MWAMBIE BAHARIA WA UKWELI ASIKURUPUKE!!! hizi Zinaitwa LUGHA ZA MSIMU
Msimu ni
maneno yasiyo
sanifu yanayoanzishwa na kikundi cha watu wachache wenye
utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi. Kwa kawaida maneno hayo huzuka na kupotea, ila yale yanayodumu husanifiwa na kuwa
msamiati rasmi wa
lugha.
Chanzo
Mabadiliko ya
kihistoria yanaoikumba
jamii katika shughuli mbalimbali na miongoni mwa utu wa watu mbalimbali.
Kwanza ni matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii; matukio hayo yanaweza kuwa
vita,
njaa,
ukame na kadhalika. Misimu hiyo yaweza kuwa ni ya kubeza, kusifu na kukejeli.
Ya pili ni uwepo wa
matabaka, uwepo wa tofauti za kimaisha katika jamii fulani: kwa mfano, walalahoi ni
maskini na magambacholi ni wenye nazo.
Ya tatu ni
utani, utamaduni wa kutaniana. Jambo lingine linalosababisha kuzuka kwa misimu, msimu huu hubeba
kejeli na
dhihaka.
Ya nne ni
maendeleo ya
sayansi na
teknolojia: hayo pia huwa chanzo cha misimu;
vitu vipya vinavyojitokeza katika jamii vinadai uwepo wa maneno yanayozuka, kwa mfano,
bajaji na
digitali.
Sifa
- 1) Huzuka na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya jamii
- 2) Ni lugha isiyosanifiwa
- 3) Ni lugha ya mafumbo
- 4) Hupendwa na watu wengi kwa sababu hufurahisha
- 5) Ni lugha inayofahamika na watu wachache
- 6) Huwa na chumvi nyingi.
Aina za misimu
Katika misimu kuna aina tatu ambazo ni:
- 1) Misimu ya pekee: misimu hii huelezea uhusiano wa kikundi kidogo kwenye utamaduni mmoja ambayo huweza kuwa shule moja, mtaa mmoja, ofisi moja na kadhalika.
- 2) Misimu ya kitarafa: misimu hii huchukua eneo pana kidogo, kwa mfano kata, wilaya na hata mkoa.
- 3) Misimu zagao: misimu hii huenea karibu nchi nzima; wakati mwingine huvuka nchi