Chama kipya cha ACT Tanzania chaendelea kurudia makosa ya vyama vya Upinzani Tanzania

Bavicha lakuvunda hata mfanye nini mnalo limewaganda kichwani zitto atawalaza nje mwaka huu.

Kama cdm inavyoendelea kuwalaza nje nyie ma ccm kwani kila uchaguzi wa serikali za mitaa mmeona moto wa cdm kwani tauari mnaitwa chama cha upinzani.Hadi kinana ameamua kujitoa akili kwa kutembea na fisi mikutanoni ili apate anagalau wa kuja kushangaa fisi
 
Kama cdm inavyoendelea kuwalaza nje nyie ma ccm kwani kila uchaguzi wa serikali za mitaa mmeona moto wa cdm kwani tauari mnaitwa chama cha upinzani.Hadi kinana ameamua kujitoa akili kwa kutembea na fisi mikutanoni ili apate anagalau wa kuja kushangaa fisi
Hebu weka wazi kwanza maslahi yako chadema ni chama cha ukoo wewe upo familia ipi kwa mtei au kwa mbowe?
 
Sijui atamdanganya nani amwamini ameshindwa kwa chama kilicho mlea akaweka tamaa mbele cjui kama atamaliza mwaka.
Zitto hayupo kwenye ukoo wa mtei na mbowe kwakuwa chama ni chama cha ukoo hana chake ndiyo maana kafukuzwa.
 
Unajua maan ya neno saccos???umeshawah kuchangia??kukopa?kukopeshwa??tumia ubongo unapoaandika kuliko kiungo kingine!!!
 
Ndani ya Chama cha kweli cha siasa na Mwanasiasa wa kweli haabudiwi mtu bali zinaabudiwa na kufuatwa Sera, ahadi, itikadi, imani, madhumuni na kanuni za chama.

Ukifuta U-kinana,U-zitto,U-mbowe,U-slaa,U-lipumba basi jua umeingia katika chama kama zuzu asiyejua amefuta nini ndani ya chama.
 
Ni kweli, zitto alitumia muda mwingi kujijenga yeye binafsi badala ya kukijenga chama chake kipindi kile hasa kule kigoma! Alitumia muda mwingi kuwanadi wagombea wa nccr mageuzi badala ya cdm! Zitto ni msaliti.
 
Madua ya kuku ni mengi kweli kweli.

Mpeni muda ajenge chama kwa Uhuru, haya mambo mengine ya kumkejeli Hayana msingi kwa sasa. Kama kweli ni msaliti, wakati utatuambia.

Wafuasi Wa Chadema mnaonyesha kutokomaa kisiasa. ZZK ni mwanasiasa, ilikuwa lazima atafute mahali pengine pa kufanyia siasa. Sasa mlitaka afanye nini ili mridhike. Na sasa utawezaje kumridhisha kila mtu.

Tuache demokrasia ifanye kazi yake.
 
Jana Zitto Zuberi Kabwe amechukua kadi ya uanachama wa chama kipya cha ACT-Tanzania na kuwa mwanachama rasmi pamoja na kuwa mwanachama wa ACT-Tanzania kwa kificho kwa muda wa mwaka mzima.

Hii inaweza ikawa ni furaha kwa wanachama wachache wa ACT-Tanzania ambao walikuwa wanasubiria kwa hamu uamuzi huo kwa msingi kwamba yeye ndiye anayeweza kukisaida chama hicho kupata umaarufu.

Historia ya vyama vingi kwa upinzani, sio Tanzania tu na hata barani Afrika kwa ujumla inaonyesha kuwa vyama vingi vya upinzani vilijenga tumaini kwa watu badala ya sera zao.

Na hii imeletezea tatizo la vyama hivi kufa au kupoteza nguvu baada ya watu hao maarufu kuhama au kufukuzwa. Historia inaonyesha kuwa vyama kama NCCR-Mageuzi, TLP, nk vilipoteza umaarufu kwasababu ya viongozi walikuwa wakionekana ndio chama kuhama au kufukuzwa. Siku moja nilimsikia Zitto Kabwe akisema, uwezi kumgusa Zitto na CHADEMA ikabaki salama.

Hii ni dhana inaoyoosha kuwa hata wanasiasa wetu wanajijenga wenyewe badala ya kujenga TAASISI. Chama kama CCM kimejitahidi kujenga misingi ya watu kuamini katika taasisi badala ya watu, na kwa hiyo unaweza ukamfukuza mtu au watu, chama kisiathirike sana, kama inavyoweza tokea kwenye vyama vya upinzani.


