Chakula: Kichocheo cha kuimarisha mahusiano mazuri ya familia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Familia bora ni ile ambayo inayoishi kwa upendo na amani, lakini ili ubora huo utimie wanafamilia wanahitaji muda wa kukaa pamoja na kuzungumza mustakabali wa maisha yao.

Familia inayotajwa hapa inajumuisha wazazi yaani baba na mama, pia watoto ambao wamejaariwa kuwa nao. Lakini kutokana na shughuli nyingi wana familia wanakosa muda wa kukutana pamoja.

Muda wa kukutana kwa wanafamilia ni muda maalumu ambao hauingiliani na shughuli nyingine yoyote. Kutokana na kukosa muda wa kukutana na watu wetu wa karibu tunajikuta tunafanya kazi kwa bidii lakini tunakosa furaha.

Kutokana na shughuli nyingi ambazo tunakuwa nazo kila siku, muda mzuri wa kukutana ni wakati chakula. Lakini sio familia zote ambazo hupata chakula pamoja.

Tafiti zinaonyesha kuwa familia ambazo zinakula chakula pamoja zinapata faida nyingi. Kula pamoja kunaimarisha mawasiliano na mahusiano ya watoto na wazazi. Watoto ambao wanakula chakula pamoja na wazazi wana nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika masomo yao na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao na kuhimili ushawishi wa makundi rika, unywaji wa pombe, matumizi ya dawa za kulevya na ngono. Pia wanajifunza jinsi ya kula mlo kamili tangu wakiwa wadogo mpaka wakifikia umri wa kujitegemea.

1.jpg

Huenda ni vigumu kula chakula pamoja na familia yako kwasababu ya mazoea uliyonayo ya kula ukiwa peke yako, fuata njia zifuatazo kukusaidia kupata chakula cha jioni na familia yako ili kuimarisha mahusiano

1. Wape uhuru wa kuchagua
Kama ni mzazi wape uhuru wana familia kuchagua chakula ambacho wangependa kula. Ukiwaruhusu watajisikia wanawajibika na wana maamuzi katika masuala muhimu ya familia.

2. Tengeneza ratiba ya Chakula
Kuwa na ratiba ya chakula ambayo inaainisha aina ya chakula ambacho familia inatarajia kula kila siku ni jambo jema. Watoto wanapenda mambo yaliyo kwenye mpangilio mzuri, kupitia njia hiyo unawajengea uwezo wa kufuata na kuheshimu ratiba kwa kila jambo wanalolifanya.

3. Gawa Majukumu
Kila mmoja ana nafasi ya kushiriki kuandaa chakula cha familia. Kama mzazi mpe majukumu kila mtu katika familia, mwingine anaweza kuandaa meza ya chakula, kuosha vyombo, ili mlo ukamilike utagundua kila mtu anawajibika kwa namna moja au nyingine. Maamuzi hayo yatasaidia kuimarisha uhusiano na watoto kufahamu majukumu yao.

4. Zingatia Muda
Ni vema muda wa kula ukapangwa ili wana familia wote wafahamu wakati sahihi wa wao kukutana mezani kwa ajili chakula. Watoto watafaidika kwa kujifunza umuhimu wa kuzingatia muda kwa kila jambo wanalofanya.

5. Ongeza vionjo vingine
Chakula kinapaswa kifurahiwe, ukiweka vionjo vya muziki, mazungumzo ya kufurahisha vyote vinaongeza hamasa ya wana familia kushiriki kikamilifu katika meza ya chakula. Huu sio wakati wa kuibua mambo mabaya au kauli za kuudhi ambazo zinalenga kumtenga mtu. Kila jambo na wakati wake.

Hata hivyo, hizi baadhi ya njia za kuimarisha mahusiano katika familia, lakini kila familia ina taratibu za kuendesha mambo yake na kujenga mstakabali mzuri.
 
