Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,032
- 828,826
Chakula ni ibada kamili, kisichezewe, kisitupwe, kisiharibiwe.
Chakula ni mojawapo ya mambo ambayo huileta familia pamoja na kujumuika wote, ni sehemu ambapo hufanyika sala na dua ya shukrani huku wakikumbukwa wale wote ambao hawakujaaliwa kupata mlo aidha kwa ugonjwa au kwa kukosa pesa nk. Chakula ni ibada kamili kwakuwa kilipitia hatua nyingi toka kupandwa kwake mpaka kukufikia wewe hapo mezani na ukajaaliwa kukila.
Chakula hakitupwi kwa namna yoyote ile labda kiwe kibovu na hakifai kuliwa, chakula ni kwa ajili ya faida ya mwili ili uweze kupata nguvu na afya za kumtumikia mungu wako na taifa na wote wenye uhitaji, chakula si ladha, ladha ni mdomoni tu. Mbwembwe zote za mapishi ni kwa ajili ya mdomo na ulimi wake basi!!! Kuna watu wana tabia ya kuagiza chakula kingi na kushindwa kukimaliza huu ni uharibifu na laana, wakati wewe unachezea chakula kuna mtu anahitaji japo robo tu ya hicho ili aweze kuishi tena!
Tukitunze na kukithamini chakula, tupo hivi tulivyo kwakuwa tunakula, chakula ni uhai na ibada kamil