Chama cha Kilaghai Tanzania...

Mkuu ZeMarcopolo Hebu rekebisha kauli yako hapo nilipo weka Red ( Mfano wa watu waliomo kwenye kundi hili ni members wa jamiiforums ambao hurusha matusi kwa kila mtu anayehoji jambo juu ya chadema.) Sio wote Member wa Jamii Forums ni Wanachama wa chama

cha chadema au CCM Au CUF sisi Wengine hatuko katika Siasa zenu za Uchwara Siasa za Ki-Tanzania kama Timu za Mpira Simba na

Yanga hazina mpango wowote kugombea kula viongozi wote wanaotaka Uongozi hutumia hata nguvu ili mradi washinde na wapate

wanachokitaka. Mimi binafsi yangu ninapinga vyama vyote kuna ubinafsi na ufisadi ndani ya vyama vyote vya kisiasa nchini

Tanzania. Jirekebishe matamshi yako umezungumza vizuri unakuja kuharibu hapo penye Red asante.
 
Kiongozi Mzizimkavu,
Tafadhali yasome vizuri maneno hayo. Yanalielezea kundi maalum lenye tabia tajwa na sio kila member wa JF.
 
Kiongozi Mzizimkavu,
Tafadhali yasome vizuri maneno hayo. Yanalielezea kundi maalum lenye tabia tajwa na sio kila member wa JF.
Ungeliandika hivi Baadhi ya Member wa Jamii forums sio kuandika ( Mfano wa watu waliomo kwenye kundi hili ni members wa jamiiforums ambao hurusha matusi kwa kila mtu anayehoji jambo juu ya chadema.) Ukiandika neno kundi hili unamanisha mimi na wewe pia tumo katika hilo kundi hilo mkuu? Kiswahili lugha yetu mkuu.@ZeMarcopolo Kuna Tofauti kubwa ya kusema kundi hili na kusema Baadhi ya Member. Samahani kama nimekukwaza jaribu kunielewa vizuri.
 
wewe ni mlaghaiwa...
pole sana kwani inathibitisha ulivyohudhuria shule na bado hujaelimika.Unajifariji mwenyewe na kundi lako la akina mwigulu na nape.Njaa kitu kibaya sana sishangai hata wakati wa ubaguzi south afrika kulikuwa na wanafiki kama nyie waliowasaliti ndugu zao .Pole sana
 
Unajaribu kulaghai watanzania KINAPE zaidi,kwani NAPE ndiyo huwa na maneno mengi akitia nukta pumba tupu mwanzo mwisho.

Kama jana kaibuka huko eti ni Chadema wenyewe ndiyo wamerusha lile BOMU kwa tafsiri rahisi ni kwamba hata lile la kule KANISANI OLASITE ni MAASIKOFU au MAPADRI basi.Kwa kauli ya huyu mh. inajieleza kuwa kwenye mikusanyiko ambayo iliyokwishatokea mlipuko ya mabomu wahusika ni viongozi wa mikusanyiko hiyo husika.
Jamani ndg zanguni,!!.!!! WATANZANIA wa Leo sio wale wakuwadanganya kirahisi kama wale wa kipindi cha nyuma.Wewe endelea kutuambia hii mvua inayonyesha huku jua linawaka eti simba anazaa.Kuna walio wavivu wa kufikiri kama wewe watakubaliana nawe.
 
sijaona mantiki yako hapo sasa sijui unataka kuuaminisha nini umma wa kitanzania? sio kila mtu ANAKUA EASLY TAKEN na ujimga wako na usifanye kua watu wanachama wa CDM hawjitambui ila maskini walio CCM kimsingi ndio wenye akili....uko wrong!
 
Kwa maneno yako inaonyesha wanachofanya CHADEMA kisiasa wako sahihi. Kwa hayo wanayofanya CHADEMA inaonekana kuwa kuna kundi limeshishika ukuta na fimbo/hamsa zinacharazwa "pants down"
 

Swala la nepotism liko kila mahali. Hata wewe leo hii ukipewa cheo chochote iwe ni CCM,CHADEMA au Serikali ya CCM lazima uta-practice the same. That's nature. Mbona Watanzania hawasemi CCM ni chama cha KIDINI,KIDUGU au KIKABILA? Vigogo karibu wote wa CCM wamejaza ndugu zao kwenye chama, anza kwa Mama Kiwete,Riz,Kiwete, Dr.Hussein Mwinyi,Nepi Mosses Nnauye,Vita Kawawa,Lusinde,Wassira, Warioba,na wengineo.

Kikwete amejitahidi sana kuingiza Waislamu kwenye Serikali yake. Mbona Watanzania hawapigi kelele kuwa kuna udini na ukabila ndani ya CCM na Serikali yake???

CCM acheni propaganda za kishenzi.
 