Sio kweli bhana, utafiti wenu huo ni uongo mtupu, Kwanzaa Kwa taaarifa yako mkizoeana na watoto wako, heshima hupungua Kwa kiasi kikubwa Sana na kupelekea watoto kukuzoea na kukuona Kama Kaka yao, pia hupelekea watoto wengi kujiingiza katika matukio mabaya Kama vile umalaya, wizi na ujambazi pamoja na uhalifu mwingne, Mzazi Kama baba usizoeane saaana na watoto wako kila Mara mko pamoja had msosi mko pamoja, muache kuiga mambo ya kizungu wale wenzetu wako mbali Sana
Utashindwa kuheshimika na watoto watakudharau na watafanya mambo ya ovyo kabisaaa, ebu fanyeni utafiti hata Kwa watoto wa wakubwa au watoto wa vigogo utagundua, Mzazi hasa baba lazima kuwa na mipaka na watoto wako kwa faida ya maisha ya baadae ya wanao, achaneni na kuwaiga wazungu watoto wa kitzt hawawez hayo kutokana na tamaduni zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
beth: huwajui watoto wa kisasa. Ukiwaambia wachague chakula, watataka chips tu mwanzo mwisho.

Aliye like huu upupu ana tatizo mahali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
beth: huwajui watoto wa kisasa. Ukiwaambia wachague chakula, watataka chips tu mwanzo mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchaguzi unaendana na a, b au c. Kimsingi waafika wengi jambo la kula pamoja siyo utamaduni wa wengi na unaweza kukuta watoto/wanawake wanaona aibu kula na wanaume. Huu ni utamaduni ambao tunatakiwa tuutokomeze na tuige kula kama wazungu. Mimi binafsi huwa nafurahi sana tunapokula pamoja wakati wa chakula.
 
Mkuu, umeandika madudu, samahan lakin
Sio kweli bhana, utafiti wenu huo ni uongo mtupu, Kwanzaa Kwa taaarifa yako mkizoeana na watoto wako, heshima hupungua Kwa kiasi kikubwa Sana na kupelekea watoto kukuzoea na kukuona Kama Kaka yao, pia hupelekea watoto wengi kujiingiza katika matukio mabaya Kama vile umalaya, wizi na ujambazi pamoja na uhalifu mwingne, Mzazi Kama baba usizoeane saaana na watoto wako kila Mara mko pamoja had msosi mko pamoja, muache kuiga mambo ya kizungu wale wenzetu wako mbali Sana
Utashindwa kuheshimika na watoto watakudharau na watafanya mambo ya ovyo kabisaaa, ebu fanyeni utafiti hata Kwa watoto wa wakubwa au watoto wa vigogo utagundua, Mzazi hasa baba lazima kuwa na mipaka na watoto wako kwa faida ya maisha ya baadae ya wanao, achaneni na kuwaiga wazungu watoto wa kitzt hawawez hayo kutokana na tamaduni zetu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli bhana, utafiti wenu huo ni uongo mtupu, Kwanzaa Kwa taaarifa yako mkizoeana na watoto wako, heshima hupungua Kwa kiasi kikubwa Sana na kupelekea watoto kukuzoea na kukuona Kama Kaka yao, pia hupelekea watoto wengi kujiingiza katika matukio mabaya Kama vile umalaya, wizi na ujambazi pamoja na uhalifu mwingne, Mzazi Kama baba usizoeane saaana na watoto wako kila Mara mko pamoja had msosi mko pamoja, muache kuiga mambo ya kizungu wale wenzetu wako mbali Sana
Utashindwa kuheshimika na watoto watakudharau na watafanya mambo ya ovyo kabisaaa, ebu fanyeni utafiti hata Kwa watoto wa wakubwa au watoto wa vigogo utagundua, Mzazi hasa baba lazima kuwa na mipaka na watoto wako kwa faida ya maisha ya baadae ya wanao, achaneni na kuwaiga wazungu watoto wa kitzt hawawez hayo kutokana na tamaduni zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Dunia ya sasa ukishindwa kuwa karibu na wanao tegemea tamthilia, dada wa kazi, social media na mabazazi ya mtaa yatamfundisha mambo ambayo ulishindwa kuwafundisha. Una mtoto wa kiume na hutaki kuwa karibu nae, atajifunza wapi kuwa mwanaume ???... au unasubiri hadi iwe too late PATHETIC
 
Familia bora ni ile ambayo inayoishi kwa upendo na amani, lakini ili ubora huo utimie wanafamilia wanahitaji muda wa kukaa pamoja na kuzungumza mustakabali wa maisha yao.

