Chama cha Walimu CWT chaanza kumeguka vipande vipande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha Walimu CWT chaanza kumeguka vipande vipande

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by thatha, Jun 16, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Walimu watangaza mgogoro na chama chao

  By Thobias Mwanakatwe | 16th June 2012

  Walimu nchini wametangaza mgogoro dhidi ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambao unaweza kusababisha mgomo wa nchi nzima kutokana na kutoridhishwa na mambo kadhaa ya ukandamizaji yanayoendelea ndani ya chama hicho.

  Kwa mujibu wa taarifa waliyoisambaza kwa vyombo vya habari, walimu wa mkoa wa Kigoma walisema kutokana na hali ilivyo ndani ya chama hicho kuna haja kwa serikali kuingilia kati mgogoro huo unaoendelea kufukuta ambao umeanza kusababisha walimu kukosa ari na moyo wa kufundisha na usumbufu mwingi wa kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi.

  "Wanachama wamenyimwa fursa na demokrasia ya kutoa mawazo na kutatua matatizo yao kwa njia ya mikutano katika vituo vyao vya kazi kwa sababu katiba mbaya ya CWT, toleo la Desemba 18, 2009 kifungu cha 11 ( a) – (c), haiwapi madaraka wawakilishi kuitisha mikutano katika sehemu zao za kazi,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Walimu hao walisema wamekuwa wakikatwa asilimia mbili ya mishahara yao ya kila mwezi kama ada ya uanachama hata wale ambao hawajajiunga uanachama jambo ambalo limekuwa likiwashangaza walimu wapya kutokana na kuwepo kwa utaratibu huo kandamizi.

  Walisema chama kimekuwa hakina uwazi katika matumizi ya pesa za wanachama na wasio wanachama wake kwa mfano makato ya ada ya uwakala ya wasio wanachama yanapaswa kuwekwa katika akaunti tofauti na ile ya wanachama wake kutokana na kifungu cha 72 (3) (e) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/ 2004;

  Walimu hao walisema kinachowashangaza ni kutokuwepo na sheria inayoruhusu mwalimu kujiondoa ndani ya chama na asiendelee kukwatwa ada ya uanachama na kuhoji suala la sheria ipi inayowaingiza kwenye makampuni ambayo yameanzishwa na CWT.

  Aidha, wamelalamikia chama kuendeshwa kibiashara bila wanachama kujulishwa kama kampuni hiyo ni ya nani na ipo kwa faida ya nani na pia zipo taarifa za kuanzishwa kwa benki wakati katiba ya CWT haisemi lolote kuhusu benki hiyo.

  Walisema kama mambo hayo yanayoendelea ndani ya chama hicho hayatapatiwa ufumbuzi na viongozi wa CWT watalazimika kutumia vyombo vya sheria kudai haki yao.

  Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Grasian Mkoba, akizungumzia malalamiko hayo alisema walimu ambao siyo wanachama wa chama hicho wanakatwa ada ya uanachama kutokana na sheria iliyoanzishwa na vyama vya wafanyakazi.

  "Sheria iliyoanzisha vyama vya wafanyakazi inasema kuwa wanachama watarajiwa wakijiunga na chama zaidi ya nusu yao waliobaki wanakatwa ada ya chama hata kama hawajajiunga,"alisema Mkoba.

  Mkoba alisema kwa walimu ambao wanataka kujiondoa ndani ya chama wanaweza wakafanya hivyo kwa kuandika barua lakini sheria inasema kama waliobaki ndani ya chama ni zaidi ya nusu waliojiondoa wataendelea kukatwa ada ya uachama hata kama wamejiondoa.


  SOURCE: NIPASHE
   
 2. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Walimu vumilieni kidogo,Chidabilyuti kitakufa na nyinyiemu yake.VIONGOZI WA CWT NI MAFISADI WA KUTUPWA.2016 ITAUNDWA TTF[TANZANIA TEACHERS FORUM].
   
 3. S

  STIDE JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Aisee!! Huu ni wizi wa hali ya juu sana!! Iweje mwalimu asiekuwa mwanachama aendelee kukatwa mshahara wake!!? Analipia nini wakati hajajiunga kwenye chama!!?

  Ila acha wakome waache kuwakumbatia Magamba!!!
   
 4. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,721
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  kwanza ni wizi wa hali ya juu,utaratibu unaotumiwa na cwt sio ulioko katika sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004,kuna ukiukwaji mkubwa sana wa sheria za kazi juu ya uanachama wa chama cha wafanyakazi na utaratibu mzima wa kujiunga.
   
 5. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  hivi vyama badala ya kutetea wafanyakazi wao wanazidi kuwadidimiza angalia watu wanavyohangaika kupata mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,ona pesa za wafanyakazi zinavyofujwa kwenye mifuko ya hifadhi ya taifa wakitoka hapo wanaenda kugombea ubunge walimu wako sahihi tujifunze kwa vyama kama vya south africa wakiamua mshahara upande lazima utapanda
   
 6. Mzururaji

  Mzururaji JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,236
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Tatizo viongoz wa cwt wamekaa kimaslai mno cjui itakuwaje hawapo kupigania maslai ya walimu kabsa kwa mfano utakuta mwl anaanza kazi hapat mshahara ukienda cwt wanasema tutawasliana na afisa elim ukiondoka ndo kwisha habar ya ndo mana walimu wa kasulu wameanzisha CWVT yan chama cha walim vijana tanzania ambapo wakijiongoza wenyewe wameweza kufuatilia mishahara yao had kutishia kwenda kulala kwa mkurugenz cha ajabu kesho yake mshahara ukatoka cwt kimya walimu mlete mabadiliko bwana achen ujinga wenu
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Walimu hawata kaa wafanikiwe kwa ujinga wao wa kutokuwa na msimamo thabiti....
   