Mdau si vyema kuzungumzia vitu usivyovijua ili mradi tu uonekane umeanzisha maada, hizo unazoleta ni prpaganda tu, na si vyema kurahisisha mambo kiasi hicho. Hii tabia ya kutoa maamuzi ya kuongea kwa kukurupuka itatugharimu watanzania jana mh. Lukuvi alikurupuka na sasa ameharibu hata uchunguzi kwa kuwa tayari majibu ya serikali yalitosha kuhitimisha uchunguzi tayari yanamuelekeo fulani wa kushutumu upande fulani kwa wenye akili tunajua nini kinachoendelea, wewe ccm hauijui tuulize sisi ndugu. watanzania tuache ulaghai dhambi ya uongo ni mbaya sana, tafakari sana haya vinginevyo tutazaa taifa la watu wasiofikiri.:shock:
 

umetoa maelezo mengi lakini nadhani yako biased, mm nisiye na chama chochote naomba nikukumbushe na kuomba ufafanuzi wa maelezo yafuatayo-

mfano kafulila ni mbunge wa NCCR mageuzi naye ameingiaje CDM kugombea uongozi

mm nijuavyo hata kabla ya Dr. Slaa kuamua kumuoa Mushumbusi, mushumbusi alikuwa analipwa kama mtaalamu na ndivyo hata ww pale ulipo kama ni mtaalam utakuwa unalipwa hivyo, je tatizo liko wapi? je sekta binafsi ina kiwango cha mishahara, mm nijuavyo, huwa ni uwezo wako wa kujiamini na kudai mshahara uutakao, kitakachokuweka ni utendaji kazi wako, kama ni mbovu utaondolewa mara moja

kila chama kina sera ya kukopeshana, mm naona tatizo la CDM ni kuweka wazi vitu vyao ndio maana mmevijua je vyama vingine hawakopeshani? lengo huwa ni kupunguza stress za viongozi katika kutatua matatizo yao ya msingi na kuwapa muda zaidi kutumikia chama,pia kulinda heshima zao, fikiria Rais Kikwete ukutane naye pale NMB/NBC akisubiri foleni ya kumuona Afisa mikopo ili amuhudumie, utajisikiaje? ni akili ya kawaida ambayo haina haja ya shule kubwa


kuhusu kupokea misaada wanayopokea cdm nakumbuka walitaja vyama vyote wanavyoshirikiana nao na viwango wanavyopokea, je vyama vingine havipokei mbona hawatuambia wanapokea sh na kutoka wapi?je endapo ujerumani baada ya kutajwa kuwa hawaisaidia cdm huoni kuwa nao huenda waliamua kutumia fursa hiyo kujitangaza kwa kutoa fedha kwa cdm, wakijua watu wengi wanaitizama cdm kama chama kinachoweza kuleta changamoto kwa ccm? hili nalo hulioni


mgawanyo wa ruzuku nadhani ulishawekwa hadharani na cdm, tatizo ruzuku ni ndogo, matokeo yake hata wakigawa kinachowafikia wale wa mwisho kinakuwa kidogo hakiwatoshi, je ww ulipo hela unayopewa au unayolipwa inatosheleza mahitaji yako, kama sivyo kwann usilalamike, ili wakuu wasikie

cdm kama ilivyo cuf/nccr mageuzi/ccm sio chama cha kilaghai ndio maana kina usajili halali na kikikosea kinaweza kufutwa. kumbuka laghai huwa hasajiliwi popote duniani

kuhusu akina mtela na wenzake, yawezekana nao walitaka madaraka, walivyonyimwa ndio wakaondoka cdm, lkn kashfa nyingine tunaambiwa walipewa kazi ya kufanya na chama kimojawapo ili kuhujumu cdm, cdm walipowatambua wakawafukuza, je huoni hawa nao wanaweza kuwa waganga njaa, je siku hizi unawasikia, je unafikiri watanzania bado wanawaamini tena kama zamani? wamekwishapuuzwa na heshima yao imeliwa na wageni kabisa

fedha za sabodo, watakuja wao kutueleza mchanganuo wake, lkn hizo nazo zinaweza kuwa propaganda za kuichafua cdm,

jengo la kupanga ofisi hatujui gharama zake, lkn je ccm ambayo ina majengo mengi yaliyojengwa na watz wote mbona hwatupi mapato na matumizi ya kukodisha majengo yetu kila mwaka, huoni hili nalo ni tatizo? kama hawa hawafanyi kwnn mnawalaumu cdm kutofanya

tenda ya ununuzi wa magari, mm nashukuru umetuongezea taarifa ambayo wengine hatukujua sababu halisi ya chris lukosi kuondoka cdm, huoni huyu naye alikuwa natafuta maslahi yake binafsi na siyo ya cdm. katk tenda mkishindaniswa wengi sio lazima ww ushinde, mwenzio anaweza kukushinda kwa kipengele kidogo mfano after sales service kama ww hukuweka. lkn nawachie cdm waje watueleze

Dr. Slaa kushiriki ufujaji wa fedha za maji za karatu,mm nisiye na chama nawashangaa wote, kama ushahidi upo, kwann serikali inaota kigugumizi kumfungulia mashitaka mahakamani wakati hilo ni kosa la jinai?

lete ushahidi jukwaani tuujadili, usipoleta tutkuhesabu kuwa ni mbeya na msengenyaji usiyefaa
 

Wewe kama hata hujui kwanini Kafulila alihama Chadema basi hili swala liko nje ya uwezo wako.
 
Wewe kama hata hujui kwanini Kafulila alihama Chadema basi hili swala liko nje ya uwezo wako.
kumbe mgonjwa si yule aliyefukuzwa na chadema uk sasa ni dhahiri wewe umemzidi yule mgonjwa hujijui hujitambui unatumia nyama za chini ya mgongo kufikiria( masaburi theory).
 
kumbe mgonjwa si yule aliyefukuzwa na chadema uk sasa ni dhahiri wewe umemzidi yule mgonjwa hujijui hujitambui unatumia nyama za chini ya mgongo kufikiria( masaburi theory).
zemarcopolo nitakutumia doze kwa dhl nipe address yako plz(siku wehu wakijitambua milembe itakuwa nursery school.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…