Chama hiki kipya yaani ACT-Tanzania kimerudia makosa yale yale, pamoja na kuwa na washauri wasomi kama Prof. Kitila Mkumbo. Ni kweli kuwa kuna principle ya leadership inayodai...A leader must have followers, however tunamtegemea huyu leader awasaidie wafuasi wake wafahamu misingi ya taasisi yake, badala ya kumfuata tu yeye.

Msingi ni kuwa, huyu leader anaweza kukengeuka wakati wowote na akafanya maamuzi ya ovyo kabisa, bila kuwa na misingi imara unaweza ukapoteza kwa kiwango kikubwa.

Kinachoendelea ACT-Tanzania ni kujenga taasisi juu ya Zitto Kabwe, badala ya kujenga taasisi juu ya misingi ya falsafa na sera zake.

Wakati CHADEMA wanachukua maamuzi ya kuwafuta uanachama Kitila, Mwigamba na Zitto, ilisemwa...."CHAMA NI ZAIDI YA MTU, NA HAKUNA MTU MAARUFU ZAIDI YA CHAMA" Kauli hii ilikuwa ni msingi dhabiti wa kuanza kutoka kwenye mwelekeo wa kujenga taasisi juu ya umaarufu wa mtu. Ifike kipindi tuache U-Zitto, U-Slaa, U-Mbowe, U-Lowasa, nk. Kwangu mimi naendelea kufatilia mwelekeo wa ACT-Tanzania.

Ukweli ni kama Zitto Kabwe asipoweza kukipa umaarufu ACT-Tanzania, basi huo ndio mwisho wa Zitto na ACT-Tanzania yenyewe.

Nawasilisha!!!!!

Mkuu Umezungumza Mambo ya Msing sana na kuongezea tu Watu waache Siasa za Kinafki na kufata Mkumbo kwa Njia hii tutafika!
 
Kula tano;na pia upinzani waelewe kupishana mawazo sio usaliti bali ndio demokrasia yenyewe na pia waache kudhani wao wapo juu ya sheria kwa kutesa watu kama ni kweli kwani ukweli halisi wanaujua wao na pia waache kuundiana zengwe zisizo na msingi kwa maslahi binafsi

Kuanzisha chama ndani ya chama Ni kupishana mawazo?Kutumika na chama tawala kudhoofisha chama ulichopo Ni kupishana mawazo?
Na waliomtesa Dr Ulimboka na kumuua Mwangosi ndio wapo juu ya sheria?Tumia ubongo kufikiri
 
A well written article, ACT wanaleta mambo ya NCCR Mageuzi ya Mrema, akahama na chama nacho kikayumba, nampongeza sana Mbatia kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya.CHADEMA haiwezi kumnyenyeke mtu ambaye anajiona yupo juu ya taasis, hiki chama kimeundwa kwa juhudi na nguvu kubwa, hatuwezi kukubali mtu mmoja ajione ni maarufu sana na atishie uhai wa chama, wanaokwenda nae waende tu, sisi tupo na tutaendelea kuwepo.
 
Kwa siasa ninavoijua ni vigumu sasa upinzani kupenya Ikulu kwani kitakachotokea CDM itachukua muda mwingi sasa kumwandama Zitto na kusahau kujenga chama ili hali yeye atautumia muda mwingi kukijenga chama chake na hali hiyo itawagharimu sana vyama vingine vya upinzani.

Prove!
 
A well written article, ACT wanaleta mambo ya NCCR Mageuzi ya Mrema, akahama na chama nacho kikayumba, nampongeza sana Mbatia kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya.CHADEMA haiwezi kumnyenyeke mtu ambaye anajiona yupo juu ya taasis, hiki chama kimeundwa kwa juhudi na nguvu kubwa, hatuwezi kukubali mtu mmoja ajione ni maarufu sana na atishie uhai wa chama, wanaokwenda nae waende tu, sisi tupo na tutaendelea kuwepo.
 
Hiko sio chama mkuu, wajanja wananielewa. Hiko ni kikundi ama kusanyiko la wasaliti. Falsafa yao ni bomoa upinzani saidi ccm. Iko strongly financed and monitored na ccm!

kweli mkuu,sema wabongo wengi wapo usingizini,tena usingizi wa pono.
 
Back
Top Bottom