Familia inayotajwa hapa inajumuisha wazazi yaani baba na mama, pia watoto ambao wamejaariwa kuwa nao. Lakini kutokana na shughuli nyingi wana familia wanakosa muda wa kukutana pamoja.

Muda wa kukutana kwa wanafamilia ni muda maalumu ambao hauingiliani na shughuli nyingine yoyote. Kutokana na kukosa muda wa kukutana na watu wetu wa karibu tunajikuta tunafanya kazi kwa bidii lakini tunakosa furaha.

Kutokana na shughuli nyingi ambazo tunakuwa nazo kila siku, muda mzuri wa kukutana ni wakati chakula. Lakini sio familia zote ambazo hupata chakula pamoja.

Tafiti zinaonyesha kuwa familia ambazo zinakula chakula pamoja zinapata faida nyingi. Kula pamoja kunaimarisha mawasiliano na mahusiano ya watoto na wazazi. Watoto ambao wanakula chakula pamoja na wazazi wana nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika masomo yao na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao na kuhimili ushawishi wa makundi rika, unywaji wa pombe, matumizi ya dawa za kulevya na ngono. Pia wanajifunza jinsi ya kula mlo kamili tangu wakiwa wadogo mpaka wakifikia umri wa kujitegemea.

Huenda ni vigumu kula chakula pamoja na familia yako kwasababu ya mazoea uliyonayo ya kula ukiwa peke yako, fuata njia zifuatazo kukusaidia kupata chakula cha jioni na familia yako ili kuimarisha mahusiano

1. Wape uhuru wa kuchagua
Kama ni mzazi wape uhuru wana familia kuchagua chakula ambacho wangependa kula. Ukiwaruhusu watajisikia wanawajibika na wana maamuzi katika masuala muhimu ya familia.

2. Tengeneza ratiba ya Chakula
Kuwa na ratiba ya chakula ambayo inaainisha aina ya chakula ambacho familia inatarajia kula kila siku ni jambo jema. Watoto wanapenda mambo yaliyo kwenye mpangilio mzuri, kupitia njia hiyo unawajengea uwezo wa kufuata na kuheshimu ratiba kwa kila jambo wanalolifanya.

3. Gawa Majukumu
Kila mmoja ana nafasi ya kushiriki kuandaa chakula cha familia. Kama mzazi mpe majukumu kila mtu katika familia, mwingine anaweza kuandaa meza ya chakula, kuosha vyombo, ili mlo ukamilike utagundua kila mtu anawajibika kwa namna moja au nyingine. Maamuzi hayo yatasaidia kuimarisha uhusiano na watoto kufahamu majukumu yao.

4. Zingatia Muda
Ni vema muda wa kula ukapangwa ili wana familia wote wafahamu wakati sahihi wa wao kukutana mezani kwa ajili chakula. Watoto watafaidika kwa kujifunza umuhimu wa kuzingatia muda kwa kila jambo wanalofanya.

5. Ongeza vionjo vingine
Chakula kinapaswa kifurahiwe, ukiweka vionjo vya muziki, mazungumzo ya kufurahisha vyote vinaongeza hamasa ya wana familia kushiriki kikamilifu katika meza ya chakula. Huu sio wakati wa kuibua mambo mabaya au kauli za kuudhi ambazo zinalenga kumtenga mtu. Kila jambo na wakati wake.

Hata hivyo, hizi baadhi ya njia za kuimarisha mahusiano katika familia, lakini kila familia ina taratibu za kuendesha mambo yake na kujenga mstakabali mzuri.

Jr
 
Chakula ni ibada bora kabisa, naweza kukosa kusali siku nzima ila sio wakati wa kula.... napenda kula pamoja sio tu meza moja bali ‘sinia’ moja (wale wa kwetu tunaelewana).

Nachukia sana mtu kusaza chakula kwa sahani, hasa kama kajipakulia mwenyewe.

Jesus saves, I spend.
 
Back
Top Bottom