Chama cha ACT Wazalendo chaboresha safu ya uongozi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
KAMATI KUU YA ACT WAZALENDO YAFANYA UTEUZI WA KUBORESHA SAFU YA UONGOZI WA KITAIFA

Katika kikao chake cha kawaida cha siku mbili (tarehe 9 na 10 Juni 2019) kinachoendelea jijini Dar es salaam, Kamati Kuu ya Chama imefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kitaifa ili kuboresha safu ya uongozi wa kitaifa wa Chama.

Viongozi walioteuliwa na Kamati Kuu ni wafuatao;

A. Mshauri Mkuu wa Chama

Ndugu Maalim Seif Shariff Hamad

B. Wajumbe wa Kamati Kuu

1. Ndugu Theopista Kumwenda

2. Ndugu Mwajabu Dhahabu

3. Ndugu Fatma Fereji

4. Ndugu Eddy Riyami

C: Wenyeviti wa Kamati za Kitaifa

1. Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi:

Ndugu Nassor A. Marzurui

2. Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezi

Ndugu Salim A. Bimani

3. Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi

Ndugu Joram Bashange

4. Mwenyekiti wa Kamati ya Oganaizesheni, Mafunzo na Wanachama

Ndugu Mhonga Ruhwanya

5. Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati, Usimamizi na Ufuatiliaji

Ndugu Ismail Jussa

D: Makatibu wa Kamati za Kitaifa

1. Katibu wa Kamati ya Oganaizesheni, Mafunzo na Wanachama

Ndugu Shaweji Mketo

2. Katibu wa Kamati ya Katiba na Sheria

Ndugu Kulthum Mchuchuli

3. Katibu wa Kamati ya Uadilifu

Ndugu Mbarala Maharagande

4. Katibu wa Kamati ya Mikakati, Usimamizi na Ufuatiliaji

Ndugu Rachel Kimambo


Imetolewa na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT Wazalendo.

Tarehe 10 Juni 2019.
 
Kumbe Mhonga naye aliondoka chadema?! Anaweza kurudi bungeni mwakani viti maalum.
 
Kwahiyo ACT wazalendo ndio imeshamezwa na Cuf ya Zanzibar?!!

Naona Zitto hamuachi dada yake kila anakoenda!
 
Mark my words, ACT original itakufa kifo cha taratibu wakati CUF-ACT inachukua chama. Kuna wakati hata Zitto atafukuzwa ACT kwa utovu wa nidhamu. Subiri mtaona. Zitto hamjui huyu Maalim.
 
Mkuu umeona mbali Sana muda n mwalimu mzur Sana
Mark my words, ACT original itakufa kifo ha taratibu wakato CUF-ACT anachukua chama. Kuna wakati hata Zitto atafukuzwa ACT kwa utovu wa nidhamu. Subiri mtaona. Zitto hamjui huyu Maalim.
 
kuna cheo kinawekwa na mtu mmoja tu kwa kutumia mamlaka yake makubwa kuliko kamati kuu nzima. Kiongozi mkuu wa chama anamuweka mwenyekiti wa Chama na hakuna wa kuhoji.

Mama yetu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alikimbia hiko chama kwa demokrasia ya majaribio ambayo haiakisi uhalisia wowote
 
Back
Top Bottom