Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,270
Gen Paul Kagame alipotwaa madaraka alicheza kulinyoosha Bunge halafu akavimaliza vyama vya upinzani,watu wa chama chake RPF wakabaki wanamshangilia na kuona wamebaki wao tu kama chama tawala!
Baada ya kuona sasa bunge ni dhaifu, mahakama ni yake na vyama vya upinzani vimebaki majina tu na wapinzani akawatia ndani, akaanza kushughulikia na chama chake RPF mbacho ni maswahiba zake waliomwingiza madarakani kutoka chama cha RPF.
Akaanza na Mkuu wa inteligensia Kanal Patrick Karegea na Mkuu wa mMjeshi Gen Kayumba Nyamwasa,akawafuta kazi na wakakimbilia afrika ya kusini kuokoa maisha yako na wengine wengi wakakimbia Rwanda na kwenda kuishi uhamishoni ile top cream ya RPF iko uhamishoni kuhofia maisha yao,leo amebaki mwenyewe!
Sasa anatamba na ameunganisha chama chake rpf na jeshi sasa system inafanya uchaguzi na anashinda mwenyewe na ameshaongeza muda wa kukaa madarakani! Ni mwerevu sana na sasa anatamba mwenyewe kama tembo uwanjani! Chama cha RPF sasa ni system ya jeshi siyo chama tena! Anakula bata na ukimsema vibaya haupo labda uzungumze ukiwa chumbani na mkeo!
Naona mahali fulani chama tawala wanashangilia vyama vya upinzani kufa,bunge dhaifu na mahakama kutotenda haki,nawashangaa kwani wanaelekea huko!Wanakoelekea chama kitabaki jina tu na wataanza kushughulikiana wenyewe kwa wenyewe hamani, madudu ya awamu zilizopita yatawekwa hadharani.
Wengi watafungwa na wengine watakimbia nchi ili bwana mkubwa abakie kama tembo uwanjani baada ya hapo chama kitaungwa na vyombo, muda utaongezwa basi mchezo umekwisha na chama kitabaki jina mfumo utatawala! Uchaguzi hewa na mambo. Chama tawala ni sawa na kuni mbichi inayocheka kuni kavu ambayo ni vyama vya upinzani iko jikoni kwa sasa wakati kesho ni zamu yake!. Kuna mtabiri aliwahi kusema akimalizana na sisi atakuja kwenu!