 8. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Najuutaaa kuwa.......Lakini inabidi waelewe sasa ivi wanaajiriwa maticha na cyo walimu na ka-idadi kanaongezeka.Kigoma,Maticha 'Thumbs up'!
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  poleni walimu
   
 10. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,084
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  walimu hali mbaya sana...ninaona dalili ya kuwa na kanda zenye matawi yenye nguvu, kigoma amabyo ni kanda ya ziwa mpaka mwanza nk.

  kanda ingine ni kaskazini kwinineko uvundo mtupu
   
 11. B

  Bob G JF Bronze Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wajinga wengi wasione hela ni lazima wagawanyike! Huyo Ticha ajitoa CWT then akifukuzwa kazi na Magamba atajuta kujitoa CWT. Vyama hivi vipo kwa sheria haviwezi kuwa na sheria kandamizi kwa kuwa na miradi ya kuongeza kipato kwa mwanachama wake. Benki haiwezi kuwemo kwenye katiba ya CWT atumie akili
   
 12. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nina kaka yangu anaiponda kweli CWT. Madai yake yanaonekana ni ya msingi; yaani hawa jamaa wa ngazi za juu nasikia hawataki mawasiliano kabisa na mwalimu wa ngazi ya chini. Mambo yote wanafanya wao huko juu. Na ndo maana CWT haina hata tovuti, hii yote ni njia ya kuhakikisha kuwa wanachama wao wanakosa mahali popote pa kutolea maoni yao. Namba za simu za mkononi ni nadra kuzipata ukiwa mwl. wa kawaida...!
   
 13. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama walimu wa Tanzania wanataka kiama yao wameguke vipande!
  Ninachofahamu hata wengine wakiunda chama kingine lazima watahitaji fedha ya kuendesha chama chao, na fedha hiyo itatokana na na michango ya wanachama. CWT ina matatizo dawa ya matatizo hayo ni walimu kukisimamia chama chao, walimu wamewekeza fedha zao kwa miaka mingi haina sababu ya kuanza kujitoa na kuwaachia wengine, mtakua adui ninyi kwa ninyi.
  Wengi wa waalimu ni waoga sana mnahaja ya kujitazama upya, adui yenu yupo nje yenu na wasaliti wapo ndani yenu hao waondoeni muunde umoja wenye nguvu lakini mukianza kukitazama chama kama adui mtakua mnatekeleza agenda ya serikali ya kukiweka mfukoni chama chenu.
   
 14. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Hivi hii sheria kandamizi ilitungwa na nani? Eti kama nusu wataendelea kuwa wanachama basi nusu nyingine watakatwa michango hata kama sio wanachama! Huu ni ukandamizaji, yaani nijiondoe kwenye chama alafu ela iendelee kukatwa!

  Mimi sio mwalimu lakini hata kwenye katiba ya TALGWU kuna kifungu hiki. Wanasheria tusaidieni jamani kuhusu ukandamizaji huu. Hatutaki kuwa wanachama wa vyama hivi ambavyo vingi ni mawakala wa nyinyiemu!
   
 15. G

  Gilly Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sasa ni wakati muafaka kama kungekuwa na Chama cha Walimu na Wazazi cha Tanzania (Tanzania Parents and Teachers Association) wote wangekuwa na ajenda ya kudai mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia watoto wetu kuanzia Awali hadi Chuo Kikuu. Hii ni pamoja na kudai mazingira yanayomotisha walimu kufanya kazi yao ya kufundisha bila mahangaiko. Kwa kuanzia tu, kitu kama Jumuiya ya Wazazi (TAPA) wanafanya nini CCM? Mimi naona TAPA hawana ajenda tofauti na wazazi wenye watoto wanaosoma kwenye shule. Jumuiya hiyo ingetoka tu CCM na kuungana na Walimu na kuanzisha Chama cha Wazazi na Walimu Tanzania. Chama hicho kingeweza kuibana serikali itoe bajeti nzuri zaidi kuboresha elimu. Utaalamu wa walimu ungeweza kusikilizwa. Ugomvi na misuguano kinzani ya wazazi na walimu kuhusu malezi ya watoto wetu inaweza kutatuliwa. Mapendekezo kuhusu mfumo mzuri wa elimu yetu yanaweza kushinikizwa na serikali ikakubali siyo kama ilivyo sasa.

  Ikumbukwe kuwa maslahi ya mwalimu siyo mshahara tu. Kuna vitu vingi.
   
 16. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mimi nimeshagoma zamaaani.
   
 17. M

  Mtimba Member

  #17
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Katiba ya nchi ambayo ndio sheria mama inasema mtu yoyote hatalazimishwa kujiunga na shirika au chama chochote bila ridhaa yake.ilishatokea kwangu wakati naanza kazi pesa yangu ikapelekwa nssf kabla sijajiunga nao nikakomaa nao na kuwambia sitaki hapo na nataka hapa maana mashirika ya hifadhi ya jamii yako mengi,walirudisha pesa yangu na nikachagua pa kuchangia.Hivyo waalim wana nafasi kisheria ya kudai hasa wale walioanza kukatwa pesa zao bila kukubali kujiunga na chama hicho.Haki hiyo inatokana na katiba ya nchi na sio kukandamizwa na sheria za kipuuzi ambazo zinakiuka katiba.
   
Loading...