MJINI CHAI
JF-Expert Member
- Dec 12, 2010
- 2,198
- 1,226
Pamoja na Jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha zao la korosho kwa wakulima kupata bei nzuri ambayo haijawahi kutokea hapo nyuma kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, mfumo huu umeingia dosari kwa baadhi ya maeneo kama Mtama kwa Nape baadhi ya wakulima mpaka sasa wanahangaika bila kupata msaada na majibu ya kutosha baada ya Majina yao kuwepo kwenye orodha ya malipo awamu ya pili, lakini wanapoenda banki hawakuti pesa.
Wakimuuliza Kiongozi/Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika ambao wanaandaa hundi na kupeleka benki husika wamekuwa wakiazungusha wananchi na kuwalaghai ya kuwa hundi zilikosewa, wakati wengine huombwa stakabadhi ili wathibitishe na wakiziacha tu kwa uelewa mdogo wa kisheria basi viongozi hao huzipoteza na kukosekana ushahidi.
Zoezi la kulipa kwa awamu ya Pili lilifanyika mwezi wa November 2017 lakini mpaka leo hakuna kinachojulikana.Tafadhali Mamlaka ya Korosho wasaidieni hawa wakulima ambao wanateseka kudai pesa zao.
MTAMA ya Mh. Nape, Mh. Majaliwa, Mh. Magufuli, bado kuna watu wanarudisha nyuma jitihada zenu!!