Chama cha SAU chazindua oparesheni Mchwa: yamnasa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo Mkuranga kupitia ACT Wazalendo

SOUND HEALTH

Member
Jul 8, 2014
82
25
Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kimezindua operation maalumu inayojulikana kama operation mchwa kwa ajili ya kuhakikisha Ushindi wa kishindo unapatikana katika uchaguzi wa marudio wa madiwani kwenye kata ambazo imesimamisha wagombea.
SAU pia kimepokea wanachama wapya kutoka ACT Wazalendo akiwemo aliyepeperusha Bendera ya chama hicho kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Mkuranga Bwana Kunje Ngombale Mwiru.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni kwa wiki katika mkutano wa viongozi wa chama juu ya mabadiliko ya safu ya uongozi ngazi ya taifa mwenyekiti mpya wa SAU Bi. Bertha Nkango Mpata alisema usawa wa kijinsia ni miongoni kwa mambo ambayo SAU kinayapa kipaumbele.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa chama hicho BKisena Fred Kisena alisema SAU ina imani na tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) na kuishauri kusimamia uchaguzi wa marudio kwa Haki na kusimamia sheria. Lengo la SAU ni kujiimarisha na hatimaye kushika dola.
Kwa upande wake Kunje Ngombale Mwiru kwa niaba ya wanachama wenzake wapya alisema ameamua kuachana naACT -Wazalendo kutokana na kuwa na viongozi wabinafsi na wenye maamuzi ya kidikteta na kujiunga na SAU chama chenye sasa safi ili aweze kuwatumikia wananchi.

Chanzo: gazeti la Majira jumatatu 30 Julai 2018
 

Attachments

  • 1532959301193.jpg
    1532959301193.jpg
    55.4 KB · Views: 19
Back
Top Bottom