simba!!Ukiwa na Wanasimba ukawaambia Tunaweza kuifunga Barcelona wanakupa tano, ukisema hivi Jangwani wanaweza kukukimbiza kama MTU aliyegundulika anaenda kuchomoa betri!!!Bado tu hujaelewa??
 
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Bora umewaambia,kumbe si wite mbumbumbu kuna wanaofikiri Vizuri, game iko open sana maana wale wanakuja kujilipua tu hawana chakupoteza
 
Bora umewaambia,kumbe si wite mbumbumbu kuna wanaofikiri Vizuri, game iko open sana maana wale wanakuja kujilipua tu hawana chakupoteza
That is my argument mkuu nashangaa Lunyasi wenzangu wakanishukia kama mwewe

Jambo jingine la kuhofia ni mentality ya kudhani Simba inauwezo wa kushinda mechi zote U/Taifa na hivyo kujijengea over confidence ambayo ni hatari hasa unapocheza na timu inayoona haina cha kupoteza
 
Kitu ambacho bado hujaelewa ni kwamba Simba hatuhitaji kuweka hisia za Uoga mbele kama Vyura, Hisia za mashabiki wa Simba ktk hatari ni kama hisia za Mmasai anapokutana na mnyama Simba porini,hisia za mashabiki wa Yanga ni kama Mzaramo anapokutana na mnyama Simba!Hapa mzaramo atawaza kufa tu na kukimbia!!

Sasa hii unayoona mashabiki wenzako wa Simba wanapambana na wewe ni kwamba hatuhitaji hisia za kiyangayanga!!Tunaona unataka kutuambukiza hisia za kufa kufa tu hisia za kiyanga hizo.Hatuzihitaji.Kitu kimoja unatakiwa ujue usione Masai ni Jasiri kupambana na Simba ukadhani Masai eti hajui kama Simba anaua.Ukishindwa kuelewa kwa maelezo haya utakuwa umeshindikana
 
M
Mwaka 2003 Simba ilipocheza hatua ya makundi kwa mara ya kwanza CCL alikua ametoka kukutana na mazingira kama hayo kwenye hatua za awali.

Ilitoka 0-0 kwenye Uwanja wa Taifa Shamba la bibi na Santos waliokua mabingwa wa South Africa na katika mechi ya marudiano iliyofanyika kule Bondeni wakatoka sare ya 1-1 na hivyo Simba ikafuzu kwa faida ya goli la ugenini

Mazingira hayo ndio yananifanya niwe na hofu pamoja na tabia ya timu zetu kudharau baadhi ya timu hasa za Msumbiji ambazo kiuhalisia mpira wao na wetu haupishani sana na huwenda wakawa juu zaidi yetu
Mwambie aliyekusimulia amekudanganya, hayo sio matokeo ya Santos Vs Simba! Nyau jike weee
 
Nimekaa mara fikra za woga zimenijia. Nahofia timu yangu Lunyasi wa Msimbazi kuaga mapema kwenye michuano ya CCL. Naomba iwe ni ndoto tu

Kumbuka kwenye mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana AS SONGO ya Msumbiji

Ndugu zangu sare ya bilakufungana ugenini ni hatari sana. Unatembea kwenye uzi mwembaamba sana baina ya kusongambele na kutupwa nje ya mashindano.

Hapo hakuna alternative kwa Simba zaidi ya ushindi. Afadhali ile sare waliotoka watani zetu wa Jangwani na Township Rollers, sare ya bao moja kwa moja. Kama Yanga wakikaza ugenini wakatoka angalau sare ya bao mbili kwa mbili au zaidi wanafuzu kwa raundi inayofuata

Msimbazi akitoa sare ya magoli ya aina yoyote anaaga mashindano, suluhu ya bilabila ni changamoto ya mikwaju ya penati ambayo sikuzote haina mwenyewe!

Tuliidharau timu hii ya Mozambique lakini siku zote Msumbiji hua inatusumbua sana iwe kwa ngazi ya vilabu na hata timu ya Taifa. Wana style yao ya kufunga goli dakika tano za mwanzo na likang'ang'ania hadi mpira unaisha

Natoa wito kwa viongozi na hasa benchi la ufundi wasiwachukulie poa hawa jamaa

Waache kabisa tabia yao ya kufanya majaribio ya wachezaji na aina ya uchezaji, tabia ambayo kocha wetu Patric anayo sana. Waweke kikosi cha kazi isitukute aibu tukakosa pa kuweka sura zetu

Sisi mashabiki panapo majaaliwa tutakuwepo uwanja wa Taifa kutoa sapoti inayohitajika kama kawaida yetu

SIMBA NGUVU MOJA
Wee endelea kukaa hapo watu wameshachomoa betriii

Hizo hofu peleka churani!
 
Watoto wadogo kwa kigezo gani lazima uwafunge , kuwafunga ni baada ya dk 90 umetengulia goli moja mbele , tuache kujipa matumaini makubwa huu ni mpira unamaajabu yake.
Huenda hajui mpira mkuu, hajui kuwa Vyura wanalazimika jua liwake au lisiwake ni lazima wafunge goli ndio wapite na hapo itategemea na FT results.
.
Simba hapa lazima ashinde wale watoto wadogo sana
 
Watu wanashindwa kuelewa ukweli kwamba Simba anakiwa kushinda tu ,safe yoyote ibamtupa nje ya mashindano , bila bila anakutana na mikwaju ya penati
Yanga yeye akipata 1-1 anakutana na mikwaju ya penati ila 2-2 ,3-3 na kuendelea Yanga anasonga mbele kwa goli la ugenini.
Simba wana option zaidi ya ushindi mkuu? Yanga wao wanawza wakatoka sare wakafuzu, au hesabu za goli la ugenini zinakupiga chenga?
 
Watu wanashindwa kuelewa ukweli kwamba Simba anakiwa kushinda tu ,safe yoyote ibamtupa nje ya mashindano , bila bila anakutana na mikwaju ya penati
Yanga yeye akipata 1-1 anakutana na mikwaju ya penati ila 2-2 ,3-3 na kuendelea Yanga anasonga mbele kwa goli la ugenini.
Yanga akipata droo ya 0-0 inakuwaje mbona hutaji??Yanga ili aendelee ni lazima afunge goli asipofunga goli lolote njeeee mbona husemi??

Sisi Simba tunajua kazi tuliyonayo ni Kumrarua UD Songo, hayo matokeo mengine mnajua ninyi Yanga na mashabiki wenye Uyangayanga(hali ya kuwa na hofu ya kushindwa muda wote)
 
Back
Top Bottom