Chama dola kinapokosa upinzani tutegemee nini?

Huko huko, lakini with current trends, hata mabeberu wanawzxa kusupport civil war ikianziswa na wasioweza kustahimili uonevu wa sasa. Nguvu ya umma haiwezekani kwa sasa, tu waogoa wa kufa sana tena sana!
Sasa kama wananchi ni waoga hiyo civil war atakubari nani kuwa frontline? Na tukienda front line tunataka tumpe nani madaraka? Juzi niliona hata Chadema vijana wanasema Mh.Mbowe hakuna kuachia uwenyekiti sasa nkafikiria je angekua ameshika dola kweli hata muda wa urais ukiisha atakubari kuachia Mbowe mwenyewe?
Mabadiriko tunayapenda lakini sasa nani mbadala au nani kule aliko anaonyesha demokrasia ya mfano mzuri? Mwisho ndo najisemea wanadamu wote ni sawa tu.
 
Jana Bashiru amesema walioomba msamaha kesi yao bado mbichi kabisa, hapo wemye akili mtaelewa kuwa huko mbele utakuwa mwendo wa visasi tu.
 
Sasa kama wananchi ni waoga hiyo civil war atakubari nani kuwa frontline? Na tukienda front line tunataka tumpe nani madaraka? Juzi niliona hata Chadema vijana wanasema Mh.Mbowe hakuna kuachia uwenyekiti sasa nkafikiria je angekua ameshika dola kweli hata muda wa urais ukiisha atakubari kuachia Mbowe mwenyewe?
Mabadiriko tunayapenda lakini sasa nani mbadala au nani kule aliko anaonyesha demokrasia ya mfano mzuri? Mwisho ndo najisemea wanadamu wote ni sawa tu.
Taratibu kila kitu kinahitaji mipango mkuu tusikurupuke lakini tuwe na malengo.
 
Mh.Mbowe hakuna kuachia uwenyekiti sasa nkafikiria je angekua ameshika dola kweli hata muda wa urais ukiisha atakubari kuachia Mbowe mwenyewe
wanasema hivyo kwa vile Jiwe alivyo apa kuua upinzani, wanadhani lazima ake tu anayefahamika kufia chama! Akina say Polepole , Bashiru siyo wafia chama ni matumbo yao! Hao hawawezi kuhimiri mitiksiko ya kufilisiwa/kufungwa/kuuawa etc (natolea mfano... hivyo hivyo kwa CDM walikuwepo watu akina Waitara....
 
View attachment 1275940

Gen Paul Kagame alipotwaa madaraka alicheza kulinyoosha Bunge halafu akavimaliza vyama vya upinzani,watu wa chama chake RPF wakabaki wanamshangilia na kuona wamebaki wao tu kama chama tawala!

Baada ya kuona sasa bunge ni dhaifu, mahakama ni yake na vyama vya upinzani vimebaki majina tu na wapinzani akawatia ndani, akaanza kushughulikia na chama chake RPF mbacho ni maswahiba zake waliomwingiza madarakani kutoka chama cha RPF.

Akaanza na Mkuu wa inteligensia Kanal Patrick Karegea na Mkuu wa mMjeshi Gen Kayumba Nyamwasa,akawafuta kazi na wakakimbilia afrika ya kusini kuokoa maisha yako na wengine wengi wakakimbia Rwanda na kwenda kuishi uhamishoni ile top cream ya RPF iko uhamishoni kuhofia maisha yao,leo amebaki mwenyewe!

Sasa anatamba na ameunganisha chama chake rpf na jeshi sasa system inafanya uchaguzi na anashinda mwenyewe na ameshaongeza muda wa kukaa madarakani! Ni mwerevu sana na sasa anatamba mwenyewe kama tembo uwanjani! Chama cha RPF sasa ni system ya jeshi siyo chama tena! Anakula bata na ukimsema vibaya haupo labda uzungumze ukiwa chumbani na mkeo!

Naona mahali fulani chama tawala wanashangilia vyama vya upinzani kufa,bunge dhaifu na mahakama kutotenda haki,nawashangaa kwani wanaelekea huko!Wanakoelekea chama kitabaki jina tu na wataanza kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe hamani, madudu ya awamu zilizopita yatawekwa hadharani.

Wengi watafungwa na wengine watakimbia nchi ili bwana mkubwa abakie kama tembo uwanjani baada ya hapo chama kitaungwa na vyombo, muda utaongezwa basi mchezo umekwisha na chama kitabaki jina mfumo utatawala! Uchaguzi hewa na mambo. Chama tawala ni sawa na kuni mbichi inayocheka kuni kavu ambayo ni vyama vya upinzani iko jikoni kwa sasa wakati kesho ni zamu yake!. Kuna mtabiri aliwahi kusema akimalizana na sisi atakuja kwenu!
Sawa naona kuna mantiki, lakini ni vizuri kuangalia role ya deep state na international community,sidhani kama zitaruhusu kufika huko.
Kuweka rekodi sawa, Kagame hakuanza na wakina Karegeya (RIP) na Nyamwasa, hawa ni victims wa miaka ya karibuni kabisa, kwenye 2000s huku, in fact Nyamwasa kabla hajakimbia alishapoteza ukuu wa majeshi na kupewa ubalozi wa India . Kagame and his cronies, wameanza kuua na kuvuruga watu wa serikali yao wenyewe na RPF mapema sana. Faustin Twagiramungu, Pasteur Bizimungu, Seth Sendashonga na wengine wengi waliuawa,kufungwa au kulazimika kwenda uhamishoni mapema sana. Si ajabu Kagame alikuwa hata nyuma ya mauaji ya Fred Gisa Rwigyema hata kabla RPF haijakamata madaraka.
Kama mtu na kundi lake wameamua kuwa wauaji na wakandamizaji, hata bunge na mahakama neutral haviwezi kusaidia. Wataumiza wenzao kwa sababu agencies za ulinzi na usalama wanazi control wao.
 
Back
Top Bottom